Chama Cha Waigizaji: Huu ni wizi mtupu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama Cha Waigizaji: Huu ni wizi mtupu...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BABA JUICE, Nov 21, 2011.

 1. BABA JUICE

  BABA JUICE JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chama cha waigizaji Tanzania kimeandaa utaratibu mpya kwa waigizaji wote nchini. Chama hicho kimeandaa utaratibu kwa kila muigizaji kuwa na kitambulisho cha uigizaji ambacho kinatambulisha kazi yake.

  Akizungumzia utaratibu huo mwenyekiti wa taifa chama cha waigizaji Tanzania, Mike Sangu alisema utaratibu huo utaanza mwezi huu. Kila muigizaji atalazimika kutoa shilingi elfu kumi na mbili kwa ajili ya

  kupata kitambulisho hicho Kufikia januari program hii itakuwa tayari kwa kila muigizaji Tanzania na waigizaji wote watavitumia vitambulisho hivyo. Mwigizaji yeyote ambaye hatakuwa na kitambulisho hadi kufikia februari atachukuliwa hatua za kisheria. Utaratibu huo utarahisisha kazi ya muigizaji kutokana na kupata usumbufu wakati wa kuigiza, na pia itasaidia muigizaji kujullikana zaidi.
  UTARATIBU MPYA KWA WAIGIZAJI…!! | DarTalk.com

  MAONI YANGU: Uigizaji ni kama mziki na ni kipaji cha mtu kinachowatofautisha watu,mi naona vitambulisho ni janja ya nyani kufaidisha wachache na kuzui wenye vipaji wasionekane! ingekuwa vizuri huyu jamaa angesisitiza waigizaji wapitie kwenye vyuo vya kuigiza ili wasionekane wanaigiza wakiwa wanaigiza! kwa tanzania tunawatu wachache sana wanaojua kuigiza wengi wao wanapiga makele tu!
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  'wasionekane wanaigiza wakiwa wanaigiza'. Imekaa vizuri. Bongo ujasiriamali ndugu, sema tu ada imekuwa kubwa ila wazo ni zuri.
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ni namna ya kutambuana, sawa tu! hakuna wizi.wajitahidi quality ya vitambulisho iendane na gharama ya fedha
   
 4. BABA JUICE

  BABA JUICE JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naamini kila wazo ni zuri tuangalie kwa upande mwingine wa shilingi ni sawa na kusema kila mwanamziki awe na kitambulisho!unajua muziki au uigizaji sio kazi hadi pale itakapokupatia kipato!kuna vipaji vingi vya watu wanojua kuigiza na kuimba lakini sema hawana good connection au pesa ya kurekodi..wenye connection hawajui kuigiza na wenye pesa hawajui kuimba hii ipo wazi! kwa nchi ambazo zimeendelea wanaangalia umeenda chuo kipi au umeigaza movies ngapi!hapa inaweza kuwa kisiasa kama umeigiza filamu ambayo inaenda kinyume na baadhi ya watu serikalini visa vinaanza........ushauri wangu hiki chama kingekazia ubora wa filamu zetu na hawa waigizaji wetu.mimi naamini muziki na uigizaji unaweza kujifunza pindi pale unapopenda kwa moyo wako hata kama hupati milions but unaenjoy what you do..ukishatanguliza wazo la pesa kwenye kazi yoyote bila kujali unachozalisha mwisho wa siku kitatoka kibovu tu...kama tunavyoona kila siku
   
 5. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hili wazo halina mantiki yoyote mbali na 'ujasiriamali' kama alivyosema mwenzetu mmoja hapo juu. Tujiulize kwanza huo utambulisho,ili iweje.Je, kuwa na kitambulisho kilichoandikwa 'mwigizaji' ndio kigezo cha kuwa mwigizaji mzuri? Wanatumia vigezo gani hadi kuridhika kwamba mtu huyu ni mwigizaji? Je, hivyo vigezo haitoshi kumtambulisha mtu, ni mpaka awe na kijikadi cha thamani ya tsh 12,000/=? Na je hivyo vitambulisho ni kwa undergrounds au waigizaji wote?

