Changia CHADEMA

Big up Nanyaro, ila tunataka taarifa za mapato yote sisi kama wadau.
 
Anza kusaidia nyanya na ndugu zako walioko kijijini choka mbaya kabla ya kufanya uharibifu wa mali zako ..

Choice is yours..wengine mtoto wa dada akimuomba pesa za nauli ya shule hatoi eti anachangia chademu

Mkuu Topical,
Kuichangia chama cha upinzani ambacho kimeonyesha dira na mwelekeo wa kweli katika harakati za ukombozi wa kifikra ni kuichangia familia au jamii ya watu waliochoka na kukata tamaa.
Mkuu Topical wewe ni msomi, najua unaelewa jinsi Serikali yetu chini ya utawala wa ccm ilivyowasahau wananchi wake na kuwakumbatia matajiri.
Kuichangia CHADEMA chama ambacho kimeonyesha kwa vitendo kuwa kipo kwa ajili ya watanzania wanyonge ni kuikomboa Tanzania ya Wanyonge!
Ukweli unaujua, pamoja na kuwa unafaidika na huu utawala mbovu wa Kikwete uliopo madarakani!
 
Hela ya ruzuku haiwatoshi hadi mnaanza kuwakamua maskini? Jipangeni wazee msije mkajikuta mnachangiwa misaada ya fedha na Al-Shabaab.

Huwa unafuatilia siasa za Marekani? Umesahau Democrats wanapata michango ya fedha kutoka kwa raia wa kawaida? Hadi sasa Obama anachangisha fedha za kampeni kutoka kwa raia wa kawaida, si matajiri kama ilivyo kwa magamba.
 
kutoa ni moyo, wenye uwezo watoe tukiamini zitatimika ipasavyooooo.
 
Mkuu umesomeka
 
Mimi ni mfugaji nataka nichangie ng'ombe mmoja.Je naweza kumtuma kwa njia ya m-pesa?
 
Mimi ni mfugaji nataka nichangie ng'ombe mmoja.Je naweza kumtuma kwa njia ya m-pesa?

usilete utani kwenye uwanja wa mapambano.mkuu jaribu kuwa makini kuna majukwaa mengi humu. unaweza kutafuta jukwaa na ukafiti kabisa kwa mchango wako.!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…