Channel Ten: Mchungaji Antony Lusekelo azungumzia Kuchinja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Channel Ten: Mchungaji Antony Lusekelo azungumzia Kuchinja!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MZIMU, Feb 20, 2013.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,067
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa hivi. Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.

  Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.

  Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".

  Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.

  Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2013
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hakuna taarifa yoyote uliyotoa hapo, kajipange upya.
   
 3. chipa GM

  chipa GM JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2013
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 1,110
  Likes Received: 1,153
  Trophy Points: 280
  mzee wa upako anasema waislamu ndo wachinje.
   
 4. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #4
  Feb 20, 2013
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 0
  Kwenye kipindi kilicho rushwa na chaneli ten mzee wa Upako ameonyesha kushangazwa na viongozi wa kikristo wanao ng'ang'ania kuchinja. Amesema ""nawashangaa sana wachungaji wenye hoja za kipumbavu eti nani achinje"

  "Wanamsumbua waziri mkuu eti kujadili nani achinje wakati nchi ina matatizo lukuki, kwani waislamu walipo kuwa wana chinja ilikuwaje?"

  Akaendelea kusema "Tuombee amani tuache hoja za kijinga eti nani achinje nani asichinje".

  Aliongea mengi kuonyesha namna ambavyo amani yetu inaweza kutoweka kwa ajili ya mawazo ya kijinga! Amewaomba wakristo kusoma Warumi 14 mstari 1 na 31.

  Naomba mwenye biblia atuweke mstari huo unasemaje.
   
 5. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,067
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  OK. Sinkala, nimezingatia comment yako, unaweza kuipitia tena hiyo thread hapo juu.
   
 6. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2013
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Jamaa mjanja sana, anasema hivyo kwa kuwa kuna waisilamu wengi sana wanaohudhuria kanisani kwake kupewa upako, hasa wakina mama, so ni aina fulani ya kuvutia wateja!
   
 7. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2013
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,892
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mchungaji Antony Lusekelo ( Mzee Wa Upako) amesema kuwa Maaskofu na Wachungaji Mwanza na Mbeya wanaotaka wapewe haki ya Kuchinja ni Wapumbavu.Amewataka Wakristo wote waelewe kuwa kazi ya kuchinja wanyama ni ya Waislamu. Hivyo amewataka Waislamu Waendelee Kuchinja ili kuepusha Vurugu!!!Mchungaji Lusekelo ametoa namba yake ya simu 0713 725473 kwa yoyote mwenye kutaka maombi na upako!!!
  Kampeni hizi zimepangwa kurushwa katika kipindi Channel ten siku ya jumamos ijayo:
  Tujiweke tayari Kusikiliza na kujibu hoja:

  Kwa ujumula wake Mzee wa upako ameungana na Askofu Gamanywa wa Wapo Mission ambaye naye anataka suala hilo limalizwe kwa kuwachia waislamu.

  Kumbukumbu za Uhamiaji zinaonyesha kuwa Askofu Gamanywa si Raia wa TZ ila mke wake ni raia. Miaka ya Nyuma alifuatiliwa sana na uhamiaji mpaka aliposhauriwa na Watu fulani kujiunga na CCM.

  Kwa upande wa Mzee wa Upako yeye ni raia tena kutoka Mbeya , aliyemleta hapa DSM ni Askofu Mwasota na alimtoa huko wakati anavuta bangi. Aliingia Dar na kufanya kazi chini ya Akofu Mwasota lakini ghafla alipindua huduma hiyo na kujiita Mzee wa upako huku akiwa hatambui uongozi wa PCT hadi sasa.

  Katiak hali ya Kushangaza Mzee wa Upako hajui kuandika lakini anajua kusoma. Alianza kujipenyeza kwa wazungu na alisafili hadi Uk. Alipofika huko alifanikiwa kuingiza mataili 250 kwa wizi wa msamaha wa kodi .
  Taarifa za TRA zinaonysha kuwa alikamatwa Bandarini wakati wa kipindi cha kwanza cha urais wa Kikwete na suala hilo lilimalizwa kwa kukubaliana kuwa Mzee wa Upako atakuwa anamuunga Kikwete hadi kifo kimikute.

  Katika kipindi cha kujivua gamba Mzee wa Upako aliasi kambi ya Kikwete na kuanza kumuunga Lowassa na alipopata Kipigo amerudi tena huko huko CCM.
  My Take:
  Viongozi wa dini wananunuliwa na CCM Kupotosha Umma:
   
 8. Root

  Root JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2013
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 23,780
  Likes Received: 9,776
  Trophy Points: 280
  Receive one who is weak in the faith, but not to disputes over doubtful things. Roman 14:1
   
 9. Root

  Root JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2013
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 23,780
  Likes Received: 9,776
  Trophy Points: 280
  Romans 14 haina verse 31
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2013
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,162
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 280
  huwa namuona hana maana lakini leo nilipo mkuta anazungumzia swala hilo nikasema ngoja nimsikilize hakika amesema vema naamini wakristo hatuta ngangania kuchinja tena lakini serikali ifute kauli kuwa waislam ndiyo wenye haki ya kuchinja...
   
 11. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2013
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,813
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  Huyu anayejiita mzee wa UPAKO a.k.a mchungaji wa matukio hana wauumini wowote wale bali washabiki toka madhehebu mbali mbali, wenye hekima wanaijua biashara yake na hawana muda wa kumsikiliza.
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2013
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,856
  Likes Received: 1,919
  Trophy Points: 280
  Rumi 14:1 Mkaribisheni yeye ambaye imani yake ni dhaifu, lakini si kwa kugombana na kubishana juu ya mawazo yake
  rumi 14:31 haipo, inaishia 23 tu.
   
