CHAMI: Ekelege na Joyce wameniponza

Kwani majukumu ya waziri ni yapi? na je yeye kama waziri aliyatekeleza majukumu yake vipi? Je uwaziri maana yake ni kutia sahihi kila kitu kinacholetwa kwako bila kukihakikisha? Kama maamuzi yale yote yalikuwa na idhini ya waziri basi asitafute wa kumlaumu hata kama yeye mwenyewe hakula kitu.
 
Wana JF baada ya badiliko la mawaziri lililopelekea aliyekuwa waziri wa viwanda na Biashara ndg Cyril Chami kutemwa,imedhihirika ripoti zote za CAG hazimtaji moja kwa moja ila ni Ekelege(mkurugenzi mkuu TBS na katibu mkuu wake bi Joyce Mapunjo ambao wamekuwa wakila dili
"Kilichoniponza ni kutoipitia taarifa ya CAG na kutoa mapendekezo kama waziri,pia nilimuamini sana katibu mkuu ambaye yeye na wenzake walinigeuka na kuanza kuwa makuwadi wa kampuni feki za ukaguzi ambazo ni zao wenyewe tena hewa..
Nimegundua kosa langu la kumtetea Mkurugenzi wa TBS na kampuni zao.
Najua kama alivyosema rais na wao wataniafuata"
Mwisho wa kunukuu.
Hizi habari toka kwa Mtumishi wa ofisi yake ambae walikuwa nae jana usiku wakisikitika.

Mheshimiwa Chami ni mbunge. Kama anayosema ni kweli basi tuone kikao cha bunge kijacho atatoa hoja gani regarding hawa wezi. What makes the next bunge session interesting is the fact that wabunge kama Mheshimiwa Chami watakuwa back-benchers kwa mara ya kwanza na macho yote yatakuwa kwao kuona kama wana la kusema against serikali ambayo imewatupilia nje. Yetu macho.
 
Sasa serikali ijkiandae kupokea Makombora ya Maangamizi toka kwa majeruhi hawa
Mheshimiwa Chami ni mbunge. Kama anayosema ni kweli basi tuone kikao cha bunge kijacho atatoa hoja gani regarding hawa wezi. What makes the next bunge session interesting is the fact that wabunge kama Mheshimiwa Chami watakuwa back-benchers kwa mara ya kwanza na macho yote yatakuwa kwao kuona kama wana la kusema against serikali ambayo imewatupilia nje. Yetu macho.
 
Kuna kila dalili kwamba ugonjwa unaomsumbua Chami umeuathiri mfumo wake wa fahamu. Maneno haya Kama kweli kayasema yanaendelea kuthibitisha athari hizo.
 
source YA MANENO YA CHAMI TAFADHALI.

ILA EKELEGE ALIZIDI KUJIBIZANA NA AKINA FILIKUNJOMBE, KWANI CHAMI HAKUONA HILI? HE IS A GOOD GUY, BUT HE HAS TO PAY THE PRICE
 
Hakika,kwa hili,Chami ameonewa!

Chami ameonewa na nani wewe? Alipewa ushauri wa kutosha ambao angeufata usingemfikisha hapa alipo-acha abebe matokeo ya ubishi au woga wake. Ukiniambia Nundu naweza nikakubaliana na wewe, hapa nahisi Mfutakamba ndiye amemponza huyu bwana
 
na ndio akome yeye kapewa mamlaka sasa kama mda wa kuisoma ripoti hana ndio atatia akili kwani ni uzembe

hahahaaa kama hana muda wa kusoma ripoti ya CAG , je anao wa kusoma hayo mamikataba wanayoingiaga?
 
Back
Top Bottom