  Kwamba Kanumba, Ray, Johari, Richie nk. hatuwatambui ni mpaka wawe na vitambulisho? Mbona kituko hiki. Waigizaji wengi tunawafahamu kwa nick names, je kwenye vitambulisho watatumia majina gani?

  Naamini waigizaji wazuri wanatambulika tu kwa uwezo wao, si mpaka mtu awe na kikadi mfukoni kuilichoandikwa Kigosi wakati mashabiki wake tunamfahamu Ray. Waigizaji tunawatambua na kuwaheshimu kwa kazi nzuri wanayofanya jukwaani sio kwa kuwa na vitambulisho mifukoni. Lakini pia waigizaji wengine ni wanafunzi ktk shule na vyuo mbalimbali na wengine ni waajiriwa katika secta rasmi kama vile makampuni wote hao wana vitambulisho, je hivyo havitoshi kuwatambulisha huko waendako? Na je, huwa wanapata shida gani ambayo hasa ianatokana na kutokuwa na vitambulisho?

  Maswali ni mengi sana ambayo nanahitaji majibu ya kina kabla ya kukusanya hela kutoka kwa waigizaji hawa. Swali la mwisho, ni nani hasa anayepata usumbufu kutokana na kukosa kitambulisho, kwa maana kwamba je hoja hii imetoka kwa waigizaji wenyewe au imetoka kwa huyo kiongozi wao?
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hakuna ubaya. Uigizaji ni kazi kama kazi zingine. Kwani wewe huna kitambulisho cha kazi? Ila kwanini iwe waigizaji tu na sio wasanii wote? Au wasanii wengine wanavyo?(inawezekana nilipitwa na habari).
  OFF TOPIC: kwanini kila jambo linalohusisha pesa akili zetu huwaza kuzulumiwa? Najaribu kufikiria hivyo vitambulisho vingekuwa vinatolewa bure mtoa mada ungejenga hoja gani?
   
 7. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kimsingi hakuna anayepinga kuwa waigizaji sio wafanya kazi, la hasha. Tatizo linaloonekana hapa ni hizo sababu zilizotolewa. Kwamba ni kutokana na kupata usumbufu wakati wa kuigiza na kusaidia msanii kufahamika zaidi.

  Hoja hapa ni, wanapata usumbufu gani wakiwa kuigiza ambao suluhu pekee ni kuwa na vitambulisho vya Tsh 12000/=? Inawezekana pengine wanapokuwa site, lakini je ina maana hawatoi taarifa mapema kwa wahusika wa site hiyo wanayokuwa wanatembelea? Kwa hiyo wanatuaminisha kwamba ukiwa na kitambulisho, inakuwa ndio mbadala wa taratibu nyingine zote?

  Kama ni issue ya msanii kufahamika, sijui anafahamika kwa nani labda. Kama ni wa mashabiki, sioni kama kitambulisho ni hoja ya msingi kwa sababu mashabiki hawna haja yakujua kama mwigizaji ana kitambulisho mfukoni au la. Mashabiki wanahitaji burudani, so sioni nafasi ya kikadi hiki ktk burudani.

  Muandaaji wa filum fulani mara nyingi ndiye anayechagua waigizaji wanaomfaa ktk filum hiyo. Kwa Tanzania hatuna utaratibu wa waigizaji kutuma maombi kwa ajili ya kushiriki ktk kazi(filum) fulani. Maamuzi yote anayo mwandaaji mwenyewe, yeye ndiye anayamua nani amtumie na nani amuache. Kimsingi mwandaaji anakuwa anawafahamu waigizaji anaowahitaji, sasa sidhani kama kitambulisho pekee ndicho kinachomwezesha mwandaaji ktk kufanya uchaguzi wake.

  Zipo kampuni mbalimbali zinazoshughulika na mambo ya filum, zinakuwa na usajili unaotambulika kisheria(sina hakika hapa ketu zipo ngapi). Waigizaji wanaweza kuajiriwa kwa mkataba ktk kampuni hizi. Sasa hapa ndipo linakuja swala la vitambulisho. Kila kampuni itatoa vitambulisho kwa wafanyakazi wake(tena bure). Lakini kwa huu utaratibu wetu wa waigizaji wanaojitegemea, sijashawishika kwa kweli. Vinginevyo tuseme hata wafanyabiashara wawe na vitambulisho maalum kwa kazi yao, hata wale dada zetu wa pale Ohio nao wawe navyo! Hapana, huyu bwana aje na hoja ya msingi kabla hatujachukuwa hiyo hela yetu.

  Issue ya hela ni very sensitive, watu hawalalamiki bure. Fikiria Visa au Master Card pale Barclays Bank unalipia Tsh ngapi halafu ulinganishe na gharama hiyo iliyotajwa hapo kisha ndio useme wanalalamika bure. Think of value for money dear.
   
 8. v

  valid statement JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  MJINI SHULE.... Njoo usomeshwe.
   
 9. C

  Claxane Senior Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kakojoe ulale bangi za chooni mwaki na ufisadi group
   
 10. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na mimi yangu nitaileta kwa kila muigizaji lazima apitie chuo cha sanaa-bagamoyo
   
 11. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Upupu tu!
   
 12. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kama sijakosea, kitambulisho cha kazi hutolewa bure na mwajiri na ukiacha kazi kinakuwa cha mwajiri. Je, kwa maelezo yako hapo juuu watakuwa wameajiriwa na nan:biggrin:i?
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  umesoma nakuelewa kilicho andikwa au ndio nyie mnao jaji kwa title enhee...
   
 14. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wasanii wa bongo ni wasanii na wala si waigizaji!
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,053
  Likes Received: 7,259
  Trophy Points: 280
  Hivyo ni vyama,
  Na kua mwanachama ni hiyari, si lazima.
  Lyatonga Mrema anaongoza Tanzania Labor Party (Chama Cha Wanyakazi), je kila mfanyakazi ni member wa TLP?
   
 16. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Itabidi kitambulisho namba moja wakampe JK, kitamsaidia sana kwenye dili zake za kupiga picha na waigizaji wa Hollywood...!
   
 17. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hujakosea mkuu.
  Una haki ya kujibiwa hili swali lako.
   
 18. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Duh!
  Hii nayo kali kwelikweli.
   
 19. BABA JUICE

  BABA JUICE JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kitu nachoofia kuhusu hili ni urasimu uliojaa miongoni mwa watanzania hasa walio na madaraka
   
 20. d

  doctorwasummary Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumekucha Tanzania! Kila mtu atadai kitambulisho chake.....wenye vipaji vya kula msosi nao wako mbioni kuwa na vitambulisho vyao! Hapo ndipo ufisadi, uchakachuaji, ukameruni na mengineyo mengi yanapoanzia...

  Wabongo tuko juu katika kubuni mambo ya kifisadi huku tukiacha mambo muhimu yakienda kombo! Huyo jammaa atwambie, je, mwigizaji asiye na kitambulisho (tusema chipukizi) hataweza kuigiza au kutambuliwa tu eti kwa sababu hana kitambulisho?

  Kitambulisho kitakuwa na jina gani kwani waigizaji wengi wanajulikana kwa a.k.a zao na wakati mwingine a.k.a zao huwa zinabadilika...Kweli dunia mti mkavu na mbichi...Msishangae kuona mtu mmoja ana vitambulisho mia mfukoni!

  Kila la heri wafanyabiashara mnaojiita wajasiriamali kwa kupotosha maana ya ujasiriamali....kwenu kila mfanyabiashara ni mjasiriamali!
   
Loading...