Channel 10 Live: Jenerali on Monday

Hv iki kipindi kina marudio siku za weekend,maana mmeponda mpaka nimecheka usiku huu .
Natamamani kukiona hivi huwa wana-upload vipidi vyao ili tuone wengine tupo mbali na TV
 
Hakuna watu wachovu nchii hii kama waandishi habari....hawasomi....wanaona wanajua kila kitu kwenye jamiii
 
Tunahitaji waendesha vipindi vya mahojiano kama Jenerali Ulimwengu. Akija mtu kama mtu aina ya Simalenga anapigwa maswali kama ya Ulimwengu ili ajiaibishe mwenyewe.

Leo mimi nilikuwa naangalia kipindi kama hicho kuhusu muungano wenye muundo wa serikali 3 kwenye kipindi cha agenda 2015 startv ilikuwa vituko vitupu. Waendesha kipindi DOTO BULENDU kituko na mwenzake Mpangala kituko. Nimeamini Startv haina waandishi wenye maarifa kwa maana wenye uwezo mkubwa kielimu. Wageni wao walikuwa ndg Mkinga, mpayukaji na ndg Alikazi mwandishi wa habari radio moja huko shinyanga. Watu ni kama wanaandaliwa vipindi kuja kupotosha watanzania kwa sababu badala ya kujadili rasimu wanamjadili mzee Warioba. Watu wa aina hii ni hatari.

Nawapongeza waandishi kama Ulimwengu na Dr. Ryoba. Tatizo la watangazaji aina ya DOTO wa startv ni kutojisomea mambo mbalimbali nje ya taaluma zao ili kujiongezea maarifa.
 

Na huyu jamaa nilishawahi kumsikia ana mpango wa kugombea ubunge mwakani huko kwao Njombe, akipita siku moja anapewa uwaziri!
 
Uyu jamaa si alikuaga msanii wa Kaole au macho yangu?
 
Uyu jamaa si alikuaga msanii wa Kaole au macho yangu?

Napata taabu kuelewa, inakuwaje watu wenye uwezo mdogo kiasi hichi wapewa nafasi kwenye kipindi kama Jenerali on Monday. Vipindi hivi kuhusu rasimu ya pili ya katiba tunahitaji watu wenye uwezo kwa maana ya uchambuzi kwa ajili ya kutoa elimu ya uraia kwa watanzania. Lkn sio watu wanaeneza maneno ya kupika uzushi kwa watz.
 
Nimeshangaa sana...huyu anakuwaje mwandishi wa habari??Yaani Taifa hili limeingiliwa....ili upate vyeo,msingi lazma uwe kilaza na mnafiki kwa watawala...huyu jamaa sifa anazo!!! Aibu sana...jitu linajiumauma bila facts...
 

Ndg yangu joely, taifa hili kama ni janga lililotukumba ni waandishi wa habari! Kitu ambacho nimegundua ni kwamba tunawashika peni na notebook sio waandishi wa habari. Kama ni waandishi tunao wachache sana. Waandishi wengi ukitaka kujua ubovu wao waambie wachangie mada zilizo nje ya taaluma yao. Wengi wana uwezo mdogo sana. In short they are not well informed. Hawasomi kabisa...inawezekana vipi mwandishi anamhoji mtu maswala ya rasimu ya katiba wakati yeye hajaisoma hata kidogo! Nimeshuhudia mara nyingi kwa waandishi wa startv anaendesha kipindi kuhusu rasimu ya katiba unamuona kabisa mwandishi huyu hajaisoma rasimu kabisa. Ni aibu....watu wanajua kukaa kwenye TV that is it. Nchi hii bado tuna safari ndefu sana. Lkn leo tumeshuhudia kwamba wale wanaopotosha wakikutana na waandishi mahiri wasomi kama Jenerali Ulimwengu watajuta kwani pamoja na kupotosha kwao watakumbana na maswali yenye kufikirisha bila kutoa yanayojitosheleza, aibu itakula kwako!!
 

Mkuu,picha zinajieleza,kama Juma Nkamia kashamuona mwenye mbwa anayefanya mbwa abwake bwake hovyo!! Clouds siku hizi imekuwa kama radio Uhuru,naanza kuamini kuwa wamesaini MoU na CCM kuelekea 2015 kwa kufanya indirect propaganda kwa kuwalenga Vijana!!!
 
Huyu jamaa alikuwa kwenye mchezo wa kuigiza wa kaole .jina lake la kisanii ni dumelo .ni mtoto sana kuhusu maswala haya .ni mtoto wa kupakatwa that's what I can say .nina maana ametumwa

dah! Nampata huyo. Kumbe ndiye simalenga?
 
Huyu jamaa alikuwa kwenye mchezo wa kuigiza wa kaole .jina lake la kisanii ni dumelo .ni mtoto sana kuhusu maswala haya .ni mtoto wa kupakatwa that's what I can say .nina maana ametumwa

Mimi sikutaka kuendelea kumwangalia kwa maana nilidhani anaigiza kama mjinga wa kutokufahamu mambo, kumbe ni mwandishi wa habari? ajabu hii, pengine ni kanjanja.
 

Mimi huwa nachekaga watangazaji wengi wa star tv wanavyojitutumua kuonesha wapo serious na kitu kwa muonekano lakn sasa wakishaanza toa yaliyo mdomoni ndo utakaposhangaa sasa kumbe kujitutumua haviendani na vilivyopo kichwani.
 
Huyo jamaa anadhalilisha hata taasisi ikiyomwajiri. Wote wanaonekana hamna kitu ni usanii tu.
Hilo ndio tatizo la kulishwa mawazo.

Na ktk hiyo Taasisi Yeye ndiyo Afisa Uhusiano Wao Sasa pata Picha Afisa Uhusiano wa Redio Mawingu hana Analytical ability Je Unategemea Nini? Hakika Ameaibisha Tasnia Nzima Ya Mawasiliano Ya Umma na Uandishi wa Habari. Kazi Ipo!!!!
 
Jamaa alipwaya mbaya! Aliingiingia kwenye kipindi akifikiri anaenda kuelezea habari za udaku!! Kwa kweli hadi nilimwonea huruma.
 
kwanza kawapotosha watanzania kuwa serikali tatu sio maoni ya watanzania bali ni kikundi cha watu wachache kilichoidhinisha serikali tatu,hapo hanma mwandishi wa habari,kwanza ameidhalilisha tasinia ya uandishi wa habari.

Kadhalilidha taasisi ya clouds anayofanyia kazi.
 

Sidhani Kama ni Kweli ila Nionavyo tu ni Kwamba hatuna Competent Journalists Japo Kielimu Wanaweza Wakawa Wana Elimu Kubwa tu tena hata Kushinda Ya Kwako. Kwa Mfano huyo Dotto Bulendu alikuwa Mbele Yangu Chuo Kikuu chetu Kile cha Papa Francis Kanda Ya Ziwa na Sasa ana Masters Yake na Kama Sijakosea Simalenga Alimaliza Diploma Yake Ya Habari DSJ ambapo hata Mke Wake alikuwa ni Mwanafunzi Mwenzake hapo hapo DSJ Chuoni na Sasa Anasoma Shahada Yake Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere. Elimu Wanazo tena Nzuri tu ILA TATIZO KUBWA LA WAANDISHI WETU WENGI WA HABARI TANZANIA HAWASOMI ISSUES MBALIMBALI, HAWAWEZI KUCHAMBUA MADA na WALICHOKALIA NI UMBEA na UZUSHI NA WANADHANI KUWA NA VYETI PEKEE NDIYO UANDISHI WA HABARI. Specialisation inatakiwa sana Kwa Waandishi Wetu Lakini pia Kuna Matatizo Makubwa Sana ktk Vyuo Vyao Kuanzia Wakufunzi Wao, Vitendea Kazi na Haswa Mazingira Ya Kusoma na Pia Ipo Haja Journalism Nayo iwe na Chombo Maalum cha Ku Screen Waandishi Kama ilivyo Kwa Fani za Sheria, Uhasibu na Madaktari ili Kabla Hawajaanza Kazi basi Wawe Wameshachujwa Vya Kutosha. Mwisho hata Huku Kuajiriwa Kwa Kujuana au Kwa Rushwa Ya Ngono Napo Kunaiponza Fani hiyo! Chuoni Mwanafunzi Anahonga Penzi Kwa Mwalimu au Anatoa Pesa Ananunua Paper au Cheti na Hapo Hapo tena Akitafuta Kazi napo Mziki ni huo huo wa Kuhonga Kwa Pesa au Ngono Je Mnategemea Nini hapo? Bado Safari ni Ndefu Sana na Inasikitisha!!!!!!!
 

Ni kweli nimeweka picha Magusudi ili GT wajue na kutambua kuwa huyo Mtu yupo kazini na mpaka sasa unaweza kuelewa yupo Kambi Gani na pia unaweza kujua Clouds ipo Kambi Gani.

Lets wait and see!

"They have Watches,But we Have Time"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…