Channel Ten: Mchungaji Antony Lusekelo azungumzia Kuchinja!

Status
Not open for further replies.
Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa hivi. Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.

Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.

Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tanu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".

Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.

Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.

huyu si mfuasi wa Yesu ni mfanyabiashara wa injili, mkristo wa kweli hawezi kula nyama iliyotolewa sadaka kwa shetani, shwari la kujiuliza ni nani shetani kati ya Yesu na allah ?
 
[FONT=lucida grande, tahoma, verdana, arial, sans-serif]Amesema vema mchungaji, hata waislamu huwa wanakuja kununua Nguruwe kwenye mabucha ya kikristo...pote pote tunapata nyama![/FONT]
 
Mzee wa upako ni mchungaji au ni mjasiriamali kwa upenyo wa dini?

1Kor 10:25-29 Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni,bila kuuliza uliza,kwaajili ya dhamiri, maana dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.Na mtu asiyeamini akiwaalika,nanyi mnataka kwenda,kuleni kila kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza,kwa ajili ya dhamiri.Lakini mtu akiwaambia,kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka,msile kwa ajili yake yeye aliyeonyesha na kwa ajili ya dhamiri.Nasema dhamiri lakini siyako bali ya yule mwingine,Maana kwanini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?
 
huwa namuona hana maana lakini leo nilipo mkuta anazungumzia swala hilo nikasema ngoja nimsikilize hakika amesema vema naamini wakristo hatuta ngangania kuchinja tena lakini serikali ifute kauli kuwa waislam ndiyo wenye haki ya kuchinja...

Tehteh! Alikuwa rafiki mkubwa wa Sheikh yahaya.
 
Tatizo la huyo bwana upako anasoma biblia kwa kuchomoa chomoa vifungu kama anavyofanya Makinda na Ndugai kule bungeni na Kanuni zao za bunge.
 
Huyu Lusekelo nae si Mchumia Tumbo tu? Kwa Magamba yupo Kwa Waislamu yupo! Anachotafuta huyu ni Kuvutia Wateja Kanisa kwake,ili aendelee Kuwavuna!!
Hana tofauti na Mleta hii Mada, anaejitambulisha kuwa yeye sio Mkristo bali Muislamu! Ulitegemea amkosoe Lusekelo,wakati anawatetea hawa "Wauaji"! Kama Lusekelo anapenda Haki mbona hazungumzii kuhusu Waislamu kuchinja pia Nguruwe?
Si huyu huyu Mwizi wa Sadaka aliwahi kusema eti KIKWETE aachwe kuandamwa ili afanye kazi zake Vizuri? Leo anaweza kutuambia nini baada ya KIKWETE kuachwa na Hatimae leo,Uongozi Umemshinda, Udini umepamba Moto!! Makanisa yanachomwa Moto, Wachungaji na Mapadri wanauawa, Wanafunzi Kidato cha Nne 94% Wanafeli,Na Mengine mengi!

Je Lusekelo anamtumikia Mungu gani aliyeshindwa kumuonyesha haya yanayo tokea leo?
Apeleke Utapeli wake huko! Kwani hatujui kua lazima ajipendekeze kwa KIKWETE angalao kama nayeye atapewa Ubunge wa Kuteuliwa kama Tapeli mwenzake Getrude Lwakatare!
Waache kuwaibia kwanza wananchi ndio tuweze kumwamini kuwa anamtumikia Mungu!
Watu wametoka kwenye Misingi ya Kufundisha watu neno la Uzima,na kwamba Watubu na Kuokoka,! wao ni kuwafundisha tu,mambo ya Utoaji! Utafikiri Mungu hawapendi wasiotowa Pesa!
Mungu awasamehe sana!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!
 
hivi unaweza kutoka ofcn na tai na shati jeupe na tai yako uangaike kuchinja hata mm naona tuwa achie hiyo ajira wao kila hoteli umuajiri mmoja wao na kila nyumba pia kwa ajili ya kuchinja
 
Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.
Ushabiki ni hatari sana
1. Mafundisho mtu mmoja hayawezi kuwa Imani sahihi ya Kikristo. Imani sahihi ipo katika neno la Mungu yaani Biblia. Tofauti na hivyo, unataka tuamini kuwa anayosema Ustaadhi Ilunga, au Sheikh Pondo, au magaidi wengineo wengi kwa majina ya sheikh ndio Imani sahihi ya Kiislam. Pengne hii itaeleza yanayotoke Syria, Somakia nk

2. Kwa sababu ya mtu mmoja kusema unachopenda kusikia basi unataka wote wawe hivyo!!! It can't be possible, msingi ni mmoja tuu, Yesu Kristo!

3.Kuhusu kuchinja nyumbani kwetu tumekuwa na vijana wa kiislam.Kwa upendo, tumekuwa tukiacha kitimoto na hata kuchinja tumekuwa tukiwaruhusu kwa upendo ili wale mana vinginevyo hawatakula nyama na hawataweza kudai haki ya kuchinja kwangu. Huu ndio upendo wa Kikristo! Kosa hawa wasiokuwa na hekima kusema kuchinja ni haki ya waislam. Hilo, kwa vyovyote vile, halikubaliki!
 
amjaacha 2 mambo ya kuchinja wajameni? Nchi inamatatizo lukuki mnakomaa na kuchinja.
 
Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa hivi. Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.

Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.

Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".

Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.

Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.

Mtume Mohamad alipokimbilia Medina baada ya kukataliwa na watu wa Mecca, pale aliwakuta wayahudi na wakristo. walimpokea na kujenga urafiki mkubwa naye. Walishirikiana kindugu na watu wa Medina walimkubali. Alipopata nguvu kijeshi na kiutawala aliwataka wajiunge naye kwa lazima. Waliokataa aliwaua bila kujali kuwa hawa awali walikuwa rafiki zake. Hiyo ndiyo mikakati ya Jihad. Siku moja Lusekelo ataja gundua kuwa lengo halikuwa kuchinja bali dini gani itakayokuja kuzitawala na kuzitiisha dini zingine zote. Na hapo itakuwa tooo late!!!!
 
Ukiniona MZIMU nimemkubali Mtu, jua huyo mtu anastahili. Jamani kwa watu wenye akili, hakuna suluhu nyengine itakayo linda Amani ya Nchii hii zaidi ya hiyo alioitoa Mchungaji Antony Lusekelo. Kwani hayo hayo ndio anayo yaongelea Mzee Pinda na Mzee Steven Wasira.

Kama kuna mkristo yoyote anapingana na huyu mchungaji, hakika huyo ndio asie itakia Mema Nchi hii.
 
nimewahi kusikia haya kwenye mahubiri ya wa Upako kupitia channel ten "nina magari sita siyo ya japan, nina Range Rover sport, nina BMW X5, nina Landrover Discovery....nikiamka asubuhi naangalia kwenye parking niendeshe lipi!!! halafu nilivyo na mkwara kwenye gari nakua peke yangu, kama wewe unakuja kanisani kwangu na haujafanikiwa umekaa mwaka wa kwanza,wa pili na haujanunua usafirii! basi wewe hutoi dhaka, hutoi fungu la kumi ndo maana hufanikiwi, Yesu hakutembea na malofa...."~Mzee wa upako aka SMG, ha ha haaaa.
 
Mtume Mohamad alipokimbilia Medina baada ya kukataliwa na watu wa Mecca, pale aliwakuta wayahudi na wakristo. walimpokea na kujenga urafiki mkubwa naye. Walishirikiana kindugu na watu wa Medina walimkubali. Alipopata nguvu kijeshi na kiutawala aliwataka wajiunge naye kwa lazima. Waliokataa aliwaua bila kujali kuwa hawa awali walikuwa rafiki zake. Hiyo ndiyo mikakati ya Jihad. Siku moja Lusekelo ataja gundua kuwa lengo halikuwa kuchinja bali dini gani itakayokuja kuzitawala na kuzitiisha dini zingine zote. Na hapo itakuwa tooo late!!!!

Haya ni yako wewe ndugu yangu na Uongo ulio dhahiri.

Usitake kuvunja Busara Nzuri alio ionyesha Mzee wa Upako. Jamani sisi Waislamu na Wakristo hatuna sababu ya kuishi kama maadui.

Kwa busara, mtu akikujia hatua moja kwa amani, wewe enenda hatua zaidi kwakwe kwa amani pia.

Mashetani wa Nchi hii utawaona tu. Wao wangependa kuona Waislamu na Wakristo hawaishi kama zamani.
 
Ushabiki ni hatari sana
1. Mafundisho mtu mmoja hayawezi kuwa Imani sahihi ya Kikristo. Imani sahihi ipo katika neno la Mungu yaani Biblia. Tofauti na hivyo, unataka tuamini kuwa anayosema Ustaadhi Ilunga, au Sheikh Pondo, au magaidi wengineo wengi kwa majina ya sheikh ndio Imani sahihi ya Kiislam. Pengne hii itaeleza yanayotoke Syria, Somakia nk

2. Kwa sababu ya mtu mmoja kusema unachopenda kusikia basi unataka wote wawe hivyo!!! It can't be possible, msingi ni mmoja tuu, Yesu Kristo!

3.Kuhusu kuchinja nyumbani kwetu tumekuwa na vijana wa kiislam.Kwa upendo, tumekuwa tukiacha kitimoto na hata kuchinja tumekuwa tukiwaruhusu kwa upendo ili wale mana vinginevyo hawatakula nyama na hawataweza kudai haki ya kuchinja kwangu. Huu ndio upendo wa Kikristo! Kosa hawa wasiokuwa na hekima kusema kuchinja ni haki ya waislam. Hilo, kwa vyovyote vile, halikubaliki!

Kwanza kabisa hao Mashekhe Ulio wataja sio Magaidi. Gaidi ni Mkristo kama wewe unae hubiri chuki.

Pili kama unafikiri kuna suluhu nyengine zaidi ya hiyo, ni bora ukaanza kuchimba handaki.
 
huyu si mfuasi wa Yesu ni mfanyabiashara wa injili, mkristo wa kweli hawezi kula nyama iliyotolewa sadaka kwa shetani, shwari la kujiuliza ni nani shetani kati ya Yesu na allah ?

Mimi nadhani Swali zuri kujiuliza hapa ni hili, Nani ni Binadamu na nani ni Mungu?.
 
Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa hivi. Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.

Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.

Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".

Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.

Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.

sawa lkn achen kukashifu ukristo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom