Under-cover
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 1,006
- 1,640
aomba nishee ka story kangu, ila wanawake 🙌. Bana nakumbuka nimemaliza chuo, sasa nilikuwa na pisi iko mwaka wa mwisho. Sasa home ilikuwa ni karibu na chuo nilikomaliza kusoma na yeye ndio alikuwa anasoma hapo. Kuna siku bwana nilimwambia tukutane mara moja nimuone kwa sababu nilikuwa nimemmisi sana ila kwa haraka. Basi tuka set saa moja na nusu usiku na eneo lilikuwa lenye ka giza flani hivi maana naye alikuwa anaelekea kuswali. Basi nimetoka zangu na jamaa yangu haraka tukafika eneo, pisi ikaja tukasalimiana nayo, jamaa yangu akatupa space. Mara kidogo difenda hiyo imebeba askari magereza, ikawa inapita maeneo yale, tukashituliwa na sauti, "Nyie mnafanya nini hapo?" Manzi alikuwa ashapiga hatua anataka kukimbia mimi nikatulia tu. Wale jamaa walikuwa kwenye doria, basi wakaja kutubeba mkuku mkuku. Ee si wakaanza kutuzingua, "Mlikuwa mnafanya nini gizani, au nyie vibaka?" Mimi kimya, manzi hapo analia vibaya.
Kulikuwa na askari wakike wawili na kama sikosei wakiume wanne au watano hivi. Sasa bana wanaume si unajua hatukandiani, wale askari wakike wawili wakaanza kunioshea mbele ya manzi yangu huku gari inaelekea kituoni kwenda kutulaza.
"Mimi nina simu ya batani, manzi ana iPhone 6." Wakamuuliza manzi nani kakununulia hii simu, akasema baba yake. Maneno yakaanza kutoka, "Mwanaume gani unashindwa kumnunulia demu wako hata simu alafu wewe unatumia batani, hivi hata pedi unaweza kweli? Unafanya kazi gani na unakaa na nani?"
Mimi jobless, nakaa na mzee. Je, anafanya kazi gani? Nikasema jw. Wakauliza cheo nika mute, wakaanza, "Kwahiyo mishahara imetoka ndio ukaona uje umdanganyie huyu binti?" Mimi kimya. "Leo itabidi ukalale ndani kesho baba yako aje akutoe." Wakaanza tena, "Sikia binti siku hizi hakuna mapenzi bila pesa, hakuna ndoa bila pesa." Manzi alikuwa analia tu. Mjuba nimetulia, kiukweli wale askari wakike walitema shombo mbaya sana juu yangu. Kwa akili yangu niliwaza hawa ni form 4 failures ndio maana wameingia huku wanaropoka uchafu, niliumia mbaya. Aisee gari ikaenda mbali sana wakaenda kutushushia mbali sana njiani, na walitaka tu kutuhangaisha tu.
Sasa ile nashuka tu alikuja askari mmoja wa kiume aliniramba kibao cha mgongo nikagugumia tu, wakasepa zao. Huku tukiwa pembezoni mwa barabara, manzi analia nambembeleza huku tunatembea na ni saa 2 kwenda 3. Basi akaniambia, "Nataka nirudi chuo," nikasema sawa. Nikamwitia boda, nikamwambia sina nauli 😅, akasema sawa anayo, huyo akapanda na kusepa.
Mjuba hapa sina hela nikaanza kutembea, nilipash mpaka home kufika saa 3. Pale nje kabla sijaingia ndani nakuta mshikaji wangu kumbe yeye alikimbia baada ya kuona ile difenda. Akaniuliza, "Vipi?" huku akicheka na kulikuwa na mwana mwingine pale, nikawaelezea wakacheka. Kisha nikasema huyu manzi kwa sumu aliyojazwa muda si mrefu naachwa. Wakanipa hope, "Oh hamna bana." Baadaye saa 4 nikamtafuta manzi nikampa pole yakaisha, ila moyoni najua soon nakula kamba.
Kweli bana siku ya 1, freshi 2, freshi na ya 3 nikaona kabadilika hata majibu yake nikasema hapa ndo bye. Siku ya nne ilikuwa tu meet nikalambwa block mpaka leo hii sijuagi yuko wapi yule manzi. Nilicheka sana na kuwaambia wana na nilipata funzo flani juu ya hawa she, ila ile sumu na zile kejeli 🙌, NIKIZIPATA nitawadharau sana hawa ubavu wa pili 😏. DUMU