Waliposema ... No Election kwa serikali ya CCM ni kama tayari walitishia kuua. Leo wakigeuka na kukubali kushiriki uchaguzi huu watakuwa wamefanya kosa kubwa sana. Watasoteshwa sana. Hii serikali haina ustaarabu kwenye uchaguzi. Historia iko wazi. Kujeruhi, kutesa, kuua, kufunga jela vyote hufanyika inapokuja suala la kulinda madaraka yao.
Ni heri CHADEMA wapotee kwenye kupigania haki kuliko kupotezwa kwa jeuri kunakoendelea. Awamu ya Tano ilibuni mkakati wa kijasiri wa kuimaliza CHADEMA kigaidi. Awamu ya Sita inaendeleza. wameshaanza 2024. Watakamilisha 2025. It is an existential threat. Have no illussion, utawala wa CCM umedhamiria kuiangamiza CHADEMA by all means. They do not want a serious opposition or political dissent in the country.
Umuhimu wa CHADEMA ni pale wananchi wenyewe watakapoamka na kujiunga na mapambano. Kama wananchi hawajali, basi acha CHADEMA ipotee tuendelee kula raha chini ya CCM isiyo na mpinzani. Inachosa sana kutumia nguvu nyingi, jasho na damu kupigania haki za watu. Nafikiri ni watu ma-sadists tu ndio bado wanapenda kuona maafa yanayowakumba baadhi ya watanzania nyakati za chaguzi zetu