Chama cha Walimu kinasimamia maslahi ya walimu?

kilindi yetu

Member
Dec 4, 2015
7
1
Walimu jitambueni na hiki chama chenu cha walimu Tanzania.jiulizeni kimewanufaisha nini?

Na je wale walio staafu umewaona wamefaidika nini na uanachama wao?

Michango ya uanachama kila mwezi inakwenda wapi? Na je unataarifa gani juu ya miradi ya chama chako hiki?

Je chama hiki kimewai kaguliwa mara ngapi, pia ujiulize uanachama huo ni wahiyari au walazima?

Ukijiuliza maswali hayo utapata jibu kuwa CWT ni jipu uchungu na dhuluma ya dhahiri kwa walimu akyeee.

JITAMBUE EWE MWALIMU
 
Walimu sijui nani katuroga jamani majengo kila mkoa yamejengwa benki zimeanzishwa bado mwalimu anakatwa asilimia 3% sijui ya nini jamani walimu inatosha tuamke.chama kwa sasa kinahela nyingi inayonufaisha wachache.
 
Ningekua na uwezo ningetumbua gujipu hugu haraka. Lkn amini ninawaambia ninyi wababe wachache mnaoendelea kuwakandamiza walimu wa nchi hii pamoja na mishahara duni yao, ipo siku mtatumbuliwa tu. Chama gani hakina kuopt out au in? Uanachama gani wa kulazimishana? Babangu tangu aanze ualimu mbona Cwt hamjawahi msaidia chochote? Hata kudai nyongeza ya mshahara serikali imewatia kwapani??? Shame on you
 
Lkn niwakumbushe tu walimu kwamba, pamoja na kuandika kwa hasira hivi msipofanya kama walivyofanya wapigania uhuru wa kuungana na kuunda umoja wa kupingana na yanayoendelea, the you will cry forever.
 
Hakuna mtu yeyote au chombo chochote chenye mamlaka ya kukata na kuchukua sehemu ya mshahara wa mtu bila idhini yake.
Mimi baada ya kugundua huu ni wizi nilimuandikia mkurugenzi kumjulisha kuwa SEHEMU YA mshahara wangu unaelekezwa CWT bila idhini yangu na huu ni kama wizi.Nikawaomba CWT makubaliano tuliyoyafanya baada ya kuitwa kwa mkurugenzi,wakadai hawana.
Nikafatilia ndani ya miezi kama mitano ndo mshahara ukaachwa kukatwa.
Wanao ruhusu huu wizi ni halimashauri zetu,kuruhusu mshahara wa mtu kukatwa bila ridhaa ya mtumishi.
CWT hapa Arusha sitaki hata kuwasikia.
Kama chama kimeshindwa kujiendesha,basi viongozi watumie mishahara yao.
 
Ningekua na uwezo ningetumbua gujipu hugu haraka. Lkn amini ninawaambia ninyi wababe wachache mnaoendelea kuwakandamiza walimu wa nchi hii pamoja na mishahara duni yao, ipo siku mtatumbuliwa tu. Chama gani hakina kuopt out au in? Uanachama gani wa kulazimishana? Babangu tangu aanze ualimu mbona Cwt hamjawahi msaidia chochote? Hata kudai nyongeza ya mshahara serikali imewatia kwapani??? Shame on you
Huo mjipu ni wa kutumbua kwa kutumia sululu... yani hicho chma kinachefua sana.. mfxxxxxx!
 
WANAFIKI Wakubwa Mbona Miaka Yote Mmekubali Kuwa Chini Uongozi Wa CWT!! Kwa Vile Viongozi Wakuu Wa CWT Juzi Walionekana Kumpinga DC Makonda Na Mpango Wake, Leo Ndio Mnajitoa Ufahamu Humu Na Kuanza Kulialia Kuhusu CWT!! Ndio Mnatumika Tu Kama Big G Tu!!! Kama Kweli Ninyi Wanachama Wa CWT Na Hamlidhiki Au Hamlidhishwi Na Utendaji Wa Chama Chenu, Why Msiweke Nguvu Kwa Umoja Wenu, Aidha Kuukataa Uongozi Au Mkabadili Katiba Ya Chama Chenu!!?? Ama Kwenda Mahakamani, Kupinga Kila Mwalimu, Ni Lazima Awe Mwanachama Wa CWT, Na Kukatwa Sehemu Ya Mshahara Wake, Kuchangia Uendeshaji Wake!! Ili Iwe Kila Mwalimu Ana Haki Ya Kujiunga Na Chama Chochote Chenye Malengo Ya Kumuendeleza Kitaaluma, Kiuchumi N.k.Na Awe Huru Kujiunga Na Chama Au Taasisi Aipendayo!! Lkn Kuibuka Tu Mara Baada Ya Viongozi Wa CWT Kupinga Jambo Au Tamko Fulani!! Huko Ni Kutumika Tu, Na Sidhani Kama Ninyi Ni Waalimu!!! Kama Kweli Ni Waalimu, Hivi Hamna Mikutano Yenu Ya Kuzungumzia Masuala Yenu!!!?? Badala Ya Kupayuka Mitandaoni!!??
 
