PreGE2025 Changamoto za "No Reforms No Elections"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
12,217
Reaction score
10,285
Ninavyoelewa mimi ni kuwa kama hapatakuwa na mabaliko katika mfumo na utaratibu wa chaguzi zetu basi hapatakuwa na uchaguzi. Kimsingi sio wazo baya ila panahiajika ufafanuzi. Nina mawazo yafuatayo:

1. Nani ataamua kuwa reform zilizofanyika ni za dhati na zitaleta kweli mabadiliko. K.m. zimetangazwa nafasi za wasimamizi wao uchaguzi ila ukiangalia sifa zinazotakiwa ni kuwa ni walewale watarudi ingawa mabadiliko yamefanyika.

2. Nini maana ya "No elections"?
Hii inaweza kutimizwa kama wapiha kura hawatajitokeza. Hii ni ngumu kufanikiwa bila kutumia nguvu ( kuwazuia watu kutoka au kufunga vituo vya kupigoa kura) kwa sababu wako watu wengi tu ambao wangependa kupiga kura na hamna quorum ya uchaguzi.
Namna nyingine ni vyama vyote vya upinzani kugomea uchaguzi. Hili nalo ni ngumu kutimizwa maana kuna vyama vitaona ni fursa kutokana na vyama vikubwa vya upinzani kutoshiriki. Na hamna mahali panaposema kuwa uchaguzi unapoteza uhalali kama vyama fulani havitashiriki.

Mtego mwingine ni wagombea wazuri wa Chadema kukosa nafasi ya kujinadi kwa wananchi kwa sababu sera ya chama chao inasema No Elections. Kwa sababu hiyo hata "reforms " zikifanyika uwezo wa kushinda utapungua. Lakini kwa upande mwingine wanaweza kupata kura zaidi kama shukrani kutoka kwa wananchi kwa kuleta mabadiliko.

3. Chadema itangaze kuwa itajitayarisha kushiriki lakini uamuzi wa kushiriki au kutoshiriki utafanyika baadae.

4. Wakati huo Chadema kifanye juhudi za dhati za kutibu majeraha kwa kuwasikiliza wale wanaoamini hawatendewi haki. Wanaweza kuanza na Njombe kuhakikisha kuwa hakuna anaejiona kuwa ni mtoto wa kambo na mwingine ndio mwana mpendwa.

Wakubali kuwa kuna wanachama hawakubaliani na hii sera kama ambavyo wako ambao hawakukubaliana na sera ya maridhiano. Wawaache tu waongee maana wataweza kuiboresha kutokana na majadiliano hayo. Waache vitisho visio na maana.

Soma Pia:

Amandla...
 
Ukimsikiliza vizuri TAL bila Reforms hakuna Uchaguzi!

Hata tukipretend CDM mzuri akaingia kwenye uchaguzi na akafanya kampeni, na akashinda, bado kutangaza mshindi ni prerogative ya CCM, Refer uchaguzi wa 2020 na 2024

Haiwezekani chama kilikuwa na wabunge zaidi ya mia after five years kikawa na mbunge mmoja!
 
Kuna suala la kusogeza uchaguzi ili mabadiliko yafanyike. Wazo hili ni baya kwa sababu:
1. Itabidi Katiba ibadilishwe ili ipate uhalali. Sidhani kama kuna kipengele cha kusogeza uchaguzi.
2. Utaliongezea muda Bunge ambalo kimsingi lipo lipo tu.
3. Limejikita kuwa chama tawala kitakuwa tayari kufanya mabadiliko ndani ya miaka mitatu. Sidhani kama Mwenyekiti wake kwa vyovyote vile atakuwa tayari kuruhusu uwezekano wa yeye kushindwa uchaguzi. Tena wakati Bunge lote ni la kwao.

Ushauri wangu ni:
1. Uchaguzi ubaki pale pale na CDM waungane na ACT-WAZALENDO katika msimamo wao wa kulinda demokrasia.
2. Kwa vile Rais wa sasa hataweza kugombea tena, atakuwa tayari zaidi kukubali mabadiliko kwa ajili ya uchaguzi wa 2030.
3. Vyama makini vitakuwa na uwakilishi zaidi Bungeni na hivyo kuweza kutoa presha kutoka ndani yake. Serikali haitarudia kosa la chaguzi zilizopita. Vyama vya upinzani vinaweza kushinikiza kuwa mawaziri na watendaji waliohusika katika chaguzi zilizopita wasihusishwe katika uchaguzi wa 2025.
4. Vyama vya upinzani vitapata ruzuku ambayo itawasaidia kujiweka vizuri kwa ajili kuleta mabadiliko kabla ya 2030. Na kisingizio cha muda hautoshi kitakosa mantik.

Sidhani kama CCM watakubali wanasiasa makini wa Upinzani warudi Bungeni, watapendelea akina Aida Khenani na COVID 19 ambao baada ya miaka mitano ya ubunge hakuna alama walioiacha bungeni!
 
Ukimsikiliza vizuri TAL bila Reforms hakuna Uchaguzi!

Hata tukipretend CDM mzuri akaingia kwenye uchaguzi na akafanya kampeni, na akashinda, bado kutangaza mshindi ni prerogative ya CCM, Refer uchaguzi wa 2020 na 2024

Haiwezekani chama kilikuwa na wabunge zaidi ya mia after four years kikawa na mbunge mmoja!
Hapo ndipo penye tatizo. Hamna namna CCM itaahirisha uchaguzi. Hata kama watagombea na DP, Chaumma, NCCR Mageuzi n.k. Uchaguzi utakuwepo na wabunge wa upinzani watakuwepo kutoka Bara na Visiwani.
Ninachoamini ni kuwa CCM hawatarudia kosa lililowafanya wawalazimishe wakina Halima waingie Bungeni ili Bunge liweze ku operate. Na utakuwa wakati muafaka wa kupima utayari wa wananchi wa kulinda kura zao.

Amandla...
 
Tumeshaamua No reform No election - huwezi kwenda kwa uchaguzi ambao unajua fika hauna macho wala masikio.

Lissu & Heche gari limeshawaka hilo na hii ndiyo agenda kuu ya taifa kwa sasa.
 
Sidhani kama CCM watakubali wanasiasa makini wa Upinzani warudi Bungeni, watapendelea akina Aida Khenani na COVID 19 ambao baada ya miaka mitano ya ubunge hakuna alama walioiacha bungeni!
Unaomuonea Aida. Ukweli ni kuwa amejitahidi.

Na nini kinakufanya uamini kuwa hali itakuwa tofauti 2028? Kumbuka shida kubwa sio taratibu bali ni uwezo wa kuzivunja bila hofu yeyote.

Amandla ...
 
Ninavyoelewa mimi ni kuwa kama hapatakuwa na mabaliko katika mfumo na utaratibu wa chaguzi zetu basi hapatakuwa na uchaguzi. Kimsingi sio wazo baya ila panahiajika ufafanuzi. Nina mawazo yafuatayo:

1. Nani ataamua kuwa reform zilizofanyika ni za dhati na zitaleta kweli mabadiliko. K.m. zimetangazwa nafasi za wasimamizi wao uchaguzi ila ukiangalia sifa zinazotakiwa ni kuwa ni walewale watarudi ingawa mabadiliko yamefanyika.

2. Nini maana ya "No elections"?
Hii inaweza kutimizwa kama wapiha kura hawatajitokeza. Hii ni ngumu kufanikiwa bila kutumia nguvu ( kuwazuia watu kutoka au kufunga vituo vya kupigoa kura) kwa sababu wako watu wengi tu ambao wangependa kupiga kura na hamna quorum ya uchaguzi.
Namna nyingine ni vyama vyote vya upinzani kugomea uchaguzi. Hili nalo ni ngumu kutimizwa maana kuna vyama vitaona ni fursa kutokana na vyama vikubwa vya upinzani kutoshiriki. Na hamna mahali panaposema kuwa uchaguzi unapoteza uhalali kama vyama fulani havitashiriki.

Mtego mwingine ni wagombea wazuri wa Chadema kukosa nafasi ya kujinadi kwa wananchi kwa sababu sera ya chama chao inasema No Elections. Kwa sababu hiyo hata "reforms " zikifanyika uwezo wa kushinda utapungua. Lakini kwa upande mwingine wanaweza kupata kura zaidi kama shukrani kutoka kwa wananchi kwa kuleta mabadiliko.

3. Chadema itangaze kuwa itajitayarisha kushiriki lakini uamuzi wa kushiriki au kutoshiriki utafanyika baadae.

4. Wakati huo Chadema kifanye juhudi za dhati za kutibu majeraha kwa kuwasikiliza wale wanaoamini hawatendewi haki. Wanaweza kuanza na Njombe kuhakikisha kuwa hakuna anaejiona kuwa ni mtoto wa kambo na mwingine ndio mwana mpendwa.

Wakubali kuwa kuna wanachama hawakubaliani na hii sera kama ambavyo wako ambao hawakukubaliana na sera ya maridhiano. Wawaache tu waongee maana wataweza kuiboresha kutokana na majadiliano hayo. Waache vitisho visio na maana.

Amandla...
Asante kwa hii recap. Lissu has nothing to lose kwa kuwa kama ni kupigwa risasi alishapigwa na kama ni kuzimu alikuchungulia.

Kwa sasa mkewe na wanae wako Belgium na anytime yeye mwenyewe tiketi ya kwenda Brussels amatembea nayo mfukoni.

Yeyote anayemsikiliza Lissu kuhusu uasi has to think twice. We don't wanna turn our country into another Sudan kwa ajili ya kusapoti watu wanaotaka uRais tu.

This is our country tuna miaka 64 ya uhuru, we have seen successes and challenges. We are not a country in distress, so to say. Hakuna justification yeyote ya kuleta uasi.

Mungu akitaka uwe Rais wa Tz utakuwa tu!! Na kama hataki uwe Rais, huwezi hata ufanye nini. Mfano ni Edward Lowassa na Maalim Seif Hamad
 
Kuna suala la kusogeza uchaguzi ili mabadiliko yafanyike. Wazo hili ni baya kwa sababu:
1. Itabidi Katiba ibadilishwe ili ipate uhalali. Sidhani kama kuna kipengele cha kusogeza uchaguzi.
2. Utaliongezea muda Bunge ambalo kimsingi lipo lipo tu.
3. Limejikita kuwa chama tawala kitakuwa tayari kufanya mabadiliko ndani ya miaka mitatu. Sidhani kama Mwenyekiti wake kwa vyovyote vile atakuwa tayari kuruhusu uwezekano wa yeye kushindwa uchaguzi. Tena wakati Bunge lote ni la kwao.

Ushauri wangu ni:
1. Uchaguzi ubaki pale pale na CDM waungane na ACT-WAZALENDO katika msimamo wao wa kulinda demokrasia.
2. Kwa vile Rais wa sasa hataweza kugombea tena, atakuwa tayari zaidi kukubali mabadiliko kwa ajili ya uchaguzi wa 2030.
3. Vyama makini vitakuwa na uwakilishi zaidi Bungeni na hivyo kuweza kutoa presha kutoka ndani yake. Serikali haitarudia kosa la chaguzi zilizopita. Vyama vya upinzani vinaweza kushinikiza kuwa mawaziri na watendaji waliohusika katika chaguzi zilizopita wasihusishwe katika uchaguzi wa 2025.
4. Vyama vya upinzani vitapata ruzuku ambayo itawasaidia kujiweka vizuri kwa ajili kuleta mabadiliko kabla ya 2030. Na kisingizio cha muda hautoshi kitakosa mantik.

Amandla...
Huwa sielewi hii dhana kuwa wapinzani wakiwa wengi bungeni wataweza kuweka shinikizo. Unaweka vipi shinikizo wakati katibu wa bungena spika ndio wanaamua nini kijadiliwe ndani ya bunge? Umesahau kikwazo cha miongozo ili kuzuia hoja kukadiliwa? Kwangu naamini mapinduzi ya kijeshi, ama machafuko kuwa ndio njia za kweli za mabadiliko kwa hapa tulipofikia.
 
Tumeshaamua No reform No election - huwezi kwenda kwa uchaguzi ambao unajua fika hauna macho wala masikio.

Lissu & Heche gari limeshawaka hilo na hii ndiyo agenda kuu ya taifa kwa sasa.
Mpaka sasa hivi ni agenda ya Chadema sio ya taifa. Hata ndani ya Chadema haijakubaliwa 100%. Ndivyo inavyotakiwa kuwa.

Amandla...
 
Huwa sielewi hii dhana kuwa wapinzani wakiwa wengi bungeni wataweza kuweka shinikizo. Unaweka vipi shinikizo wakati katibu wa bungena spika ndio wanaamua nini kijadiliwe ndani ya bunge? Umesahau kikwazo cha miongozo ili kuzuia hoja kukadiliwa? Kwangu naamini mapinduzi ya kijeshi, ama machafuko kuwa ndio njia za kweli za mabadiliko kwa hapa tulipofikia.
Hayo ni mawazo yako. Mimi siamini kuwa machafuko na mapinduzi ya kijeshi ndio jawabu.

Amandla...
 
Asante kwa hii recap. Lissu has nothing to lose kwa kuwa kama ni kupigwa risasi alishapigwa na kama ni kuzimu alikuchungulia.

Kwa sasa mkewe na wanae wako Belgium na anytime yeye mwenyewe tiketi ya kwenda Brussels amatembea nayo mfukoni.

Yeyote anayemsikiliza Lissu kuhusu uasi has to think twice. We don't wanna turn our country into another Sudan kwa ajili ya kusapoti watu wanaotaka uRais tu.

This is our country tuna miaka 64 ya uhuru, we have seen successes and challenges. We are not a country in distress, so to say. Hakuna justification yeyote ya kuleta uasi.

Mungu akitaka uwe Rais wa Tz utakuwa tu!! Na kama hataki uwe Rais, huwezi hata ufanye nini. Mfano ni Edward Lowassa na Maalim Seif Hamad
Usitake kuleta upotoshaji wa kijinga. Hakuna popote Lisu anapolazimisha kuwa rais, Lisu anataka chaguzi ziheshimiwe. Hayo mambo ya kutuambia mkewe yuko Belgium na familia yake haiondoi ukweli wa madai yake. Na ukweli ni kuwa chaguzi zetu ni za kishenzi. Hatuko tayari kutawaliwa na ccm kwa shuruti.
 
Mpaka sasa hivi ni agenda ya Chadema sio ya taifa. Hata ndani ya Chadema haijakubaliwa 100%. Ndivyo inavyotakiwa kuwa.

Amandla...
Haya ndio matamanio ya kila mwanaccm. Hivyo usijali. Ajenda inayokubaliwa na kila mwananchi ni kuendelea kuwa na hizi chaguzi za udanganyifu.
 
Kuna suala la kusogeza uchaguzi ili mabadiliko yafanyike. Wazo hili ni baya kwa sababu:
1. Itabidi Katiba ibadilishwe ili ipate uhalali. Sidhani kama kuna kipengele cha kusogeza uchaguzi.
2. Utaliongezea muda Bunge ambalo kimsingi lipo lipo tu.
3. Limejikita kuwa chama tawala kitakuwa tayari kufanya mabadiliko ndani ya miaka mitatu. Sidhani kama Mwenyekiti wake kwa vyovyote vile atakuwa tayari kuruhusu uwezekano wa yeye kushindwa uchaguzi. Tena wakati Bunge lote ni la kwao.

