Changamoto gani ulikutana nayo lakini ikageuka kuwa fursa ya kukufikisha?

g dex

Member
Feb 12, 2021
8
4
Habari zenu wataalam,

Najua wengi wetu tumepiga hatua tulipo sasa baada ya kukutana na changamoto fulani huko nyuma ambayo imekua ni fursa.

Kuna kijana wa karibu nilikua namuona ana jitihada sana katika masomo ya habari (chuo kikuu) nilipojaribu kumuuliza ni kipi kinachomfanya awe bize zaidi kwenye kile anachokisomea akanijibu ni kwa sababu ana shauku ya kuja kumwonesha mzazi wake ambae alimkatalia kusoma kidato cha tano na kweli kijana alishindwa kusoma kidato cha tano kutokana na ukaidi wa baba.

Basi aliamua kuenda chuo kuanza cheti kwa siri na baadae mzazi wake alijua. Mzazi wake huyo huyo alikataa kumlipia ada isipokua relative's wake walikua wakimptia msaada wa mwaka wa kwanza.

Na ni kweli sasa kijana ameajiriwa baada ya kupata cheti, huku sasa anaendelea kusoma diploma.

Nikaona changamoto yake ya kukataliwa kusoma na mzee na kutokupewa ushirikiano katika suala la ada ilimsaidia kupambana mpaka kupata ajira hiyo.

Sasa tujikumbushe na sisi changamoto zilizotukumba ambazo baadae ziligeuka kuwa Fursa ili iwatie hamasa wengine.

Asanteni
 
Nikihadithia changamoto yangu naweza nisimalize nikaaandika itaendelea. Alafu wadau kwa hasira wanaweza kunitupia hata jini.

Lakin bila changamoto kutoboa ni ngumu. "Comfort zone is a great place but nothing grow there"
 
Nimesoma chuo miaka 6 kuanzia cheti mpka jiwe. Lakini kipindi nasoma nilikuwa najisikia vibaya sana. Niliosoma nao secondary walikuwa kila mara wananiuliza sijamaliza tu kusoma? Ikafikia hatua kama hawajaniona maeneo ya chuo nawaambia nilishamaliza kumbe bado.

Hii hali ilinikosesha amani kabisa nikawa najutia kwanini sikuenda advanced yaan form five na six? Hii ilitokea baada ya kupata ushauri kutoka kwa mtu wangu wa karbu.

Baada ya kumaliza masoma nimehangaika kutafuta kazi kwa cheti cha degree lakin matokeo yake ile certificate ndo inaniweka mjin zaidi hata ya mwenye degree.
 
Nikihadithia changamoto yangu naweza nisimalize nikaaandika itaendelea... Alafu wadau kwa hasira wanaweza kunitupia hata jini


Lakin bila changamoto kutoboa ni ngumu. "Comfort zone is a great place but nothing grow there"
Hahahah uhakika mzee
 
Back
Top Bottom