Ni kweli ni tetesi lakini naamini taarifa inayotolewa kwenye vyombo vya habari ambavyo vina wataalam zinakuwa na ukweli, hiyo nimeisoma kwenye gazeti la leoMkuu mbona kama habari yako ni TETESI tu, halafu habari yako haijabeba vizuri KICHWA CHA HABARI.
Badala ya kufungua makampuni ya kuwekeza hasa kwenye KILIMO na UFUGAJI, watu kila siku na madegree yao ni kufikiri kufungua vyama vya siasa tu -- KUNA BIASHARA GANI HUKO????
Ni kweli ni tetesi lakini naamini taarifa inayotolewa kwenye vyombo vya habari ambavyo vina wataalam zinakuwa na ukweli, hiyo nimeisoma kwenye gazeti la leo
ugonjwa wetu mkubwa watanzania ni uvivu wa kusoma tunapenda kusoma neno moja tukijitahidi sana mstari mmojaullichokiandika hakiendani kabisa na kichwa cha habari. inaonekana wazi kabisa kwamba umevurugwa.
ugonjwa wetu mkubwa watanzania ni uvivu wa kusoma tunapenda kusoma neno moja tukijitahidi sana mstari mmoja
basi niseme ni ugojwa wako wewe , mbona heading na contents vinaendana, na wenzako wameelewa kilicho andikwa au ndo zile shule zetu za Kata ?huo ni ugonjwa wako usiwatupie watu wengine. halafu ww sio msemaji wa watanzania
Mh. Dr. Slaa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwa Iringa amesema wamebariki madiwani 2 walioomba kujiuzulu Shinyanga, hiyo ndiyo Demokrasia ya kweli, madiwani hao moja ya sababu kubwa ya kujiuzulu ni kwamba wanamuunga mkono Mh. Zitto , Mh. Dr. Slaa amesema kuna taarifa pia kuwa chama cha ACT kiko mbioni kusajiliwa na baadhi ya wale waliovuliwa uanachama CHADEMA.
Kama ni kweli chama hicho kitasajiliwa na viongozi wake ni miongoni mwa waliovuliwa uanachama CHADEMA, basi Dr. Kitila Mkumbo atakuwa ni mtu wa kuogopwa kama UGONJWA WA KUFISHA, ataogopwa na kizazi kilichoshuhudia usaliti wake na kizazi kitakacho kuja kuzaliwa na kusimuliwa kisa hiki.
Kama watafanya kosa hilo la kusajili chama hicho , natabiri wakiweza kupata wanachama hata elfu kumi kwa nchi nzima basi ntajua watanzania wengi hatunazo akili. Dr. Kitila amekuwa akinukuliwa na magazeti baada ya usaliti wake kukwama na kuvuliwa uanachama akisema tunahitaji chama mbadala cha upizani zaidi ya CHADEMA kumbe malengo yake yalikuwa ni hayo. Huyu mtu ni msomi mzuri lakini nashawishika kusema siasa sio mahali pake alikosea njia, na kama ni mahali pake basi anauchu mbaya sana na tamaa ya madaraka.
Tunahitaji kuikomboa Tanzania kwa kuiondoa CCM madarakani
Zitto kaponza vijana wengi sana huku yeye akiendelea kupeta kaua ndoto za vijana kisiasa
basi niseme ni ugojwa wako wewe , mbona heading na contents vinaendana, na wenzako wameelewa kilicho andikwa au ndo zile shule zetu za Kata ?
ni kweli hicho chama kipo na bwana kabwe ndio muasisi wake, kinaitwa Alliance for Change and Transparence. nimeiona kadi yao ya uanachama in rangi ya zambarao kama jezi za mbeya city. juzi juzi tu hapa kigoma uliwaka moto baada ya wafuasi wa chama hicho kutaka kupandisha bendera yao kwenye tawi la chadema la urusi (kwa wanaoijua kigoma watakuwa wanakijua kijiwe cha chadema cha urusi) ndipo wanaharakati wa chadema walipozuia upuuzi huo mpaka polisi waliingilia kati