Changamoto ya kigezo cha kupitia JKT kutumika kama sifa kuu kujiunga na Majeshi nchini

ministrant

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
554
1,134
Wasalaam,

Kumekuwa na changamoto kubwa kwa vijana wengi wenye sifa kujiunga na Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kama vile Polisi, Magereza na JWTZ kukwama kujiunga kutokana na kukosa kigezo kimoja tu kuwa hawakupita mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.

Hii inapelekea vyombo hivi kupoteza vijana wengi wenye weledi kujiunga na vyombo hivyo kwa kukosa fursa ya kupita JKT kutokana na mifumo iliyopo kujiunga na JKT.

Napendekeza hiyo ibaki tu kuwa sifa ya ziada ili kutoa fursa sawa ya ushindani kutokana na mifumo ya kielimu kutowapa fursa ya wao kupita huko.

Kwa mfano kijana amemaliza kidato cha nne au sita lakini shule yake haikuwamo katika orodha ya wanaotakiwa kupatiwa mafunzo hayo kwa mwaka husika, hivyo kupelekea kijana huyu kwenda chuo moja kwa moja mathalani na kuchukua masomo ya udaktari wa Binadamu na baada ya kuhitimu akakosa sifa ya kujiunga na vyombo hivyo eti kwakuwa tu hakupita JKT.

Napendekeza Serikali ifanyie marejeo utaratibu huu ukiachilia mbali uwezo mdogo wa kambi za JKT kutoa mafunzo kwa kila kijana aliyefikisha umri wa miaka 18 na kuendelea.

Pia hivi sasa kumeibuka ubaguzi hata kwa hao waliopitia JKT katika ajira kipaumbele kinatolewa kwa waliojitolea miaka 2 na kuwakataa wale waliopitia mafunzo hayo hayo kwa mujibu wa sheria baada ya kuhitimu kidato cha 6.

Kupita JKT ni jambo jema lakini kuna nguvu kazi kubwa na yenye weledi wa hali ya juu inapotes mtaani ambayo ingekuwa msaada kwa vyombo vyetu lakini inakutana na changamoto hiyo.
Nawasilisha

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Wasalaam,
Kumekuwa na changamoto kubwa kwa vijana wengi wenye sifa kujiunga na Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kama vile Polisi, Magereza na JWTZ
Kwa hiyo unatakaje ndugu?vijana wengi wakiambiwa waende JKT wanakataa iwe kwa Kujitolea(Form Four)au kwa Mujibu wa Sheria(Form Six)

Sasa kama walichaguliwa na wakakataa,basi na Ajira haziwahusuS
Labda sema kwa wale ambao wanakuwa hawajachaguliwa kwenda JKT ndio wana Haki ya kulalamika,lakini waliochaguliwa na wakakataa kwenda walie tu
 
Wakimaliza six wanachaguliwa JKT bado kuna fursa za kwenda kwa kujitolea wewe ulitakaje kwamfano
 
Wewe jamaa hukwenda JKT na unataka kazi ya Jeshi; unatafuta huruma ya bi FaizaFoxy ili akipita humu basi aku PM au aondoe hicho kigezo. Kwanza bi mkubwa alipita humu asubuhi saivi yupo bussy na mawaziri umefeli
 
Wewe jamaa hukwenda JKT na unataka kazi ya Jeshi; unatafuta huruma ya bi FaizaFoxy ili akipita humu basi aku PM au aondoe hicho kigezo. Kwanza bi mkubwa alipita humu asubuhi saivi yupo bussy na mawaziri umefeli
Mkuu mimi umri wa kutafuta ajira umeshapita nawazia kikokotoo tu hapa nilipo, nawasaidia vijana waliopishana na fursa ya ajira na kuvitakia mema vyombo vyetu wasije wakaacha watu potential mtaani kisa tu hawakuvaa pensi za Blue na 'T-shirt' za kijani
 
Back
Top Bottom