Changamoto za mpenzi zinanikosesha raha

Changamoto za mpenzi zinanikosesha raha

Loh, kazi unayo bidada. Mwanaume wa kublock? Mie wangu alifanya hivyo mara moja alivyorudi nikamwambia kbs siku ukiniblock tena ujue ndio bye bye. Na hata hivyo kwa lile kosa langu kweli nilistahili block ya muda ili apate relief.
 
Ninamjali sana mkuu. Na ndio hicho kinachomrudishaga sana. Ninamjali mpaka ananiambia mwenyewe kuwa am too good for him.
The greatest love of all ni kujipenda ww kwanza... Anafanya hvyo anajua unampenda na huna pa kwenda but ungempotezea ukatafuta mwngne lazma angenyooka hawa wanaume tunawapenda lakin kuwapenda kusitufanye tuwe watumwa.. Aniblok kila nikikosea tena atakuta nshatafuta wa kuzugia na kumueka whatsap profile ataomba poo! Anaweza enda uko akaja na magonjwa hujui anakua na nani!
Think abt your life first mama
 
Unyonge ktk Mapenzi unatesa mno,naye akishajua ndiyo unampenda kiasi hicho hiyo ndiyo inakuwa fimbo ya kukupigia!fanya maamuzia ambayo yatakupa furaha
 
Habari zenu?
Moja kwa moja niende kwenye mada. Mimi ni mdada mwenye elimu yangu, kazi zangu na malengo mazuri nikipata uhai na kibali cha Muumba.
Nilipata mpenzi ambaye tumedumu nae kwa mwaka sasa. Ananijua vema. Kuanzia familia mpaka kila kitu kinachonihusu. Yeye pia ninamjua sana hata familia yake ingawa hatujatambulishana.
Mwenzangu simuelewi. Mwanzo alinijali kwa kidogo alichonacho. Kabla sijapata kazi yeye alikua namba moja kujua nimekula nini au kuvaa nini.
Lakini baada ya mwenzangu kuhamishia makazi yake mbali kidogo na nyumbani, amebadilika sana.
Hanijali kama mwanzo. Ugomvi kidogo ukitokea ananiblock. Hata kama hakuna la maana. Kuunblock ni mpaka ajisikie yeye. Anaweza akakaa hata mwezi alafu akanipigia simu usiku kuomba radhi na maisha yanaendelea. Hapo atafululiza kunijali kwa siku kadhaa lakini ninapomuuliza jambo ambalo pengine amenikosea, basi anasusa na kuniblock. Kuniunblock tena ni mpaka ajisikie. Lakini ni lazima anarudi.
Wakuu mi simuelewi. Nimeshamsema tabia hii na bado nikaambulia block. Nikamtafuta kwa namba Mpya na kumwambia bora tuachane. Akakubali lakini baada ya siku kadhaa akanipigia simu na kuniomba msamaha na kudai hawezi kuniacha kabisa. Wakuu hapa nilipo nimepigwa block tena. Nimemuambia asirudi tena ingawa najua atarudi. Siwezi kubadili namba kwa ajili yake.
Hivi na wengine wanapata changamoto kama mimi au? Mimi nimechoka kwa kweli. Ananiambia nimvumilie ye ndivyo alivyo. Namwambia anapoteza muda sana, huo muda wa kuniblock tungekuwa tumefanya jambo la maana la maendeleo, wala haelewi. Na ni mtu mzima kuliko mimi. Yeye ana 28 years sasa.
Mkuu wewe ni me/ke? Ref: Ninatamani kurudi kwake...
 
UTASTUKIA UNAONA PICHA ZA NDOA YAKE FB. WE JICHELEWESHE AENDELEE KUKURARUA. CHUKUA HATUA. MPGE CHINI, FANYA YAKO. KUWA NA MSMAMO BINT
 
Elewa yupo mwenzio anakusaidia hapo.


Mwanamke akishaniblock ndio kaenda na maji i will never be the same person again,fikiria mtu kama huyo ndio mnaishi nyumba moja.
 
Ushauri huu unaopewa hautokua na manufaa kwako kama bado utabaki na msimamo wako wa kumpokea kila atakapo jirudi, huruma yako maumivu yako. Ameshajua udhaifu wako huyo, mpotezee mazima hata kama akijirudi usipokee simu zake wala kujibu meseji zake. Anza maisha mapya maana inaonekana huko aliko ameshampata mwingine ambaye ameshaziba pengo lako ingawa bado hamjaachana. Trust me utakuja kukumbuka ushauri huu pale utapo onja tamu ya kumsahau baada ya muda kupita.
 
Huyo amecalculate anaona kbs kakupa 60% yaan kuna roho inasema muache tu huyu mwanamke na kuna roho inasema ana vitu flani hivi vichache vzr unaweza kosa kwa mwanamke mwingine...kifupi huyo yupo njia panda
 
Ni mtu mzimaa kuliko wewe Ana 28yrs! Hapo ndio kwenye tatizo, muache aongeze umri kidogo...
 
Fal* huyo achana nae, Kama vipi chukua hata pic yangu weka katika prof pic ya whatsapp, alafu Annika jinsi unavyofurahia kuwa na mwaume anayekujali....shenzy kbsa
 
Fal* huyo achana nae, Kama vipi chukua hata pic yangu weka katika prof pic ya whatsapp, alafu Annika jinsi unavyofurahia kuwa na mwaume anayekujali....shenzy kbsa
Hahahaaa mkuu... Nitumie basi niweke dp
 
kitu kimoja ambacho wanawake mmejaaliwa ni uwezo wenu wa kujieleza unapokuwa una tatizo hata kama mkosaji ni mwananke mwenyewe,jamii inawaelewa sana mkijieleza,mwanzo kwa nini alikuwa so caring kipindi hiki awe hivyo,Sisemi kwa wewe una tatizo ila angalia wapi na wewe unateleza then kila mmoja aki admit udhaifu wake mtakuwa poa,kwa haraka haraka kitu niniachikiona hapo ni umbali kati yenu,anaweza akawa anaku block ili apate chance sahihi ya yeye kuwa huru kufanya lolote huko ailko,japo ni asumptions tu,lakini kwa upande wako usitumie neema ulizo nazo mafanikio elimu,kipato nk kuona kwamba unaweza mwambia mwanaume chochote akafanya,utakuwa unakosea,pia usipende kueleza mipango yenu nini mnatakiwa kufanya na mumeo kwa kupitia simu.Kwa nini usiende hukohuko mkaongea hayo masuala ya kufanya maendeleo live,orodhesha vitu unavyotakiwa kuongea na mpenzi wako aliyeko mbali,vipi uongee kwenye simu na vipi muongee ana kwa ana
Au shughulikieni kwanza vipi mtakuwa pamoja tena karibu,Hapa utapata comment za kukubomoa tuu sio kukujenga maana anayeongea muda huu kuhusu matatizo yenu ni wewe peke yako hatujamsikiliza nae mumeo,he may be more perfect than you and viceversa,
No one is perfect,pambana na uliye naye usiye naye humjui nae ana madhaifu gani
 
Ana mwenzako huko wewe kilaka kama mmiliki hayupo unabadili kwa muda tu fanya maamuzi sahihi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom