Changamoto katika mashine saka – search engine


Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
52
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 52 0
CHANGAMOTO KATIKA MASHINE SAKA – SEARCH ENGINE

Kwa watumiaji wa Kompyuta haswa wale wanaotembelea mitandao mbalimbali ya kompyuta duniani kitu Mashine Saka sio kigeni kwao , wamekuwa wakitumia Mashine Saka kwa kazi zao nyingi sana hata hivyo Mashine Saka hizo zimezidi kukuwa kwa kasi kutokana na tekinologia mbalimbali zinazotumika kujenga Mashine Saka hizo , kwa kuongezewa vitu vingine ili watu waweze kupata njia rahisi zaidi katika kutafuta taarifa na mengine mengi wanayotaka katika mitandao .

Mimi ni kati ya watu wanaotumia sana Mashine Saka kama sio kutafuta taarifa basi nitaangalia jinsi taarifa Fulani inavyosambaa , watu wanavyochangia kupitia programu zingine zilizounganishwa na Mashine Saka hizo , siku hizi unaweza hata kutumia simu yako ya mkononi kutafuta vitu kadhaa Kwenye Mashine Saka hizo .

Pamoja na kukuwa huku kwa teknologia , taarifa na mambo mengine mengi , yatupasa kuanza kudodosa baadhi ya vitu ambavyo inawezekana wengi hawajui au wamewahi kukutwa na vitu kama hivyo bila kujua ni nini kinachoendelea .

Kutokana na kukuwa sana kwa biashara mbalimbali za mitandao hii inahusiana pia na wale watu wanaotumia mitandao hiyo kwa ajili ya kutafuta bidhaa na taarifa mbalimbali ambazo wao wanazitaka kwa wakati Fulani , pia kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu kwa njia ya mtandao haswa kwenye sehemu ya majibu ya taarifa ambazo mtu anatafuta .

Unaweza kufungua www.naombakazi.com hii inahusu masuala ya kazi nafasi za masomo na makala mbalimbali , mfano ukianza kutafuta taarifa za naombakazi kupitia Mashine Saka utapata nyingi sana lakini unaweza kukuta nyingi ya taarifa hizo zinaweza kuwa kwa ajili ya kuanzisha uhalifu wa aina Fulani kwa njia ya mtandao .

Kwa mfano unaweza sasa kufungua naombakazi.com , kwenye majibu ya kwanza unaweza kuona vizuri lakini jinsi unavyozidi kwenda unaweza kuona unakutana na vitu kama cashjobs , salesjobs na vitu vingine kama hivyo , sasa kama mtu anatafuta kazi za mauzo kwa mfano atashawishika kuingia kwenye tovuti ya salesjobs.com kwa mfano kuangalia ni nini kinachoendelea huko .

Sasa unaona kwa kutafuta naombakazi.com ukakutana na salesjobs.com , ndani ya sales jobs unaweza kukutana ndio na nafasi za kazi zinazohusiana na sales lakini ambazo unatakiwa ulipie kiwango Fulani cha pesa au malipo ya aina Fulani ili uweze kupata kazi hiyo au upendeleo Fulani , sio hiyo tu unaweza kukuta kuna hata ofa za programu za kompyuta zinazohusiana na mambo ya sales , huku ukiendelea na kutafuta zaidi program za ajabu zinaweza kuingia kwenye komputa yako bila ya wewe kujua .

Hapo hapo unatakiwa ujue kwamba tovuti nyingi sana zinatabia ya kukusanya taarifa za watu wanaotembelea tovuti zao pamoja na kujua wakati unatembelea anuani yao ulitokea tovuti gani taarifa hizi zinaweza kutumika na wenye tovuti hizo kwa ajili ya masuala yao mengine ya kibiashara kwa siku za mbeleni au kuuzia watu wengine hata wahalifu kwa kazi zao za kihalifu .

Tunapata funzo moja hapo ni vizuri unapotafuta vitu kwa njia ya mtandao uhakikishe hauko ndani ya anuani yako ya barua pepe kwasababu unapotafuta taarifa zao zinaenda mikononi kwa watu wengine hili unaweza kuzuia pale unaposajili anuani hiyo kwa kuzuia taarifa hizo zisihifadhiwe .

Unaposikia mtu Fulani ameibiwa taarifa zake binafsi kwa njia ya mtandao moja ya njia rahisi ni hii ya kujua tovuti ambazo mtu anatembelea , sehemu ambazo anaweka taarifa zake zingine kama kwenye mitandao jamii kama facebook au hi5 , rafiki zake kwenye mitandao hiyo hiyo jamii , vitu anavyopenda kuchangia kwenye majukwaa hayo .


Hili ni tishio ambalo watu wanatakiwa wawe makini nalo sana sasa hivi na hata siku chache zijazo , pamoja na kwamba kampuni nyingi zinazotengeneza bidhaa za ulinzi kama antivirus , antispyware na firewalls kuwekeza sana kwenye kupambana na uhalifu wa aina hii lakini bado mashambulizi yanaonekana kuzidi maradufu .

Moja ya kitu ambacho ni changamoto kwa kampuni hizi ni kuwa na database moja yenye taarifa muhimu za masuala ya uhalifu na matishio mengine ingawa hili linaweza kuwa tatizo kwa sababu kila kampuni inataka kuvuta wateja wengi kwenye kutumia bidhaa zake pia kuna kampuni ambazo mtindo wake wa kufanya updates ya vitu ni mwepesi kutokana na teknologia wanazotumia kwahiyo inaweza kuleta madhara kwa bidhaa zingine .

Pia kuna kampuni ambazo ni kubwa hizi zidhani kama zitapenda kuwa kitu kimoja na kampuni ndogo kwenye shuguli hii , hizi kampuni zimewekeza sana kwenye masuala mbalimbali kwa muda mrefu na kutumia pesa nyingi zisingependa kushindanishwa kwenye masoko na wachipukiaji .

Bila kusahau ni kampuni gani haswa ziruhusiwe kujiunga na database hiyo , kuna kampuni zenye antivitus pekee , kuna zingine zina antivirus , internet security , kuna zingien zenye antivirus zenye antispyware na bidhaa zingine zilizounganishwa ndani .

Cha mwisho ni suala la Lugha , kampuni nyingi za bidhaa zinazofanana na hizi hazijawa na mipango inayoeleweka ya kuweka bidhaa zao kwenye lugha zingine ili iwe rahisi kwa watu wa huko mfano sisi tunatumia Kiswahili ni vizuri tungekuwa na bidhaa zilizokuwa kwa Kiswahili na taarifa zake ziwe kwa lugha ya kwetu ili iwe rahisi kwa watu wengi kutumia na kusoma habari mpya zinazotoka zinazohusu bidhaa husika .www.naombakazi.com www.bonyeza.blogspot.com www.wanabidii.net
 

Forum statistics

Threads 1,250,869
Members 481,514
Posts 29,748,920