1. Wenye nia ya kugombea hawanyimwi nafasi ya kurudisha fomu. Njia rahisi ni kuhakikisha ofisi ya msimamizi wa uchaguzi anakuwepo kwenye kituo chake na ofisi inakuwa wazi wakati wote. Na kila mwenye nia asizuiwe kuwasilisha fomu zake.
2. Kuhakikisha kuwa hakuna kuenguliwa kwa sababu za kijinga. Fomu zipelekwe mapema na msimamizi atakiwe kuziidhinisha kuwa zimekamilika na kama mapungufu aya ainisha kabla deadline. Ama pawe na muda wa kisheria wa kurekebisha makosa. Mathlani mwisho wa kupokea fomu ni tarehe fulani na Msimamizi anatakiwa aseme zipi hazijadhi matakwa ndani ya wiki moja na mapungufu yote yaainishwe kwa maandishi na wagombea wapewe wiki moja zaidi ya kufanya marekebisho na kuwasilisha.
3. Kama zitapokewa fomu zaidi ya moja kutoka kwenye chama kimoja, Katibu Mkuu wa Chama husika athibitishe kwa maandishi zipi ni halali. Atakayejulikana kuwa amefoji achukuliwe hatua za kisheria.
4. Kuhakikisha hakuna kuenguliwa bila sababu ya maana.
5. Mawakala wa vyama husika wasaidiwe kuwepo katika vituo vyao. Wananchi wahakikishe vitambulisho vinapatikana mapema na hawazuiwi kuingia katika kituo chao.
6. Maboksi ya kupigia kura yawe transparent na mawakala waruhusiwe kuyapiga picha.
7. Kura zihesabiwe kwa uwazi mbele ya mawakala katika kituo cha kupigia kura. Mawakala wapewe fomu za matokeo na waruhusiwe kuzipiga picha na kuzituma kwa chama chao.
Yote haya yasimamiwe na wananchi.
Amandla...
Hapana kumbe kuna vitu bado hujavielewa.
Ni kwamba kunyimwa nafasi ya kurudisha fomu sio kikwazo pekee.
Utaratibu uliopo ni kuwa hata ukifanikiwa kurudisha fomu bado haikupi guarantee wewe ya kujihakikishia kuwa utashiriki kugombea.
Ni kwasababu ni mpaka huyo mkurugenzi aziwasilishe hizo fomu zenye majina yako kwenye vituo husika vya kupigia kura.
Kwa hiyo ishawahi kutokea watu wamerudisha fomu lakini walipoenda siku ya uchaguzi, msimamizi akasema siwatambui kwasababu hampo kwenye orodha. Kwa maana mkurugenzi hakuwasilisha majina yao.
Kuhusu kuenguliwa.
Hili kwanza linaanzia kwako wewe unaye hoji. Je binafsi yako una amini kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani kuna tokana na wao kufanya makosa wakati wa kujaza fomu?
Je una amini kuwa ni CCM pekee kwa 100% ndio wenye huo uwezo wa kujaza fomu kiusahihi? (Kwasababu hakuna mgombea yeyote wa CCM aliyewahi kuenguliwa kwa kukosea kujaza fomu)
Ikiwa kama una amini hayo mambo mawili hapo juu kuwa ndio sababu, basi hizo suluhu ulizodai wazifuate zinaweza kuwa na tija.
Lakini kama kuenguliwa kunakuja kutokana na mpango maalumu wa kisiasa kuhakikisha upinzani wanakosa nafasi za kugombea basi hiyo haiwezi kuwa suluhisho.
Kuhusu mawakala kuwepo kwenye vituo na kuhakikisha kura zinapigwa kwa uwazi na kuzuia kura feki
Nadhani kabla ya yote kwenye hili swali tujiulize ni nani mwenye uwezo wa kumzuia polisi mwenye silaha ambaye amebeba kura feki?
Nani mwenye huo uthubutu?
Kwasababu tumekuwa tukiona vyombo vya dola ndio vikiwa vimepewa hilo jukumu la kusambaza kura feki.
Sasa ukizingatia kauli yako ya awali ya kulinda Demokrasia unawezaje kulinda kura katika mazingira kama hayo at the same time uwe umelinda na Demokrasia?