KERO Changamoto Sekondari Mchungaji Mwema: Walimu, Mishahara na Utawala

KERO Changamoto Sekondari Mchungaji Mwema: Walimu, Mishahara na Utawala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
KERO

Mimi kama mzazi na mdau wa elimu shule ya sekondari mchungaji mwema iliyoko chini ya dayosisi ya Kagera nakelwa na mambo kama haya
1. Walimu KUNYIMWA MKATABA ambao ni silaha ya kulinda ajira yao Kwa mujibu wa SHERIA.

2. Mishahara ya kusuasua Kwa WAFANYAKAZI na kulipwa kinyume na SHERIA TSH.200000 badala ya KIMA kilichopendekezwa na SERIKALI.

3. Shule kuongozwa na mkuu wa shule na mtaaluma tu, hakuna delegation of power.

4. Huduma mbovu ya chakula Kwa Watumishi Kwa kuminywa na Mkuu wa shule.

Ombi Kwa meneja wa shule:

Kufanyia kazi changamoto hizo ILI shule kuongeza ufaulu, pia wazazi kushirikishwa kwenye mikutano ya maendeleo ya shule.

Bila hivyo, mkurugenzi na meneja watazidi kulalamika kuhusu ufaulu mbovu Kwa kuwa na utawala hafifu usiojali shule

IMG_20260611_132831_587.jpg
 
Back
Top Bottom