Changamoto za Vyama vya Ushirika katika Kilimo cha Miwa Kilombero

MsemaKweli69

New Member
Sep 14, 2022
1
2
Habari Wakuu,

Mimi ni mkulima wa Miwa katika bonde la Kilombero, katika bonde hili huwa tunalima Miwa na kuuza kwa kampuni ya sukari Kilombero. Kwetu huku hili ni zao kuu la kibiashara Kama ilivyo korosho Mtwara.

Sasa Basi nimekuja hapa kueleza changamoto tuzipatazo sisi wakulima hivyo kuweza kuwafikia wenye mamlaka au waliopo kwenye ngazi za maamuzi. Kwa ufupi ni kwamba zao hili la Muwa huwa linasimamiwa na vyama vyetu vya ushirika akiwemo afisa ushirika toka serikalini ambaye anamonitor shughuli zote za vyama vya ushirika na kutoa miongozo katika vyama hivyo.

Kiutaratibu kwa sisi wakulima ambao pia ni wanaushirika tunatakiwa kuripoti matatizo au changamoto tuzipatazo kwa huyu afisa ushirika,lakini kwa bahati mbaya system nzima ipo corrupt hivyo hata ukiripoti changamoto hizo ni bure tu na ndio kwanza unakuwa umejipalia mkaa kwani huyo afisa ushirika mwenyewe naye ana mashamba hivyo ana play safe sababu wanajua wanatoanaje na viongozi wetu.

Sasa niende kwenye point kwa kuwa hii jamii forum inaangaliwa hata na viongozi wenye mamlaka Basi natumia nafasi hii kuwawakilisha hata wale wakulima wenzangu waliokosa nafasi ya kusema. Niwe Specific Kuna chama Cha ushirika kinaitwa KIHELEZO AMCOS GROUP hiki chama ni mojawapo ya vyama vyenye utaratibu mbovu Sana wa uvunaji wa Miwa ya wakulima kwani ratiba zao za uvunaji zinakuwa zinalenga watu Fulani either wenye vyeo katika ushirika au wanaotoa Mlungula au rushwa, lakini pia Kuna ukanda ndani yake kwa maana watu wanaotoka maeneo ambayo viongozi wanaishi. Na hili unaweza kuliona pale ambapo wewe mkulima umepakana na mwenzio lakini unakuta mwenzako anavuniwa alafu wewe unaachwa bila kuwa na sababu yeyote ya msingi.

Sasa kutokana na utaratibu kuwa mbovu kumetokea tabia ya baadhi ya wakulima either kwa kushirikiana na viongozi au kwa ubinafsi wao wanapoona ratiba haipo kwenye maeneo yao Basi wanachoma Miwa makusudi ili chama kihamishie ratiba huko hivyo kuvuruga kila kitu especially ktk chama hiki Cha KIHELEZO AMCOS.

Hivyo Sina Nia ya kumchoma mtu Ila naomba kwa yeyote mwenye mamlaka au hata viongozi wenyewe waweze kujitathmini na kuona wapi wameanguka kwani wakulima tunayumbishwa tunashindwa pangilia Mambo yetu kwani hujui lini utavuna kwa kuwa chama hakuna utaratibu rafiki na shirikishi katika kushughulika na uvunaji.

Nimeongea kwa staha nahitaji suala hili lishughulikiwe Kuna madudu mengi sijayasema nikiwa nimetoa nafasi ya watu kuona Cha kufanya vinginevyo nitayaanika hapa.

Unaweza kuona kwenye hiyo ratiba hapo haisemi tarehe za uchomaji na inawabagua watu waliochukua mikopo na wasio na mikopo.Inawezekana mtu Hana mkopo Ila Ana matatizo kuliko yule mwenye mkopo Kuna watu wanauguliwa na ndugu zao Muhimbili huko pamoja na shida zingine.

IMG_20220912_202200_967.jpg
 
Wachaga watupu Mana nachofahamu walugulu wanakodisha tu mashamba heka moja kwa mikato mitano
Wachaga sio wengi wapare ndio wengi

Huku warugulu sio wengi wapogolo,wangindo,wandamba,wangoni wahehe na wabena...changamoto ni kwamba chama kinavuna miwa kikabila nyie wengine mtavuniwa baada ya wao kuvuniana kwa wingi
 
Wachaga sio wengi wapare ndio wengi

Huku warugulu sio wengi wapogolo,wangindo,wandamba,wangoni wahehe na wabena...changamoto ni kwamba chama kinavuna miwa kikabila nyie wengine mtavuniwa baada ya wao kuvuniana kwa wingi
Eeh
 
Back
Top Bottom