CHAMI: Ekelege na Joyce wameniponza

CHAMI: Ekelege na Joyce wameniponza

nikiachia uwaziri jimbo langu la Moshi Vijijini 2015 litakwenda CDM' mwisho wa kunukuu

sasa ngoja hiyo 2015 ataona kama atapata hata robo ya kura alizopata

2010 pumbavu kabisa
 
Anasikitika nini? Kwa hiyo sisi tusio mawaziri ni nyau? Wananchi wa jimbo lake hawakumchagua awe waziri, bali awe mbunge.
 
Anajitetea tu huyo. Ninavyomfahamu Joyce inawezekana aliripoti na yeye waziri alimtetea. Tungoje nao watakavyojitetea. Siri zote zitafichuka>
Wana JF baada ya badiliko la mawaziri lililopelekea aliyekuwa waziri wa viwanda na Biashara ndg Cyril Chami kutemwa,imedhihirika ripoti zote za CAG hazimtaji moja kwa moja ila ni Ekelege(mkurugenzi mkuu TBS na katibu mkuu wake bi Joyce Mapunjo ambao wamekuwa wakila dili
"Kilichoniponza ni kutoipitia taarifa ya CAG na kutoa mapendekezo kama waziri,pia nilimuamini sana katibu mkuu ambaye yeye na wenzake walinigeuka na kuanza kuwa makuwadi wa kampuni feki za ukaguzi ambazo ni zao wenyewe tena hewa..
Nimegundua kosa langu la kumtetea Mkurugenzi wa TBS na kampuni zao.
Najua kama alivyosema rais na wao wataniafuata"
Mwisho wa kunukuu.
Hizi habari toka kwa Mtumishi wa ofisi yake ambae walikuwa nae jana usiku wakisikitika.
 
katika hili, hata kama siyo mpenzi wa mageuzi, inabidi kuwashukuru chadema.  vuguvugu lao la kisiasa limesaidia kuamsha wengi na dhana ya kuwajibika inaanza kukubalika na kufanya kazi.  na kwa mtindo huu, na kama rais Kikwete atatekeleza azma ya kuwajibisha wote wanaofanya madudu wizarani, serikali za mitaa na kwenye mashirika ya umma, hakuna sababu ya ccm kutopeta mwaka 2015 kwa kuwa itakuwa imerejesha imani ya wapiga kura.  kitendawili ni kama watawajibishwa na kwa wakati unaostahili.  agenda ya uwajibikaji haijafungwa bado.  tutaendelea kusubiri.  mpaka sa sasa kwa rais Kikwete (pamoja na Baraza kuwa kubwa kwa kulinganisha na uwezo wa uchumi wa taifa) tunaweza kusema Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Nakumbuka alilaumu kuwa CAG kwapa ripoti wapinzani akina Nassari wakati yeye waziri hajapewa
Sawa kabisa mdau.
Sasa waziri kama huyu inaonesha haijui kabisa Wizara yake, hakutakiwa kupewa ripoti ya CAG maana yeye hakumuajiri CAG, CAG ni mteule wa Rais. Hata kabla ya CAG hajatoa ripoti, yeye kama waziri mwenye dhamana alitakiwa ajue wapi pana mianya ya ubadhirifu kabla na kuanticipate measures mapema. Hata kama kweli hahusiki na ubadhirifu ni wazi huyu uwaziri hauezi.
 
Kuna utetezi wake mimi sikuupenda,kwamba yeye ripoti ya CAG aliiona bungeni!!hivi kwanza tujiulize,ina maana kwamba yeye hakujua bungeni wanaenda kwa masuala gani,mimi nijuavyo unakuwa unajua kuwa ktka bunge mfano la saba,mada zitakazojadiliwa ni moja,mbili,tatu n.k.n.k,sasa kaka yangu ,ina maana wewe hukujua kuwa ripoti za CAG zitaenda kujadiliwa?kwa vyovyote ulijua,sasa iweje hata kama hukuletewa ripoti mezani kwako kabla hujaenda bungeni,si ungeifuatilia upewe ili uifanyie kazi,yani kwa kuwa hawakukupa nawe ukakaa kimya!mmmmmh!hapa kuna utata!anyway,karibu tena uraiani
 
nikiachia uwaziri jimbo langu la Moshi Vijijini 2015 litakwenda CDM' mwisho wa kunukuu

sasa ngoja hiyo 2015 ataona kama atapata hata robo ya kura alizopata

2010 pumbavu kabisa

Punguza hasira Mkuu Mods are online.
 
Jinga hilo wacha liende kuwahudumia wananchi jimboni na akajibu maswali kwa nini amekwiba pesa za umma na kutetea wezi wenzake. Tondolubeta
 
Sawa kabisa mdau.
Sasa waziri kama huyu inaonesha haijui kabisa Wizara yake, hakutakiwa kupewa ripoti ya CAG maana yeye hakumuajiri CAG, CAG ni mteule wa Rais. Hata kabla ya CAG hajatoa ripoti, yeye kama waziri mwenye dhamana alitakiwa ajue wapi pana mianya ya ubadhirifu kabla na kuanticipate measures mapema. Hata kama kweli hahusiki na ubadhirifu ni wazi huyu uwaziri hauezi.

Huyu ni taahira kabisa hata huo uwaziri sio aliupata vipi! Kabla hata ya ripoti ya CAG wabunge walishapiga kelele kuonyesha ufisadi wa makampuni ya ukaguzi lakini hakufanya chochote, Naibu wake alimtaarifu na kumpa ushauri wa kumsimamisha kazi Ekelege lakini alipuuza-sasa analaumu watu wengine; hili ni kubwa jinga!!!!
 
Huyu jamaa ni buege wa kutupa..Watafuata wapi? Kwa kauli ya jana JK amesema 'kwa misingi ya sasa', thats means from now on (from yesterday- 4 May 2012) ndio watafuata, manake kwamba dhambi ya kabla ya hapo zimesamehewa!

Unajua baada ya watu wengi ku'ipindisha' hiyo kauli ya mkuu, nikaanza kuquestion uelewa wangu. Coz nilielewa kuwa next time, wengi watahusika; na kwa mtazamo wangu that was very weak of him. Why next time why not now, wakati sheria inaruhusu.

Na kingine ni swala la kutuhumu kuwa watu wengine wanapika majungu/fitina; yaani pale ndipo aliponichefua zaidi. Yaani kinachomuuma mkuu ni hao maswahiba wake kupikiwa majungu na wala si pesa za walipa kodi watanzania ambao kubahatisha milo miwili kwa siku ni heavens kwao zinavyotafunwa. Honestly huyu baba ananichefua!!!!!!!!
 
Zile usd 35000 alizotoa Mapunjo ili wagawiwe wabunge Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara kawadhulumu na kawaahidi kuwapeleja Japan kukagua shughuli matokeo yake wabunge wamemgeukia waziri wake,wanangoja hiyo safari ya Japan ili waibue madudu zaidi
 
na ndio akome yeye kapewa mamlaka sasa kama mda wa kuisoma ripoti hana ndio atatia akili kwani ni uzembe
Nadhani alikuwa anafikiri kuwa bado kunakufanya kazi kwa umoja katika serikali (uwajibikaji wa pamoja).
 
Wana JF baada ya badiliko la mawaziri lililopelekea aliyekuwa waziri wa viwanda na Biashara ndg Cyril Chami kutemwa,imedhihirika ripoti zote za CAG hazimtaji moja kwa moja ila ni Ekelege(mkurugenzi mkuu TBS na katibu mkuu wake bi Joyce Mapunjo ambao wamekuwa wakila dili
"Kilichoniponza ni kutoipitia taarifa ya CAG na kutoa mapendekezo kama waziri,pia nilimuamini sana katibu mkuu ambaye yeye na wenzake walinigeuka na kuanza kuwa makuwadi wa kampuni feki za ukaguzi ambazo ni zao wenyewe tena hewa..
Nimegundua kosa langu la kumtetea Mkurugenzi wa TBS na kampuni zao.
Najua kama alivyosema rais na wao wataniafuata"
Mwisho wa kunukuu.
Hizi habari toka kwa Mtumishi wa ofisi yake ambae walikuwa nae jana usiku wakisikitika.

Viongozi wengi wanajisahau wanapenda kuletewa taarifa mezani badala ya kuhangaika huku na kule kutafuta ukweli wa mambo mwisho wa siku anaanza kutetea uovu maskini ya Mungu kumbe halijui atendalo hii imekula kwake alikula ya mbusi sasa ameota mapembe.
 
Wakubwa mimi mtazamo wangu naona kama Maawaziri wengi ni wahanga wa mfumo mbaya wa utawala ambao tunao Tanzania.Mamlaka karibu yote ya utawala yako kwa raisi wa nchi ambae amehodhi nguvu zote.Waziri na hata waziri mkuu hawana mamlaka yoyote ya kuwawajibisha Wakurugenzi wa mashirika,wizara,au makatibu wakuu,ambao ndio hasa madudu yanapofanyika.Kinachofanyika ni kwamba waziri/waziri mkuu anatoa ushauri tu kwamba fulani hafai utendaji wake.Mimi nafikiri lawama zote za wizi huu apelekewe mkuu mwenyewe maana yeye ndio aliowachagua hao wahuni wezi wa mali zetu na ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuwawajibisha.

Mimi siamini kama Ekelege na timu yake wamefanya madudu yote hayo kwa muda mrefu bila usalama wa magamba kumfikishia taarifa mkuu,isipokuwa tu aliona uzito kuwatoa maswahibu wake.

Tusiridhike na kubadilishiwa sura za mawaziri bali kinachotakiwa ni kupambana katika marekebisho ya katiba mpya kujenga mfumo mzuri wa uwajibikaji ambao nguvu ya utawala itatawanyika badala ya kubaki kwa mtu mmoja tu.
Tujenge mfumo ambao Waziri mkuu kama mtu anaesulubiwa kwa utendaji wa serikali bungeni apewe uwezo wa kuhire and fire watu wa timu yake.Hii itampa nguvu ya kweli ya usimamizi wa shughuli za serikali.
Na mawaziri nao wajengewe uwezo wa kuondoka na shingo za watendaji walio kwenye wizara zao.Isiwe mtu mwingine achague watu waajabu na wala hamuwezi kumuhoji kawateua kwa kigezo kipi halafu madudu yao wakifanya wanaowajibishwa mawaziri ambao pengine toka siku ya kwanza hawajaridhika na utendaji wao.
 
Wana JF baada ya badiliko la mawaziri lililopelekea aliyekuwa waziri wa viwanda na Biashara ndg Cyril Chami kutemwa,imedhihirika ripoti zote za CAG hazimtaji moja kwa moja ila ni Ekelege(mkurugenzi mkuu TBS na katibu mkuu wake bi Joyce Mapunjo ambao wamekuwa wakila dili
"Kilichoniponza ni kutoipitia taarifa ya CAG na kutoa mapendekezo kama waziri,pia nilimuamini sana katibu mkuu ambaye yeye na wenzake walinigeuka na kuanza kuwa makuwadi wa kampuni feki za ukaguzi ambazo ni zao wenyewe tena hewa..
Nimegundua kosa langu la kumtetea Mkurugenzi wa TBS na kampuni zao.
Najua kama alivyosema rais na wao wataniafuata"
Mwisho wa kunukuu.
Hizi habari toka kwa Mtumishi wa ofisi yake ambae walikuwa nae jana usiku wakisikitika.

katika wote waliofukuzwa wale ambao hawahusiki na madudu wizarani kwao ni huyu Chami, Nundu na Dr mponda hawa wametemwa kimajukumu zaidi.

waliotemwa kwa ubadhirifu dhahiri au kushindwa kazi ni hawa akina Mkulo, Maige, Ngeleja, na jizi lenyewe mfutakamba
 
aisee this kind of manung'uniko toka kwa phd holder, hainingii kichwani kwa kweli....au wakipewa haya madaraka reasoning za ki-daktari zinafutika? dah, jamaa anaongea kama std 7 leaver?
 
Back
Top Bottom