Changamoto nayopitia bank ya FNB

Changamoto nayopitia bank ya FNB

unazunguka dsm, mwanza, dodoma na nje ya nchi nini? Hufiki wilayani, btw hata baadhi ya makao makuu ya mikoa hayana bank hii, kigoma mmojawapo, Mimi pia mteja wa absa since barclays days, lakini ukosefu wa mtandao wa matawi ni big weakness. Hao na kina Equity, Eco bank etc ni bank za mijini tu

Equity unatumia app

Unavuta na kuweka pesa popote
 
Kwa wale wachakarikaji wanaowekewa miamala na wadau wao wa bushi? Ma Makere, Manyovu, kazuramimba huko? Aiseee kule ni zile banki 3 tu wadau ndio wanazijua, wanaofanya biashara kama za nafaka watakuwa wanaelewa changamoto hii.

Anahamisha kutoka kwenye M-pesa

Binafsi nadeposit kutoka kwenye M-pesa kwenda Equity, hamna mambo ya foleni wala safari Za kwenda bank
 
Mrejesho:kwanza kabisa napenda kutoa Shukrani zangu za dhati kabisa kwa wale walioguswa na hili jambo langu kwa kunipa ushauri na namna ya kufanya kama juhudi zikigonga mwamba!
Pia wapo waliotoa maneno ya kejeli n.k,ukweli ni kwamba nilikuwa kwenye kipindi kigumu sana kwa siku hizo 8 kujua hatma ya pesa yangu maana ni pesa niliyokuwa nategemea kwa mambo mengi zije ziyeyuke kizembe namna hii!
Hatimaye tatizo langu limetatuliwa nimetoa pesa zangu na amani imerejea upya inshaallah [emoji120]
 
Ninavyojua tangu mwaka jana au juzi FNB ilikuwa na mpango wa kufunga shughuli zake hapa nchini na nimeshangaa kusikia kwamba bado wanaendelea na operations zao!

Nakushauri ukiweza ondoa kila kitu chako na uweke kwenye benki nyingine kwani huwezi kujua usumbufu utakaotokea endapo watafunga benki kutokana na kufilisika. Hii benki chimbuko lake ni Africa Kusini ni benki kubwa kule.
Huu ushauri unaompa ni wa muda mrefu! Huyu mdau anataka ushauri wa nini kifanyike ili akaunti yake ifunguliwe, sasa ataondoaje kila kilicho chake wakati akaunti imefungwa?
 
Nimejaribu kupiga simu huduma kwa wateja wanasema ombi langu wanalishughulikia hadi nimechoka wakuu!
Msaada wakuu nina ninachotakiwa kufanya maana mipango yangu imesimama huku nikiteseka na pesa zangu mwenyewe!
Usiishie kuongea tu na hawa umbwa wa kwenye kaunta ingia kwa meneja ueleze shida yako. Kuwa serious usicheke nao maana hiyo ni haki yako!
 
Me natumia KCB the only downsides are

1. Sijaonaga mawakala wao japo hapa mjini matawi yapo yapo. Uhuru, Lumumba, Samora, Msasani, Buguruni, Mlimani city na Mbagala, Pia wana ATM msimbazi. Kwa mikoani wana Branch Moro, moshi na Zanzibar.

2. Downside ya pili ni Card yao ya Visa siyo 3D secured, Hivyo inanibana kufanya POS kwenye baadhi ya sites. Sijajua kama wana aina nyingine ya Card ambayo ni 3d secured.

The rest wapo Okay.

Niliendaga BancABC uhuru Heights kufungua account, wakaniambia nilete barua ya utambulisho nikaona uchawi.

Ila nasikia ni bank nzuri.
Kitambulisho tu cha taifa unafungua account
 
Hii ni last option mkuu,maana ukienda huko bank inapigwa faini kubwa sana
Yes i know...na fine ni one million kwa kila siku tangu issue imerepotiwa bila kufanyiwa kazi.so kama issue ipo pending for 30 days..basi itakua ni 30*1000,000 so total ni 30,000,000m.. therefore wwkipigwa fine ndo adabu itakuja na hiyo option yakwenda BOT ni last option baada ya hizi jitihada zake za kuhangaika na Exim bank(fnb acquirer) kugonga mwamba. Na anataikiwa a lodge official complaint kwenda bank husika na a baki na copy yake ya complain lodgement na agongewe muhuri wakuonesha complain yake ilikua received.
 
Barclays
Wana service nzuri Jamani

Ila Equity sihami
Mwaka wa 5 Equity Bank Tz sijawahi kupata shida yoyote zaidi ya max withdrawal amount kufika Branch yao ilikuwa solved ndani ya dk 5 nikasepa

Tawini naenda kufanya miamala tu Hawa wakenya Technology yao sio ya kitoto

NMB ninayo kupokea miamala ya watu tu na pesa za ndogo za matumizi, CRDB washenzi wakubwa
 
Back
Top Bottom