yaani hao jamaa ni wapigaji sana..walimu wamejengwa kuwa waoga japo ndo wakombozi wa nchi hii...na walimu wengi ni kutoka familia duni na watu wengi kutoka kwa familia duni ndio wanafanya kazi hizi wanazoziiita "community works" na ndo maana hata mishahara yao ni midogo kama polisi, jeshi, manesi, walimu n.k hivyo mishahara ni midogo na kujikomboa ni vigumu na watu hao wataendelea kuwa masikini hadi mwisho,,,na tambua masikini hana sauti
hao CWT wanakula hela za hao walimu na mwisho wa siku ndo pesa za walimu zinatumika kwenye uchaguzi(GENERAL ELECTION) na kisha viongozi wanaofanikisha wanapewa ukuu wa wilaya na vyeo vingine vya juu kwa kufanikisha wizi wa pesa za walimu
kweli inauma sana
 
inaonesha hujui chochote kuhusu vyama vya wafanyakazi , cwt sio mfuko wa hifadhi wala saccos, changia kijana ukitaka kuzifaidi na wewe unaomba ukatibu wa wilaya au mkoa unakunywa maji baridi
 
tatizo ni moja. mnalalamika kila siku lakini hamchukui hatua. " a barking dog seldom bite" . sasa mmezoeleka kuwa ni "barking dogs". mtafute hata huyo anaelalamika muulize amewahi hata kuiona katiba ya cwt?Anajua mwanachama ni nani? na nani si mwanachama?kujiunga je ni lazima?......
mngeisoma na kuielewa basi wala CWT isingewasumbua.Hakuna mahala wamesema uanachama ni lazima.HAKUNA
Policy Documents
 
Hakuna mtu yeyote au chombo chochote chenye mamlaka ya kukata na kuchukua sehemu ya mshahara wa mtu bila idhini yake.
Mimi baada ya kugundua huu ni wizi nilimuandikia mkurugenzi kumjulisha kuwa SEHEMU YA mshahara wangu unaelekezwa CWT bila idhini yangu na huu ni kama wizi.Nikawaomba CWT makubaliano tuliyoyafanya baada ya kuitwa kwa mkurugenzi,wakadai hawana.
Nikafatilia ndani ya miezi kama mitano ndo mshahara ukaachwa kukatwa.
Wanao ruhusu huu wizi ni halimashauri zetu,kuruhusu mshahara wa mtu kukatwa bila ridhaa ya mtumishi.
CWT hapa Arusha sitaki hata kuwasikia.
Kama chama kimeshindwa kujiendesha,basi viongozi watumie mishahara yao.
Nimependa Post yako. Na mshahara unaotoka hazina unakatwa na nani na je ukitaka kuzuia makato TTA kwa sasa ambayo mshahara unaotoka wizarani unafanyaje? Mbona kama kuwa TTA siyo optional?
 
Walimu sijui nani katuroga jamani majengo kila mkoa yamejengwa benki zimeanzishwa bado mwalimu anakatwa asilimia 3% sijui ya nini jamani walimu inatosha tuamke.chama kwa sasa kinahela nyingi inayonufaisha wachache.
Wana hela hadi wanakopesha vyama vya siasa.
 
Walimu jitambueni na hiki chama chenu cha walimu Tanzania.jiulizeni kimewanufaisha nini?. na je wale walio staafu umewaona wamefaidika nini na uanachama wao?.michango ya uanachama kila mwezi inakwenda wapi? na je unataarifa gani juu ya miradi ya chama chako hiki?..je chama hiki kimewai kaguliwa mara ngapi?.pia ujiulize uanachama huo ni wahiyari au walazima?????. ukijiuliza maswali hayo utapata jibu kuwa cwt ni jipu uchungu na dhuluma ya dhahiri kwa walimuuu akyeeeeeeeeeeeeeeeee.....JITAMBUE EWE MWALIMU
Hivi ni lazima kujiunga ni chama cha walimu CWT au ni hiari maana naona kila mwalimu huwa analalamika juu ya uendeshwaji wa hiki chama
 
Wanalazimisha kujiunga ukikataa wanakukata kilazima kwenye mshahara wako bila idhini yako.
 
Wanalazimisha kujiunga ukikataa wanakukata kilazima kwenye mshahara wako bila idhini yako.
wakishakukata bila ridhaa yako,wewe unachukua hatua gani?au unaishia kulalamika?mshahara wako ni jasho lako na hakuna mahala katika mkataba wako na mkurugenzi wako kuwa mshahara utakatwa kupewa mtu mwingine bila wewe mwenyewe kutoa taarifa au idhini. sasa kosa mnalofanya walimu ni hili,mkishakatwa mnanyoosha miguu.inabaki kulalamika tu. Ila ukiwasha moto kwa mwajiri wako basi dakika sifuri tu hiyo hela haitakatwa tena.
 
Back
Top Bottom