 13. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #13
  Feb 20, 2013
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 0
  1-Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.-
  2-Watu huhitilafiana: mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu; lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani.-
  3-Mtu ambaye hula kila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kula kila kitu; naye ambaye hula tu mboga za majani asimhukumu anayekula kila kitu, maana Mungu amemkubali.-
  4-Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
  5-Mtu anaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maana zaidi kuliko nyingine; mtu mwingine aweza kuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja na afuate msimamo wa akili yake.-

  6-Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.-

  7-Maana hakuna mtu yeyote miongoni mwetu aishiye kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe-

  8-maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana.-

  9-Maana Kristo alikufa, akafufuka ili wapate kuwa Bwana wa wazima na wafu.

  10-Kwa nini, basi wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe,

  kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele

  ya kiti cha hukumu cha Mungu.

  11-Maana Maandiko yanasema: "Kama niishivyo, asema Bwana kila mtu atanipigia magoti,

  na kila mmoja atakiri kwamba

  mimi ni Mungu."

  12-Kwa hiyo, kila mmoja

  wetu atatoa

  hoja yake mbele

  ya Mungu.

  13-Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo

  kwa ndugu yetu au kumsababisha aanguke katika dhambi.-

  14-Katika kuungana

  na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi

  kwa asili yake; lakini, mtu akidhani kwamba kitu fulani

  ni najisi, basi, kwake huwa najisi.-

  15-Kama ukimhuzunisha ndugu yako

  kwa sababu

  ya chakula unachokula, basi mwenendo wako hauongozwi

  na mapendo. Usikubali hata kidogo chakula chako kiwe sababu

  ya kupotea

  kwa mtu mwingine ambaye Kristo alikufa

  kwa ajili yake!-

  16-Basi, msikubalie kitu mnachokiona

  kuwa kwenu

  ni kitu chema kidharauliwe.-

  17-Maana Utawala

  wa Mungu si shauri la kula

  na kunywa, bali unahusika

  na kuwa na uadilifu, amani

  na furaha iletwayo

  na Roho Mtakatifu.-

  18-Anayemtumikia Kristo namna

  hiyo humpendeza Mungu,

  na kukubaliwa

  na watu.-

  19-Kwa

  hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani,

  na yanayotusaidia kujengana.-

  20-Basi, usiiharibu kazi

  ya Mungu

  kwa sababu

  ya ubishi juu

  ya chakula. Vyakula vyote

  ni halali,

  lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya mtu aanguke katika dhambi.-

  21-Afadhali kuacha kula nyama, kunywa divai, au kufanya chochote ambacho chaweza kumsababisha ndugu yako aanguke.-

  22-Basi, shikilia unachoamini kati yako

  na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.-

  23-Lakini mtu anayeona shaka juu

  ya chakula anachokula, anahukumiwa

  kama akila,

  kwa sababu msimamo

  wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho

  na msingi wake katika imani

  ni dhambi.

  ?
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2013
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Mimi nitakuwa najichinjia! Siwezi kutumia kitoweo kilichochinjwa na waislam. Labda kama ni kitimoto
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2013
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,856
  Likes Received: 1,919
  Trophy Points: 280
  Tatizo hakuruhusu maswali. ningekutuma umwulize hili:

  1kor 10:27 Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kila kitu kitakachowekwa mbele yako bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini kama mtu ye yote akikuambia, "Hiki kimetolewa kafara kwa sanamu," basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri.

  ndugu Mohamedi Mtoi shida ipo hapo kwenye red, na tatizo limekuwa kubwa baada ya waislam kutangaza wazi kuwa kuchinja ni ibada. Ibada ya namna hiyo kwa mkristo ilisha komeshwa na ujio wa YESU KRISTO. Thus kula nyama iliyochinjwa kwa minajili ya Ibada, ni sawa na wewe umeshiriki ibada ile. Hii hairuhusiwi pamoja na kwamba tumeagizwa upendo.

  Onyo, Mohamedi Mtoi, wewe ni kati ya watu wanaoheshimika sana hapa JF. Angalia uzi huu ulioanzishwa usije kukushua heshima.
   
 16. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2013
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,193
  Trophy Points: 280
  Ewe mktistu mwenzangu jiulize swali moja tu "je ukila nyama iliyochinjwa na muislam imani yako inaathirika?". Hata maandiko yanatuelekeza kiingiacho si haramu bali kitokacho ndani ya nafsi ya mtu.
  Ni suala la busara tu kuwa hawa wenzetu imani yao imewabana katika hilo, basi tuwaheshimu na tuwaachie kazi hiyo iwe yao. Lakini vilevile nao waweke ustaarabu kutambua kuwa kuchinja sio haki yao bali ni utamaduni tu uliochangiwa na kuishi pamoja kwa kuheshimiana.
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2013
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,856
  Likes Received: 1,919
  Trophy Points: 280
  ni kati ya double agents wengi hapa nchini.
   
 18. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2013
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,122
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Wagalitia kazi mnayo!
   
 19. Kyenju

  Kyenju JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2013
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 4,574
  Likes Received: 269
  Trophy Points: 180
  Kwani LUSEKELO ni nani, na ana title gani kwenye ukristo mpaka awasemee wakristo. Nafikiri ni maoni yake na kanisa lake.
   
 20. don12

  don12 JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2013
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 657
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  huyu jamaa naye ni mchungaji?huwa anajipendekeza kwa serikali asidaiwe kodi,.kuna taasisi gani anayomiliki inayosaidia watanzania?mimi nimezoea kuona anajigamba tu kuwa ana magari mapya ana ulinzi lkn huwa haelezi anavipata pata je,kadhalika na wafuasi wake hivyo hivyo.ifike mahali manabii hawa wa uongo wachunguzwe kama ni madrag dealer au la.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...