Changamoto za mpenzi zinanikosesha raha

Changamoto za mpenzi zinanikosesha raha

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
381
Habari zenu?

Moja kwa moja niende kwenye mada.

Mimi ni mdada mwenye elimu yangu, kazi zangu na malengo mazuri nikipata uhai na kibali cha Muumba.Nilipata mpenzi ambaye tumedumu nae kwa mwaka sasa. Ananijua vema. Kuanzia familia mpaka kila kitu kinachonihusu. Yeye pia ninamjua sana hata familia yake ingawa hatujatambulishana. Mwenzangu simuelewi. Mwanzo alinijali kwa kidogo alichonacho.

Kabla sijapata kazi yeye alikua namba moja kujua nimekula nini au kuvaa nini.Lakini baada ya mwenzangu kuhamishia makazi yake mbali kidogo na nyumbani, amebadilika sana.Hanijali kama mwanzo.

Ugomvi kidogo ukitokea ananiblock. Hata kama hakuna la maana. Kuunblock ni mpaka ajisikie yeye. Anaweza akakaa hata mwezi alafu akanipigia simu usiku kuomba radhi na maisha yanaendelea.

Hapo atafululiza kunijali kwa siku kadhaa lakini ninapomuuliza jambo ambalo pengine amenikosea, basi anasusa na kuniblock. Kuniunblock tena ni mpaka ajisikie. Lakini ni lazima anarudi.

Wakuu mi simuelewi. Nimeshamsema tabia hii na bado nikaambulia block. Nikamtafuta kwa namba mpya na kumwambia bora tuachane. Akakubali lakini baada ya siku kadhaa akanipigia simu na kuniomba msamaha na kudai hawezi kuniacha kabisa.

Wakuu hapa nilipo nimepigwa block tena. Nimemuambia asirudi tena ingawa najua atarudi. Siwezi kubadili namba kwa ajili yake. Hivi na wengine wanapata changamoto kama mimi au? Mimi nimechoka kwa kweli.

Ananiambia nimvumilie ye ndivyo alivyo. Namwambia anapoteza muda sana, huo muda wa kuniblock tungekuwa tumefanya jambo la maana la maendeleo, wala haelewi. Na ni mtu mzima kuliko mimi. Yeye ana 28 years sasa.
 
hapo hauhitaji ushaurii, hivii unalamikia mapenzi ya nini ndugu,muachee aende zakee
 

Attachments

  • FB_IMG_1505733918468.jpg
    FB_IMG_1505733918468.jpg
    31.2 KB · Views: 70
Akikublock nawe mblock ili akija kuku-unblock akute block yako ili ajue inavyokera

Alafu mbona haya ya kublock huwa tunafanya sisi wa kike
Nami nashangaa jamani. Anasusa na kublock hovyo. Kama jana hoja tuliyoongelea ni kufungua mradi, nikamwambia mimi nakusaidia kufungua ila sitahusika na mali yoyote na siwezi kutoa pesa zangu sababu naogopa kukuamini, we si mume. Hilo neno kuogopa likaniletea block jamani. Au nilikosea kusema hivi?
 
Nami nashangaa jamani. Anasusa na kublock hovyo. Kama jana hoja tuliyoongelea ni kufungua mradi, nikamwambia mimi nakusaidia kufungua ila sitahusika na mali yoyote na siwezi kutoa pesa zangu sababu naogopa kukuamini, we si mume. Hilo neno kuogopa likaniletea block jamani. Au nilikosea kusema hivi?

Ungetafuta hata neno lingine la kuziba hilo neno kutokumuamini(hata kama ni kweli humuamini)
Mpenzi wako unamchanaje live hivo kuwa humuamini jamani?

Ila hata hivyo mwanaume anakuwaje na tabia ya kususa susa hivo,anakosea
 
Habari zenu?
Moja kwa moja niende kwenye mada. Mimi ni mdada mwenye elimu yangu, kazi zangu na malengo mazuri nikipata uhai na kibali cha Muumba.
Nilipata mpenzi ambaye tumedumu nae kwa mwaka sasa. Ananijua vema. Kuanzia familia mpaka kila kitu kinachonihusu. Yeye pia ninamjua sana hata familia yake ingawa hatujatambulishana.
Mwenzangu simuelewi. Mwanzo alinijali kwa kidogo alichonacho. Kabla sijapata kazi yeye alikua namba moja kujua nimekula nini au kuvaa nini.
Lakini baada ya mwenzangu kuhamishia makazi yake mbali kidogo na nyumbani, amebadilika sana.
Hanijali kama mwanzo. Ugomvi kidogo ukitokea ananiblock. Hata kama hakuna la maana. Kuunblock ni mpaka ajisikie yeye. Anaweza akakaa hata mwezi alafu akanipigia simu usiku kuomba radhi na maisha yanaendelea. Hapo atafululiza kunijali kwa siku kadhaa lakini ninapomuuliza jambo ambalo pengine amenikosea, basi anasusa na kuniblock. Kuniunblock tena ni mpaka ajisikie. Lakini ni lazima anarudi.
Wakuu mi simuelewi. Nimeshamsema tabia hii na bado nikaambulia block. Nikamtafuta kwa namba Mpya na kumwambia bora tuachane. Akakubali lakini baada ya siku kadhaa akanipigia simu na kuniomba msamaha na kudai hawezi kuniacha kabisa. Wakuu hapa nilipo nimepigwa block tena. Nimemuambia asirudi tena ingawa najua atarudi. Siwezi kubadili namba kwa ajili yake.
Hivi na wengine wanapata changamoto kama mimi au? Mimi nimechoka kwa kweli. Ananiambia nimvumilie ye ndivyo alivyo. Namwambia anapoteza muda sana, huo muda wa kuniblock tungekuwa tumefanya jambo la maana la maendeleo, wala haelewi. Na ni mtu mzima kuliko mimi. Yeye ana 28 years sasa.
Mh hayo mapenzi yenu ni ya kitoto haswa hilo la yeye kukublock kila mara,mtafute ongea nae ana kwa ana kama hatobadilika fanya maamuzi magumu!
 
wewe moyo wako unakusukumaje maana mwisho wa siku wewe ndie mwenye maamuzi ya mwisho
pengine ameshajua udhaifu wako kwake kwamba unampenda kupitiliza
 
Mpenzi sio mchumba
Mchumba sio mke/Mme
Mapenzi yanachangamoto nyingi sana na nyingi huwa ni za kuvunja moyo chache ni za kutia moyo hapo unaweza kufanya jambo moja ambalo litakuwa msaada wako wa baadae kuachana nae kwa kuwa kupoteza mda mwingi kusuruhisha mahusiano ni kujipotezea wakati

Na kuenda kuanzisha mahusiano mapya sio tiba ya matatizo uliyo kimbia

Hapo jipe moyo wa uvumilivu jipe mda wa kutafari tatizo linaweza kuwa ni wewe
 
Ivi kwann utesek na mtu mmoj tu why ulizaliw nae? Si umpotezee uangalie mtindo mwingine wa maisha duh mi sjawai tesek ivo ATI mapenz labda uenda namm yatanifik ila sizan
 
Achana naye sasa mtu anakubuloku mwezi mzima bado unatafuta ushauri kwa nini usiondoke kimyakimya njoo huku hutojuta wengine hizo chance tunazitafuta kwa sana.[emoji85][emoji85][emoji85]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom