Msaada ameyakanyaga Bank ya ABC

Adolph Jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
5,560
8,638
Nimepokea, taarifa usiku huu za rafiki yangu aliyepatwa na msiba mwishoni mwa mwaka jana na kuzika January mwaka huu.

Ni mtumishi wa serikalini kapatwa na msiba ghafla akaenda kukopa Bank ya ABC ili kumsaidia na masuala ya msiba, Tsh milioni 2 hiyo tarehe 29/12/2023.

Kaambiwa baada ya masaa 24 pesa itaingia ila hadi leo tarehe 8/01/2024 pesa hakuna na kwa taarifa ni kuwa, taarifa zake kwa mkuu wake wa kazi zimeishapita kasaini apewe mkopo ila kaambulia patupu hadi leo.

Msiba uliishaisha kwa msaada wa raia wema wakamkopesha akayamaliza huko kwao, sasa ndiyo naongea naye hapa anaomba ushauri jinsi ya kujitoa kwenye mkopo huu hewa.

Msaada kwa huyu ndugu kama ni wa kisheria ajitoe tu kwenye hili janga.
 
Duh kama masuala hayakukaa sawa aende benki aka-cancel, sema sasa alisemaje wakati anakopa?,

kama ni business wata-force auchukue maana sidhani kama kuna taasisi itakupa mkopo kwa kigezo cha msiba lazima tu upige fix mahali

Ikishindikana nenda BOT watakusaidia kukunasua, sijajua hakika kwa angle yako ila kuna mtu namfahamu alitapeliwa hela na mojawapo ya wakala wa taasisi za fedha, alivyoomba kurudishiwa akazungushwa mwishoni alienda BOT wakamsaidia
 
Nimepokea, taarifa usiku huu za rafiki yangu aliyepatwa na msiba mwishoni mwa mwaka jana na kuzika January mwaka huu.

Ni mtumishi wa serikalini kapatwa na msiba ghafla akaenda kukopa Bank ya ABC ili kumsaidia na masuala ya msiba, Tsh milioni 2 hiyo tarehe 29/12/2023.

Kaambiwa baada ya masaa 24 pesa itaingia ila hadi leo tarehe 8/01/2024 pesa hakuna na kwa taarifa ni kuwa, taarifa zake kwa mkuu wake wa kazi zimeishapita kasaini apewe mkopo ila kaambulia patupu hadi leo.

Msiba uliishaisha kwa msaada wa raia wema wakamkopesha akayamaliza huko kwao, sasa ndiyo naongea naye hapa anaomba ushauri jinsi ya kujitoa kwenye mkopo huu hewa .

Msaada kwa huyu ndugu kama ni wa kisheria ajitoe tu kwenye hili janga.
Akishapokea hizo pesa azirejeshe tu kama malipo ya mkopo siku hiyo hiyo. Itakuwa haijaanza Riba.
 
Duh kama masuala hayakukaa sawa aende benki aka cancel, sema sasa alisemaje wakati anakopa kama ni business watafirce auchukue maana sidhani kama kuna taasisi itakupa mkopo kwa kigezo cha msiba lazima tu upige fix mahali

Ikishindikana nenda BOT watakusaidia kukunasua, sijajua hakika kwa angle yako ila kuna mtu namfahamu alitapeliwa hela na mojawapo ya wakala wa taasisi za fedha, alivyoomba kurudishiwa akazungushwa mwishoni alienda BOT wakamsaidia
BOT mkoani?
 
Msiba wa mzazi, mwenza au mtoto serikali/ofisi yake hugharamikia.
Ilikuwaje akakope au ni msiba usiotambulika ofisini kwake?
Au yuko local government?
Maana huko local government mambo yenu mnayajua wenyewe.
Mwajiri wake ndiye anaweza ku cancel huo mkopo within 5 minutes.
So, asisumbue madalali wa bank ABC
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom