Changamoto nayopitia bank ya FNB

Mnyiramba

JF-Expert Member
Jun 19, 2022
1,112
2,957
Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa hii bank ya Fnb kwa muda mrefu sana na sikuwahi kupitia changamoto yeyote hadi wiki iliyopita ndio nikakutana na kizaazaa!

Ipo hivi hii bank huwa natumia kusave vipesa navyopata kwa malengo ya muda mrefu kwavile huwa hawana makato ya hapa na pale!

Sasa wiki iliyopita nikawa na shida na pesa yakuzungushia kwenye biashara yangu inabidi niende kuchukua kama milioni 3 hivi mara naambiwa akaunti yangu imeblokiwa kwahiyo siwezi kufanya muamala wowote!

Sema kweli nilichanganyikiwa kutokana nilikuwa nahitaji hiyo pesa haraka sana iwezekanavyo!

Ikabidi niulize kulikoni kufunga account ya mteja bila taarifa yeyote bila sababu za msingi? Nikajibiwa kwamba inabidi nijaze taarifa zangu upya za ki bank!

Kweli nikafanya hivyo na ukizingatia pia nilishajaza taarifa zangu upya miaka miwili tu iliyopita,lkn cha ajabu hadi leo siku ya 8 hawajafungua akaunti yangu ni danadana tu kwa kwenda mbele,nimeenda bank mara mbili mwendo ni kujaza fomu kila kukicha!

Nimejaribu kupiga simu huduma kwa wateja wanasema ombi langu wanalishughulikia hadi nimechoka wakuu!
Msaada wakuu nina ninachotakiwa kufanya maana mipango yangu imesimama huku nikiteseka na pesa zangu mwenyewe!
 
Ninavyojua tangu mwaka jana au juzi FNB ilikuwa na mpango wa kufunga shughuli zake hapa nchini na nimeshangaa kusikia kwamba bado wanaendelea na operations zao!

Nakushauri ukiweza ondoa kila kitu chako na uweke kwenye benki nyingine kwani huwezi kujua usumbufu utakaotokea endapo watafunga benki kutokana na kufilisika. Hii benki chimbuko lake ni Africa Kusini ni benki kubwa kule.
 
Ninavyojua tangu mwaka jana au juzi FNB ilikuwa na mpango wa kufunga shughuli zake hapa nchini na nimeshangaa kusikia kwamba bado wanaendelea na operations zao...
Kwa maneno haya unataka kusema mdau atakuwa amepigwa kwenye mshono? Nayajua maumivu yake.

Hizi bank za kuunga unga toka ile efata iondoke na million nane zangu hunikuti humo, NMB na CRDB japokuwa wana vitozo vya ajabu ajabu lakini bado wanafaa sana kwa sisi wa vipato vya kawaida.
 
Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa hii bank ya Fnb kwa muda mrefu sana na sikuwahi kupitia changamoto yeyote hadi wiki iliyopita ndio nikakutana na kizaazaa...
Kwanza pole. FNB bank walikua acquired na Exim bank, mwaka 2022 mwezi july..so all assets and liabilities (customer deposits) za fnb zilihamishiwa Exim bank.

Therefore that being a case all complains regarding your fnb account zinatakiwa kua handled na Exim bank..so endapo jitahada zitagonga mwamba Basi nenda BOT dawati/section ya customer compliant watashughulikia issue yako immediately.

(kumbuka BOT walitoa regulation inayohusina na consumer protection kwa wateja wa mabenki..na kuweka timelines(SLA ya kila tatizo na duration ya kutatuliwa such that hiyo duration ikizidi basi mteja a lodge complain yake BOT.
 
Kwanza pole. FNB bank walikua acquired na Exim bank..mwaka 2022 mwezi july..so all assets and liabilities (customer deposits) za fnb zilihamishiwa Exim bank.. therefore that being a case all complains regarding your fnb account zinatakiwa kua handled na Exim bank..so endapo jitahada zitagonga mwamba Basi nenda BOT dawati/section ya customer compliant watashughulikia issue yako immediately.(kumbuka BOT walitoa regulation inayohusina na consumer protection kwa wateja wa mabenki..na kuweka timelines(SLA ya kila tatizo na duration ya kutatuliwa such that hiyo duration ikizidi basi mteja a lodge complain yake BOT.

Asante kwa ushauri mkuu,nasubiri hadi Jumatatu kama bado kimya naanza huo mchakato
 
NMB CRDB NBC hizi ndiyo bank za TANZANIA za uhakika na salama muda wote... Tatizo lenu WaTz mnapenda sana vya bure mnataka muweke pesa bank isikatwe hata shilingi mia, sasa bank itajiendeshaje kama sio kufa na kudhulumu wateja...
 
Kwanza pole. FNB bank walikua acquired na Exim bank, mwaka 2022 mwezi july..so all assets and liabilities (customer deposits) za fnb zilihamishiwa Exim bank.

Therefore that being a case all complains regarding your fnb account zinatakiwa kua handled na Exim bank..so endapo jitahada zitagonga mwamba Basi nenda BOT dawati/section ya customer compliant watashughulikia issue yako immediately.

(kumbuka BOT walitoa regulation inayohusina na consumer protection kwa wateja wa mabenki..na kuweka timelines(SLA ya kila tatizo na duration ya kutatuliwa such that hiyo duration ikizidi basi mteja a lodge complain yake BOT.
Wewe ni Afisa wa Bank gani? Nataka nije kufungua Fixed deposit, Mnatoa rate ngapi kwa USD 200,000
 
Back
Top Bottom