Juzi kati yalinikuta NMB.
Nilikuwa sina hata 100 nikamchukua boda hadi OPEN pale biafra, kufika pale wanaweka hela. Kutokana na haraka zangu nikamwambia boda twende Morocco, kufika pale tukaambiwa ATM mbovu ina siku 2. Nikamwambia boda turudi OPEN watakuwa wameshaweka hela.
Baada ya kufika, aliyekuwa mbele yangu mteja wa bank tofauti na NMB, hela ilitoka na alipata msg, but hela haikutoka.
Roho ilisita kutoa lakini nikafanya kama nacheza kamari tu. Nikatoa, ATM ikahesabu hela kisha ikatulia na ikahesabu kwa mara ya pili, ikafungua kimlango cha kutolea hela na kufunga tena. Hapo hapo nikapata msg kuwa nimetoa hela, but no hela.
Baada ya dakika 2 nikapata msg kuwa hela imerudishwa kwenye akaunti, nikajaribu kutoa tena, ikanifanyia mchezo ule ule.
Hapo nikaamua kwenda Mwanamboka ATM ya CRDB na ndio nikafanikiwa.
Sasa hivi kadi yao nikichomeka ATM nikichagua lugha tu inatema, nikienda ATM tofauti na NMB inafanya kazi. Nilirepot tatizo wanasema kabda imekufa niombe nyingine.
Hizi ndio bank za kiz