#COVID19 Chanjo ya Corona ina umuhimu sana, Awamu ya tano ilikosea kwa kutotambua umuhimu wa sayansi

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Faida ya chanjo imezirudisha nchi nyingi hasa za Ulaya, China, USA, CANADA, SOUTH KOREA ETC katika uchumi wao wa kawaida. Yaani wanaitwa nchi zilizoendelea.

Wananchi wao wamepata chanjo na sasa hawana tena hofu na ugonjwa wa CORONA. HUDUMA ZA JAMII, STAREHE, N.K ZIMERUDI KAMA KAWAIDA.

Hapa kwetu awamu ya tano tena bila aibu ikatuambia tutumie njia za asili yaani tukapoteza mamilioni kujenga sehemu ya kujifukiza hapo Muhimbili huku watu wanateketea. Waziri wa Afya bado yupo. Inashangaza kuona hakuondolewa katika Baraza la Mawaziri wa Awamu ya Sita.

Jopo la Wataalam limetoa mapendekezo yake na yakitekelezwa tutarudi katika uchumi bora sana yaani mishahara itapanda, watalii mabilionea original kama wanaokwenda Kenya mfano wataongezeka na watu wa aina hii huwa wanakuja na wapambe kibao(wengi) ,vivyo hivyo wawekezaji wakubwa watakuja kuwekeza.

Tukifanikiwa kufuata ushauri wa kamati kuhusu CORONA miradi mingi itaongezeka, HOFU miongoni mwa hawa wachache niliowataja itaondoka.

Leo tu kwa wapenzi wa soka la England viwanja vimeanza kufurika watu.

Baada ya mapendekezo ya ripoti ya wataalam kuhusu corona kutolewa,sasa ni wakti muafaka kwa Waziri wa Afya kuachia ngazi.Katutia aibu kubwa duniani.

#KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA #KAZI IENDELEE.
 
WAKALA + WATAALAM =WAPUUZI+

Corona ya Ku deal na mabwanyenye sisi haituhusu.
Mtuache na maisha yetu haya, anaetaka kwenda ulaya apate chanjo, sisi wengine Kariakoo ndo mwisho.
 
Faida ya chanjo imezirudisha nchi nyingi hasa za Ulaya,China,USA,CANADA,SOUTH KOREA ETC katika uchumi wao wa kawaida.Yaani wanaitwa nchi zilizoendelea.Wananchi wao wamepata chanjo na sasa hawana tena hofu na ugonjwa wa CORONA.HUDUMA ZA JAMII,STAREHE,N.K ZIMERUDI KAMA KAWAIDA...
Lini tz iliwahi kua mbali na starehe, shughuri za uzalishaji na mambo mengine yaambatanayo na uzalishaji mali kisa uwepo wa covid? Hizi elimu zinazozalisha matahila sijui kwanini zmekuepo vizazi hadi vizazi
 
Embu njoo hapa kitambaa cheupe alafu ndio utajuwa kuwa hii sio nchi ya hofu hofu hapa ni bata mpaka kukuwanakimbia,tutoleeni migonjwa yenu ya kutengeneza hukoo,comrade alishasema hamna corona na hamna corona kweli,isomeke hivyo
 
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Ugonjwa ni issue ya kisayansi hivyo lazima upatiwe suluhisho la kisayansi. Imani, mila na tamaduni ni kweli zina umuhimu,lakini si kwenye matatizo yakisayansi.
 
Faida ya chanjo imezirudisha nchi nyingi hasa za Ulaya,China,USA,CANADA,SOUTH KOREA ETC katika uchumi wao wa kawaida.Yaani wanaitwa nchi zilizoendelea.Wananchi wao wamepata chanjo na sasa hawana tena hofu na ugonjwa wa CORONA...
Subiri uchanjwe utulie
 
Lini tz iliwahi kua mbali na starehe, shughuri za uzalishaji na mambo mengine yaambatanayo na uzalishaji mali kisa uwepo wa covid? Hizi elimu zinazozalisha matahila sijui kwanini zmekuepo vizazi hadi vizazi
Mtoa mada sidhani kama anaijua hali halisi ya. Huko kwa watoa chanjo.... Kwa ujumla uhuru uanao uzungumzia haupo
 
Mtoa mada sidhani kama anaijua hali halisi ya. Huko kwa watoa chanjo.... Kwa ujumla uhuru uanao uzungumzia haupo
Biden ameruhusu waliochanjwa kutobeba barakoa kwenye mizunguko yao. Uingereza pia imelegeza masharti mengi ya lockdown ikiwemo kuruhusu mikusanyiko.

China zamani walishalegeza masharti mengi.

Ujerumani maambukizi yanapungua siku hadi siku nadhani nao wako mbioni kupunguza masharti.

Kadri waliochanjwa wanavyoongezeka ndivyo na maambukizi yanavyozidi kupungua..


India- waliamua kuproduce wenywewe ile Astrazeneca lakini imeonekana na majibu tofauti, kuna wasiwasi kuwa wahindi wamepiga dili ama bahati mbaya wamekosea.
 
Faida ya chanjo imezirudisha nchi nyingi hasa za Ulaya,China,USA,CANADA,SOUTH KOREA ETC katika uchumi wao wa kawaida.Yaani wanaitwa nchi zilizoendelea.Wananchi wao wamepata chanjo na sasa hawana tena hofu na ugonjwa wa CORONA.HUDUMA ZA JAMII,STAREHE,N.K ZIMERUDI KAMA KAWAIDA...
 
Back
Top Bottom