Ya ubinafsishaji wa bandari za Tanzania na kudharau sayansi ya biashara na uchumi

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Unapoongelea ubinafsishaji, moja kwa moja inakupeleka kwenye uchambuzi wa kiuchumi na kibiashara. Maana yake ni kwamba, huu uchambuzi wa kiuchumi na kibiashara, ni masuala ya umuhimu kabisa kufanyika mwanzo na kufanyika vema kabla hata ya kufika kwenye maamuzi ya kubinafsisha kitu.

Watu wengi wamejikita sana kwenye masuala ya mikataba na MOU na kusahau ‘the core part’ ambayo ndo hiyo sayansi nzima nyuma ya ubinafsishaji.

Kwenye jicho la kibiashara, ubinafsishaji sio jambo geni. Na sio jambo geni kwasababu dhana ya ubinafsishaji maana yake ni kwamba unabadilisha umiliki wa mali au assets kutoka kwa serikali kwenda kwa kampuni binafsi. Na kuna mambo mengi sana hapo huwa yanatokea kwenye ku change ownership, inaweza kuwa ni ubinafsishaji kupitia ‘debt issuance’ au ‘equity acquisition’.

Na aina hii ya kubadilishana kwa umiliki wa biashara au kampuni, ipo pia kwa kampuni binafsi. Yaani unaweza ukawa na kampuni binafsi ikanunua kampuni nyingine binafsi. Haina tofauti na ubinafsishaji kwasababu kinachofanyika huwa ni kitu kile kile, sema tu kwenye ubinafsishaji unazungumzia kampuni ambalo ni state owned, kwamba unakuta kampuni au mwekezaji anaamua kununua haki ya umiliki wa kampuni nyingine au kuwekeza kwenye kampuni nyingine kupitia ‘debt issuance’ au ‘equity aqcuisition’.

Kwa maana hiyo, dhana nzima ya ubinafsishaji sio ngeni kwenye ulingo wa kibiashara, ni kitu ambacho kipo na kinafanyika.

Sasa ningependa nigusie, ‘sayansi ya ubinafsishaji’. Kama nilivyosema hapo mwanzo, sayansi ya ubinafsishaji unaweza kusema ni ule uhitaji wa ubinafsishaji au kubadilisha umiliki kwa maamuzi yenye jicho la kiuchumi na kibiashara.

Na kwenye jicho la kibiashara na uchumi kwenye ubinafsishaji, huwa tunaangalia Zaidi hali halisi ya uchumi na biashara kabla ya ubinafsishaji na matokeo baada ya ubinafsishaji kufanyika. Endapo kama sayansi haikuzingatiwa vizuri, maana yake ‘no matter how good was the MOU or Contract’ hakuwezi kuwa na matokeo mazuri kwenye ubinafsishaji.

Nitaongelea kwa kina namna sayansi ya uchumi na biashara namna inavyotakiwa I play role kwenye masuala mazima ya maamuzi ya ubinafsishaji na uhamishaji wa mitaji.

Sayansi yenyewe ya biashara na uchumi - mfano
Kwa mfano unaweza kuwa na biashara ambayo ufanisi wake ni mdogo na kupitia takwimu za kibiashara kama mahesabu ya kila mwaka ukaona kabisa kwamba ni biashara ambayo haina tija na inasuasua

Kampuni XYZ


Mwaka 1Mwaka 2Mwaka 3
Mauzo10,0008,5006,000
Faida700120(1,200)


Maana yake, kwa huo mfano hapo juu unaweza ukakupa picha kwamba ufanisi wa kibiashara wa kampuni XYZ upoje.

Kwa mazingira kama hayo, inaweza kuwa kwamba pamoja na kusuasua kwa ufanisi wa kampuni XYZ, lakini ni kampuni ambayo ina operate kwenye sekta ambayo ni promising, kwamba kwa sekta ambayo hii kampuni ipo, kama itaweza kuongeza mtaji na kufanya maboresho hapa na pale – aidha kwa kufanya uwekezaji mpya ama kufanya upanuzi hapa na pale, basi kuna namna fulani kwamba baada ya miaka mitano au kumi, mauzo na faida ya kampuni XYZ yanaweza kuimarika maradufu hata kufikia 100,000 kutoka 6,000 ya mauzo ya sasa.

Kwa mantiki hiyo, akisema sasa atokee mwekezaji wa kuinunua hii biashara, tayari pasi na shaka maamuzi hayo yanakuwa tayari yapo supported na sayansi nzima ya biashara na uchumi nyuma ya hii biashara XYZ.

Kwahiyo maana yake, endapo kama kampuni XYZ ni kampuni la umma na linatoa huduma ambazo zina masilahi kwa public, maana yake ni kwamba inakuwa rahisi kwa serikali kuangalia ni namna gani mkataba wa ubinafsishaji na MOU wa kampuni XYZ utakuwa unahakikisha kwamba yaliyomo kwenye sayansi ya biashara na uchumi kwenye ubinafsishaji yanatimizwa kikamilifu.

Kwa maana hiyo, contract na MOU haya ni mambo ya mwisho mwisho sana kufanyika baada ya sayansi nzima kuzingatiwa.

Ubinafsishaji wa bandari za Tanzania. Je, jicho la sayansi ya biashara na uchumi limezingatiwa?

Nimefuatailia mijadala kwenye social medias, lakini ambacho naona watu wakijadili ni mkataba wa kisheria pekee.

Nimesikitika sana maana kuna ‘core issues’ naona zinasahaulika kuhojiwa. Kwa mifano tu, nimejaribu kujiuliza haya maswali na nimekosa majibu.

  • Je kuna aliyeona taarifa za kifedha za badhari zetu, mfano hii bandari ya Daslam?
  • Je mapato yao yapoje? Yanaongezeka au yanapungua?
  • Je bandari zetu zinajiendesha kwa hasara au kwa faida?
  • Je ufanisi wa uendeshaji upoje? Na ufanisi unatakiwa uweje?
  • Je ikiwa SGR ikakamilika, na ikiunganisha Rwanda, Burundi, na Congo, port Dar es salaam, inatakiwa ikue kwa kiasi gani?
  • Je kuna mapato kiasi gani yataweza kutengenezwa kwenye bandari yetu baada ya SGR kuanza kuhudumia Rwanda, Congo, na Burundi?
  • Je serikali itatakiwa kuwekeza pesa kiasi gani ili kupanua bandari na kuhimili kuongezeka kwa mahitaji ya bandari baada ya project ya SGR?
  • Je serikali inazo pesa kiasi gani kuhimili upanuzi huu?
  • Je kama haina pesa za upanuzi, inaweza kufanya nini kuhakikisha upanuzi unafanikiwa?
  • Kama ubinafsishaji utahusika kwa nia ya kufadhili upanuzi wa bandari, je, tubinafsishe nini na nini?
  • Je kama bandari zinajiendesha kwa faida, kuna haja ya kubinafsisha?

Maswali kama hayo na mengine mengi, ndiyo yanayotengeneza ‘core issues’ kwenye dhana nzima ya maamuzi ya kubinafsisha bandari kwenye jicho la uchumi na biashara. Kwasababu kuna hatari kwamba, endepo kama haujui hii sayansi, unaweza ukawa unataka kujaribu kumtibu mtu ambaye haitaji matibabu. Ama ukatoa tiba ya magonjwa mawili kwa mtu anayeugua magonjwa saba, ambapo matokeo yake atakufa tu.

Suala la bunge kusema watu wajadili mkataba, is even wrong approach. Unajadili vipi mkataba ambao watu hawaelewi hata sayansi ya biashara na uchumi kwenye hicho kinachobinafsishwa? Maana yake, hata wanaojadili mkataba, ‘they are playing on the wrong field’.

Kuna mwanauchumi mmoja wa kimarekani anaitwa ‘Thomas Sowell’ kwenye kitabu chake cha ‘Knowledge and Decisions’, kuna mahali ameandika kwamba ‘ideas exist in superabundance, which makes the production of knowledge more difficult rather than easier. Thus, authentication is as important as the raw information itself.’

Maana yake ni kwamba, kwenye ku make decisions kama hizi za ubinafsishaji na nyinginezo, process ya muhimu kabisa ni ‘authentications’ ambayo ndiyo nimejaribu kuigusia na kuiweka kama ‘sayansi ya biashara na uchumi’.

Thomas Sowell anakuambia kwamba, ukifanya authentication kwenye idea, ndipo unaweza kugundua kwamba hii idea ni fact, hii myths, illusion, hii upigaji, huu ni ujambazi, etc.

Ubinafsishaji ni sayansi, ukiuchukulia kama ni Sanaa, basi ujue umepotea.

Niishie hapo tu

N.Mushi
 
Kiongozi barikiwa sana kwa elimu nzuri kutoka kwenye kona uliyoina wewe. Nafikiri wenye maono mapana ya mambo haya kila mmoja akichangia toka kona yake mwisho wa siku tutapata jambo zuri sana. Be blessed
 
Hitimisho lako ni nini?
Hitimisho langu ni kwamba, 'authentication' inapaswa kufanyika kwenye miwani ya kibiashara na kiuchumi halalfu ndo hayo mengine yatafuata. Ila kwa sasa, naona kila mtu anamulika hili suala kwenye angle ya mkataba na kusahau 'the core issues'
 
Back
Top Bottom