Habari zenu?
Moja kwa moja niende kwenye mada.
Mimi ni mdada mwenye elimu yangu, kazi zangu na malengo mazuri nikipata uhai na kibali cha Muumba.Nilipata mpenzi ambaye tumedumu nae kwa mwaka sasa. Ananijua vema. Kuanzia familia mpaka kila kitu kinachonihusu. Yeye pia ninamjua sana hata familia yake ingawa hatujatambulishana. Mwenzangu simuelewi. Mwanzo alinijali kwa kidogo alichonacho.
Kabla sijapata kazi yeye alikua namba moja kujua nimekula nini au kuvaa nini.Lakini baada ya mwenzangu kuhamishia makazi yake mbali kidogo na nyumbani, amebadilika sana.Hanijali kama mwanzo.
Ugomvi kidogo ukitokea ananiblock. Hata kama hakuna la maana. Kuunblock ni mpaka ajisikie yeye. Anaweza akakaa hata mwezi alafu akanipigia simu usiku kuomba radhi na maisha yanaendelea.
Hapo atafululiza kunijali kwa siku kadhaa lakini ninapomuuliza jambo ambalo pengine amenikosea, basi anasusa na kuniblock. Kuniunblock tena ni mpaka ajisikie. Lakini ni lazima anarudi.
Wakuu mi simuelewi. Nimeshamsema tabia hii na bado nikaambulia block. Nikamtafuta kwa namba mpya na kumwambia bora tuachane. Akakubali lakini baada ya siku kadhaa akanipigia simu na kuniomba msamaha na kudai hawezi kuniacha kabisa.
Wakuu hapa nilipo nimepigwa block tena. Nimemuambia asirudi tena ingawa najua atarudi. Siwezi kubadili namba kwa ajili yake. Hivi na wengine wanapata changamoto kama mimi au? Mimi nimechoka kwa kweli.
Ananiambia nimvumilie ye ndivyo alivyo. Namwambia anapoteza muda sana, huo muda wa kuniblock tungekuwa tumefanya jambo la maana la maendeleo, wala haelewi. Na ni mtu mzima kuliko mimi. Yeye ana 28 years sasa.