Wakubwa mimi mtazamo wangu naona kama Maawaziri wengi ni wahanga wa mfumo mbaya wa utawala ambao tunao Tanzania.Mamlaka karibu yote ya utawala yako kwa raisi wa nchi ambae amehodhi nguvu zote.Waziri na hata waziri mkuu hawana mamlaka yoyote ya kuwawajibisha Wakurugenzi wa mashirika,wizara,au makatibu wakuu,ambao ndio hasa madudu yanapofanyika.Kinachofanyika ni kwamba waziri/waziri mkuu anatoa ushauri tu kwamba fulani hafai utendaji wake.Mimi nafikiri lawama zote za wizi huu apelekewe mkuu mwenyewe maana yeye ndio aliowachagua hao wahuni wezi wa mali zetu na ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuwawajibisha.
Mimi siamini kama Ekelege na timu yake wamefanya madudu yote hayo kwa muda mrefu bila usalama wa magamba kumfikishia taarifa mkuu,isipokuwa tu aliona uzito kuwatoa maswahibu wake.
Tusiridhike na kubadilishiwa sura za mawaziri bali kinachotakiwa ni kupambana katika marekebisho ya katiba mpya kujenga mfumo mzuri wa uwajibikaji ambao nguvu ya utawala itatawanyika badala ya kubaki kwa mtu mmoja tu.
Tujenge mfumo ambao Waziri mkuu kama mtu anaesulubiwa kwa utendaji wa serikali bungeni apewe uwezo wa kuhire and fire watu wa timu yake.Hii itampa nguvu ya kweli ya usimamizi wa shughuli za serikali.
Na mawaziri nao wajengewe uwezo wa kuondoka na shingo za watendaji walio kwenye wizara zao.Isiwe mtu mwingine achague watu waajabu na wala hamuwezi kumuhoji kawateua kwa kigezo kipi halafu madudu yao wakifanya wanaowajibishwa mawaziri ambao pengine toka siku ya kwanza hawajaridhika na utendaji wao.