Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

...and Tendwa, still insists......CCJ is HOAX!

We hizo terminology za kwa akina Mama Lwakatare na misukule nawe wazileta huku??

Tehe teheeee.... mambo vipi? Mbona ile issue unataka kuniacha kitonga?
 
jamani hivi tutegemee nini kutoka katika hiki chama, kama kiongozi anaulizwa unafanya shughuli gani anasema yeye ni mjasilia mali lakini awezi kusema anafanya nini, sasa kama anauza bangi je? chama kilikuwa kinasound good lakini stratergies zake za kuingia kwenye jamii zinatia shaka kidogo
 
Kuanzia nimeanza kusikia habari za kuwepo kwa Chama Cha Jamii (CCJ) sijasikia hata jina la mmoja wa wanachama wanaounda chama hicho.
Taarifa zilizopo zinasema tu kuwa CCJ ni ya vigogo waliokuwa ndani ya CCM bila kuwataja majina.
Kwanini wapashaji wa habari wanaogopa kuwataja majina?
Je chama hicho kinaundwa na kina nani?
Nijulisheni mie kalagabaho nipate kujua.
 
Hoax sii Hoax kuna kitu kinaendelea na itajukuja julikana tu. Kifupi viti vyenu mkae na wenye kuchukua popcorn tubebe kabisa tukae mkao wa sinema...
 
We hizo terminology za kwa akina Mama Lwakatare na misukule nawe wazileta huku??
Tendwa naye alikuja na hiyo term jana, akikanusha uwepo wa CCJ! sasa nashindwa kushangaa kama anayajua hayo yaliyowekwa hapo juu......!

Tehe teheeee.... mambo vipi? Mbona ile issue unataka kuniacha kitonga?
Poa mzee......Dar takupa update.....bt hujaachwa Kitonga mzee.....!
 
Jamani naiomba CV ya hawa akina Kiyabo na huyo mwenzie Muhabi. Hawa background zao ni nini? Kwa nini wanapewa hadhi inayofanana na CCM wakati wao ni sisimizi tu?
Binadamu wote ni sawa na wana haki sawa ...... Hao wenye hadhi nao walianzia kwenye usisimizi tu!
 
Wadau wa JF naomba mwenye data za kweli atusaidie watu walioko nyuma ya CCJ maana kila muhusika mshukiwa anayeulizwa aidha anakataa au anapatwa kigugumizi kujibu. Natanguliza shukrani.
 
kama kweli wana nia na tuwasome katika sura zao kwamba wana nia dhamira ya kweli na nchi hii, wanaweza kufanikiwa, kwa sababu watanzania ni rahisi sana kuwahamizha kimawazo, lakini kama ni kinyume chake basi wajiunge na upinzani!!
 
Kisije kikawa ni Chama cha Mafisadi, No. 2, in disguise!

Mafisadi kamwe hawawezi kuwa na falsafa hiyo ya kuwaletea watanzania wote kama sio walio wengi maendeleo,mafisadi na wa binafsi na wanaopenda kujilimbikizia mali wenyewe.Wnajiangalia wao wenyewe na familia zao.

Hawana imani ya kuwa nchi inaweza kuendelezwa na wote wanaimani kuwa matajiri wachache ndio watakaoleta maendeleo katika nchi hii.

Mtazamo wa CCJ ni tofauti kabisa na mafisadi nashawishika kuwa CCJ ni zao la wapingaufisadi na inatubidi tuwaunge mkono kwa hili walilolianzisha kama tunataka uhuru wa kweli Tanzania.
 
Tunasubiri CCK- Chama Cha Kifisadi???????????kije maana ndio wakati huu.
 
Gazeti la Raia Mwema toleo la leo lina habari ifuatayo
Habari zinaeleza kwamba CCJ imeitikisa CCM, pamoja na kauli za kujifariji zinazotolewa kupooza makali ya chama hicho ambacho hata usajili hakijapata, kikineemeka kwa gharama za hofu ya ndani ya CCM.

Uchunguzi wa Raia Mwema umethibitisha kwamba vyombo vya dola vimekuwa katika harakati za kuwafuatilia watu wote wanaohusishwa na CCJ hata kwa kutajwa tu, wakiwamo wabunge na hata viongozi wastaafu na wa sasa serikalini.
Kaazi kweli kweli, kuna watu hawalali ati !! Halafu twadai tuna demokrasia !

Masikini Tendwa, halafu anadai anatimiza wajibu wake kwa uhuru na bila kuingiliwa !

Wakati vyombo vya usalama vikiwa katika harakati hizo, baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM, akiwamo Katibu Mkuu wake, Yussuf Makamba, wameendelea kutoa kauli za kupuuza kuanzishwa kwa chama hicho na kuhusishwa kwake na vigogo mashuhuri wa CCM.


Eti CCJ ni hoax !! Believe this and you will believe anything ! Njaa mbaya sana !
​
 
Wadau wa JF naomba mwenye data za kweli atusaidie watu walioko nyuma ya CCJ maana kila muhusika mshukiwa anayeulizwa aidha anakataa au anapatwa kigugumizi kujibu. Natanguliza shukrani.


watu wa happiness katabazi utawajua tu huwa hawajui kufichama
 
Kwa nini chama hiki kinaonekana kujificha ficha katika mambo yake? ni kweli chama hicho kipo au kinafikiriwa/ kutegemea kuanzishwa miaka ijayo? Ubabaishaji wakati wa kuanzishwa chama ni dalili mbovu wanakotarajia kuelekea.
 
Wakuu CCJ wamenza kuwekewa kiwingu.

Hivi haiwezekani hiyo CCJ kuwaomba wanachama wake toka hiyo mikoa 8 ya Bara na Miwili huko Visiwani kwenda Ofisini kwa Mrajisi ili aweze kuwa hakiki?

Mfano wa Dar labda Jumatatu, Moro - Jumanne, Dodoma - J'tano, Aruisha - Alhamisi, Kilimanjaro - Ijuma, Tanga - Jumatatu inayo fuatia, Iringa - Jumanne nk nk , wamuulize tu waje na vitambulisho gani na barua gani za nyumba kumi kumi?

Au CCJ wamkopeshe mrajisi hela za usafiri za hao makarani wake wakafanye uhakiki.
 
Wakuu CCJ wamenza kuwekewa kiwingu.

Hivi haiwezekani hiyo CCJ kuwaomba wanachama wake toka hiyo mikoa 8 ya Bara na Miwili huko Visiwani kwenda Ofisini kwa Mrajisi ili aweze kuwa hakiki?

Mfano wa Dar labda Jumatatu, Moro - Jumanne, Dodoma - J'tano, Aruisha - Alhamisi, Kilimanjaro - Ijuma, Tanga - Jumatatu inayo fuatia, Iringa - Jumanne nk nk , wamuulize tu waje na vitambulisho gani na barua gani za nyumba kumi kumi?

Au CCJ wamkopeshe mrajisi hela za usafiri za hao makarani wake wakafanye uhakiki.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…