Ushauri wangu ni:
1. Uchaguzi ubaki pale pale na CDM waungane na ACT-WAZALENDO katika msimamo wao wa kulinda demokrasia.
2. Kwa vile Rais wa sasa hataweza kugombea tena, atakuwa tayari zaidi kukubali mabadiliko kwa ajili ya uchaguzi wa 2030.
3. Vyama makini vitakuwa na uwakilishi zaidi Bungeni na hivyo kuweza kutoa presha kutoka ndani yake. Serikali haitarudia kosa la chaguzi zilizopita. Vyama vya upinzani vinaweza kushinikiza kuwa mawaziri na watendaji waliohusika katika chaguzi zilizopita wasihusishwe katika uchaguzi wa 2025.
4. Vyama vya upinzani vitapata ruzuku ambayo itawasaidia kujiweka vizuri kwa ajili kuleta mabadiliko kabla ya 2030. Na kisingizio cha muda hautoshi kitakosa mantik.

Amandla...
Kwa haya mazingira yaliyopo ,umeshajaribu kugombea ?
 
Tatizo ni vyama pinzani kutokua na ushirikiano lakini pia utitiri wa vyama pinzani.
Kuna vyama zaidi ya 15, na vyote vinatofautiana mitazamo na kunyukana na kwenye uchaguzi vinagawana kura, usitegemee hiyo kitu kupata nguvu maana bila shaka kuna vyama ni gelesha ya chamadola.

Walau vyama vikuu 4 vingekua na nia ya pamoja kweli hilo lingewezekana ila kwa chadema pekee, tena humohumo ndani kuna watu wanatamani wagombee nafasi mbalimbali aloo sijui kama itatoboa hiyo "no reform no election"
 
Huwa sielewi hii dhana kuwa wapinzani wakiwa wengi bungeni wataweza kuweka shinikizo. Unaweka vipi shinikizo wakati katibu wa bungena spika ndio wanaamua nini kijadiliwe ndani ya bunge? Umesahau kikwazo cha miongozo ili kuzuia hoja kukadiliwa? Kwangu naamini mapinduzi ya kijeshi, ama machafuko kuwa ndio njia za kweli za mabadiliko kwa hapa tulipofikia.
Nakubaliana na hoja yako hakuna namna ya kubadili katiba bila machafuko Afrika nzima na haitawahi itokee na ndicho anachofanya lissu yani yupo tayari kukinukisha ili reforms zipatikane

Katika nchi zetu hii mifumo imejisimika na ni ngumu kuibadilisha hayupo na hatakuwepo rais wa chama tawala akakubali chama kimfie mikononi mwake hayupo
 
Hakuna jinsi, bila machafuko itakuwa ni hadaa za bei rahisi.
 
Huo ndio ukweli but binafsi sioni wa kukinukisha Tz labda miaka buku ijayo uthibitisho utaonekanwa soon
 
Hata mimi sioni wa kukinukisha kwa sasa, lakini hiyo ni lazima itokee.
 
Asante kwa hii recap. Lissu has nothing to lose kwa kuwa kama ni kupigwa risasi alishapigwa na kama ni kuzimu alikuchungulia.

Kwa sasa mkewe na wanae wako Belgium na anytime yeye mwenyewe tiketi ya kwenda Brussels amatembea nayo mfukoni.

Yeyote anayemsikiliza Lissu kuhusu uasi has to think twice. We don't wanna turn our country into another Sudan kwa ajili ya kusapoti watu wanaotaka uRais tu.

This is our country tuna miaka 64 ya uhuru, we have seen successes and challenges. We are not a country in distress, so to say. Hakuna justification yeyote ya kuleta uasi.

Mungu akitaka uwe Rais wa Tz utakuwa tu!! Na kama hataki uwe Rais, huwezi hata ufanye nini. Mfano ni Edward Lowassa na Maalim Seif Hamad
Acha propaganda za kipuuzi hapa,Sisi tunachotaka ni kura zetu ziheshimiwe tu(Hakuna kuleta ujanja ujanja kwenye sanduku la kura). Kama ni mshindi ashinde kwa haki hatuangalii nani kashinda,akishinda yeyote yule poa tu.Mshindi akipatikana kwa halali ataheshimu wapiga kura wake kwa kuwajibika kwao na sio sasa mshindi akawajibika kwa hule aliyesababisha ushindi wake wa mchongo.Huneni basi aibu mmeshaiba pesa za kutosha sn ccm fanyeni hayo mabadiliko kwani mnaogopa nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom