Changamoto za mpenzi zinanikosesha raha

Changamoto za mpenzi zinanikosesha raha

Huwa watu wa hivyo ni visirani, nilikuwaga nablock nafuta namba zote siku 2 naanza kuitafuta hadi anipigie nimehaha hasira hizi jaman.
 
Habari zenu?

Moja kwa moja niende kwenye mada.

Mimi ni mdada mwenye elimu yangu, kazi zangu na malengo mazuri nikipata uhai na kibali cha Muumba.Nilipata mpenzi ambaye tumedumu nae kwa mwaka sasa. Ananijua vema. Kuanzia familia mpaka kila kitu kinachonihusu. Yeye pia ninamjua sana hata familia yake ingawa hatujatambulishana. Mwenzangu simuelewi. Mwanzo alinijali kwa kidogo alichonacho.

Kabla sijapata kazi yeye alikua namba moja kujua nimekula nini au kuvaa nini.Lakini baada ya mwenzangu kuhamishia makazi yake mbali kidogo na nyumbani, amebadilika sana.Hanijali kama mwanzo.

Ugomvi kidogo ukitokea ananiblock. Hata kama hakuna la maana. Kuunblock ni mpaka ajisikie yeye. Anaweza akakaa hata mwezi alafu akanipigia simu usiku kuomba radhi na maisha yanaendelea.

Hapo atafululiza kunijali kwa siku kadhaa lakini ninapomuuliza jambo ambalo pengine amenikosea, basi anasusa na kuniblock. Kuniunblock tena ni mpaka ajisikie. Lakini ni lazima anarudi.

Wakuu mi simuelewi. Nimeshamsema tabia hii na bado nikaambulia block. Nikamtafuta kwa namba mpya na kumwambia bora tuachane. Akakubali lakini baada ya siku kadhaa akanipigia simu na kuniomba msamaha na kudai hawezi kuniacha kabisa.

Wakuu hapa nilipo nimepigwa block tena. Nimemuambia asirudi tena ingawa najua atarudi. Siwezi kubadili namba kwa ajili yake. Hivi na wengine wanapata changamoto kama mimi au? Mimi nimechoka kwa kweli.

Ananiambia nimvumilie ye ndivyo alivyo. Namwambia anapoteza muda sana, huo muda wa kuniblock tungekuwa tumefanya jambo la maana la maendeleo, wala haelewi. Na ni mtu mzima kuliko mimi. Yeye ana 28 years sasa.
Hiyo ndio inaitwa akufukuzae akwambii toka, sasa sijui ww unasubiri nin dada, na wewe mblock na usimuunblock tena..
 
Mwanaume mzima kazi ku-block tu!
Pole bi dada ila jua hii ni trela muvi halisi ndoani ndo atakua anasepa kabisa home kurudi baada ya mwezi.
 
Nami nashangaa jamani. Anasusa na kublock hovyo. Kama jana hoja tuliyoongelea ni kufungua mradi, nikamwambia mimi nakusaidia kufungua ila sitahusika na mali yoyote na siwezi kutoa pesa zangu sababu naogopa kukuamini, we si mume. Hilo neno kuogopa likaniletea block jamani. Au nilikosea kusema hivi?
ndio ulikosea unaacha kumuamini huyo mwandani wako utamwamini nani,ni pm tafadhali
 
Mi nakushauri hivi we umblock ili akija kukutafuta ahahe na unampa hiyo discipline kwa miezi kama 6 hv ukiona ndani ya muda wote huo anakubembeleza kwa namba nyngne basi unamunblock unaendelea naye hata rudia tena mbona.
 
Ivi kwann utesek na mtu mmoj tu why ulizaliw nae? Si umpotezee uangalie mtindo mwingine wa maisha duh mi sjawai tesek ivo ATI mapenz labda uenda namm yatanifik ila sizan
Hujawahi penda wewe
 
Hujui kusoma hata picha huoni mpendwa, hakuna mume wa hivyo mkiwa ndani ugomvi kidogo atahamia baa mwezi. Apite hiiii we futa delete namba zake na block kabisa msumbufu huyo.
 
Aisee una moyo wa plastic yaani ana kublock anarudi na mnaedelea kama kawaida aafu unasema mna uhusiano...na akirudi unamsamehe kama vile wewe ndio mwenye kosa mnaedelea mpaka aje aku block tena...serious huitaji ushahidi mwingine zaidi ya huu..upo mahala hutakiwi kabisaa na jamaa kashajua weakness zako anakuchezea kama vile wewe ni mdoli.
Ushawai kumblock hata mara moja nae aoje joto la jiwe kama wèwe.
Hapa chomoka mbio mblock milele sio tu simu hata ndani ya moyo wako na futa kabisa kwenye akili yako lolote kuhusu huyu mr block.
 
labda nyendo zako na maneno yako ni kero kwake pia yanamwondolea concentration labda ndo maana anakublock
 
Natamani nikuazime moyo wangu,.hivi anakublokuje kwa mfano?? Joanah kakujibu vzr kweli akikublock naww unamblock na blacklist juu kuna wanaume wanavielementi vya kike asee,.Fanya kazi,make your own money then build yo' empire watakuja tuu utakuwa na kazi ya pick n' choose yupi afurahishe moyo wako achana naee buana kwani shin'ngapi...
 
Aisee una moyo wa plastic yaani ana kublock anarudi na mnaedelea kama kawaida aafu unasema mna uhusiano...na akirudi unamsamehe kama vile wewe ndio mwenye kosa mnaedelea mpaka aje aku block tena...serious huitaji ushahidi mwingine zaidi ya huu..upo mahala hutakiwi kabisaa na jamaa kashajua weakness zako anakuchezea kama vile wewe ni mdoli.
Ushawai kumblock hata mara moja nae aoje joto la jiwe kama wèwe.
Hapa chomoka mbio mblock milele sio tu simu hata ndani ya moyo wako na futa kabisa kwenye akili yako lolote kuhusu huyu mr block.
You are really marvelous
 
You are really marvelous
inaboa sana....where love is not reciprocated is a dead end no matter hoe sweet th past t was....mapenzi hua hayalazimishwi na ukishji expose ua weakness umekwisha kabisa...hapa ni kama toilet paper imetumika na kuitupa hukoooo...
 
unasubiri msaada wa watu wa marekani waje kukwambia hakufai au?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom