Changamoto ya Michango ya Harusi

Changamoto ya Michango ya Harusi

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,038
Michango ya harusi imekuwa mzigo kwa familia na wachangiaji. Ingawa ni desturi ya kijamii kutoa michango katika matukio haya, ni naona lazima kutafakari kama michango hii inasaidia kweli familia au inawaongezea mzigo wa kifedha.

Badala ya kuendelea na utaratibu wa kuchangia harusi na misiba, ni vyema jamii yetu ianze kuzingatia michango kwa ajili ya mambo ya msingi kama,

  • Elimu: Kuchangia ada za shule kwa watoto wa familia maskini ili kuwapa fursa ya kupata elimu bora.
  • Afya: Kuchangia gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaohitaji msaada wa haraka.
  • Biashara: Kusaidia mitaji ya biashara kwa vijana na wanawake ili kuwawezesha kujitegemea kiuchumi.

Ni wakati sasa wa kubadili mtindo wa michango katika jamii yetu. Badala ya kuwekeza katika sherehe za kifahari, tuwekeze katika maendeleo ya kijamii kwa kuchangia elimu, afya, na biashara.

Je, tunahitaji kubadili mtindo huu wa michango ya harusi ili kulinda uhusiano wetu wa kijamii na kifamilia? Ni wakati wa kutafakari na kuchukua hatua.

~Chavalikungu hapa ,nilifunga ndoa misa ya asubuhi nilipotoka nkaenda zang kufyatua tofali za biashara
 
KUCHANGIA HARUSI NI UPUMBAVU

MSIBA KWELI MAANA HAUNA HODI NA MASUALA YA AFYA PIA

ILA HARUSI NI UPUMBAVU
 
Ni kuchangia tu gentleman,
ikitokea harusi changa, ikitokea msiba changa, ikitokea michango ya matibabu au elimu changa tu gentleman,

hakuna haja kukwepa kwa makusudi mambo haya ya kijamii ambayo ni madogo madogo tu Lakini ni muhimu sana.

In fact,
vikundi vingi mijini vimejikita zaidi kwenye harusi, misiba, afya, kukopeshana na get-together.
Tuendako elimu itapewa umuhimu wake tu 🐒
 
Siku hizi sichangii hovyo masuala ya harusi, maana ni kutiana umaskini tu.

Mtu unataka kufanya sherehe kusanya pesa zako alika watu waje sio kuanza kubembeleza kuchangiwa kuwaongezea watu mzigo na kuwajaza kwenye groups za WhatsApp.

Kiukweli Watanzania sisi ni wabinafsi,wanafiki na tuna roho mbaya hatujawahi kusaidiana au kuinuana kwenye mambo ya msingi.
 
Kuna jamaa mmoja hapa nusura nimzabatue makofi, kachapisha kadi za mchango wa harusi watu wamchangie. Cha ajabu anaishi vizuri tu na mke wake na wana watoto wanne! Eti anasema hana ndoa anataka afunge ndoa na huyo mke wake. Sasa si akafunge tu!?. Ni usumbufu kufanya sherehe ya harusi kwa kutegemea mifuko ya watu. Zamani watu walijibeba wenyewe kufanya sherehe bila kuchangiwa. Utalisha watu kwa mfuko wako mwenyewe
 
Sio lazima uanzishe Uzi.

We fanya maamuzi kwamba huchangii harusi basi! Mbona wapo watu kibao hawchangii harusi tena ni watu weny vipato TU!

Ila kwakweli ni upuuzi...unatoa laki yako unagharamia usafiri, viwalo, etc....halafu ukumbini kamati inatoa vinywajibkwa upendeleo kisa wabakishe vinywaji vya kuvunjia kamati. 😂🤣

Kwa laki yako ukienda Chinese restaurant unafaidi taste mpyampya na mkeo mnadumisha upendo shwaaaah
 
~Chavalikungu hapa ,nilifunga ndoa misa ya asubuhi nilipotoka nkaenda zang kufyatua tofali za biashara
Tatizo huwa linaanzia hapaa! Yaani ukichangiwa shughuli yako, nawe jiandae kuandamwa na shughuli za watu. Mimi pia nilifunga ndoa misa ya asubuhi jumamosi moja; kisha wapambe nikawapeleka hoteli tukapata menu na kinywaji kidogo saa 8 mchana biashara kwisha...!
 
AKUPE NANI MTAJI😀 ?? AKUSAIDIE KIAFYA?
LABDA SIO WABONGO WENYE ROHO MBAYA! UKITAKA KUWAPIGA ANDAA HARUSI HALAFU TIMKIA CANADA😀
nina kadi 8 za harusi kila moja kima cha chini single ni 70K
 
Kuchangia msiba sawa kwa sababu ni jambo linalotokea bila kutarajia

Mgonjwa anaweza akachangiwa kwa ajili ya matibabu na akafariki vile vile so kuchangia msiba pia ni jambo la heri
NAUNGA MKONO HOJA NA HILO NALIFANYA KWA KADIRI YA UWEZO WANGU,IKIBIDI HUWA NASHIRIKI
 
KUCHANGIA HARUSI NI UPUMBAVU

MSIBA KWELI MAANA HAUNA HODI NA MASUALA YA AFYA PIA

ILA HARUSI NI UPUMBAVU
nina kadi 8 za harusi kila moja kima cha chini single ni 70K
 
Tatizo huwa linaanzia hapaa! Yaani ukichangiwa shughuli yako, nawe jiandae kuandamwa na shughuli za watu. Mimi pia nilifunga ndoa misa ya asubuhi jumamosi moja; kisha wapambe nikawapeleka hoteli tukapata menu na kinywaji kidogo saa 8 mchana biashara kwisha...!
SIJUTII HILI LAKINI WALINIITA MBAHILI,NKAMCHAPA WIFE KA 1M KA MTAJI
 
Sio lazima uanzishe Uzi.

We fanya maamuzi kwamba huchangii harusi basi! Mbona wapo watu kibao hawchangii harusi tena ni watu weny vipato TU!

Ila kwakweli ni upuuzi...unatoa laki yako unagharamia usafiri, viwalo, etc....halafu ukumbini kamati inatoa vinywajibkwa upendeleo kisa wabakishe vinywaji vya kuvunjia kamati. 😂🤣

Kwa laki yako ukienda Chinese restaurant unafaidi taste mpyampya na mkeo mnadumisha upendo shwaaaah
nina kadi 8 za harusi kila moja kima cha chini single ni 70K
 
Kuna jamaa mmoja hapa nusura nimzabatue makofi, kachapisha kadi za mchango wa harusi watu wamchangie. Cha ajabu anaishi vizuri tu na mke wake na wana watoto wanne! Eti anasema hana ndoa anataka afunge ndoa na huyo mke wake. Sasa si akafunge tu!?. Ni usumbufu kufanya sherehe ya harusi kwa kutegemea mifuko ya watu. Zamani watu walijibeba wenyewe kufanya sherehe bila kuchangiwa. Utalisha watu kwa mfuko wako mwenyewe
NI HUZUNI
 
Kuna msiba wa pili baada ya kuchangiwa Ada na ukoo, maana baada ya kupata elimu na kupata kazi utaitajika kulipa fadhila na endapo kipato chako hakitaweza kumudu kutoa msaada kama wanavyotarajia basi utabeba laana kama zote. Ndiyo maana wengi tunatamani familia zetu/wazazi wangeweza kutusomesha.
 
nina kadi 8 za harusi kila moja kima cha chini single ni 70K
Yani 70k ndo single skuizi
Afu ukienda unakutana na maujinga ya bibi na bwana harusi na marafiki zao👐
Hamna cha maana! Nna card hapa kama zako mpaka nmechoka nazo
 
Kamwe sichangii $TAREH£ na sihitaji KUCHANGIWA, msiba sawa nitatoa rambirambi. sherehe ni starehe, haina ulazima. na ukinilazimisha sana lazima nitamla tako mkeo, usinilaumu.
 
Ni kuchangia tu gentleman,
ikitokea harusi changa, ikitokea msiba changa, ikitokea michango ya matibabu au elimu changa tu gentleman,

hakuna haja kukwepa kwa makusudi mambo haya ya kijamii ambayo ni madogo madogo tu Lakini ni muhimu sana.

In fact,
vikundi vingi mijini vimejikita zaidi kwenye harusi, misiba, afya, kukopeshana na get-together.
Tuendako elimu itapewa umuhimu wake tu 🐒
Nichangie nikale mkuu, sijala
 
Back
Top Bottom