Chama cha Mapinduzi: Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chama cha Mapinduzi: Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,629
Reaction score
6,812
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Siku za hivi karibuni kumeibuka baadhi ya watu ambao wamekuwa kwa makusudi na kwa malengo maalum wakitunga na kujiandikia taarifa, za uongo, kujenga hofu na au kupotosha na kisha kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa malengo mahsusi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi.

Watu hao katika nyakati tofauti wamekuwa wakitengeneza uzushi na uongo huo na kuusambaza kwenye mitandao pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kwa lengo lisilo wazi.

Baadhi ya uzushi na uongo uliotungwa na kusambazwa na watu au kikundi hicho ni pamoja na hii ya leo inayoeleza mambo mbalimbali juu ya Ndugu Edward Lowasa na ambayo watunzi wake wameandika kuwa imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.

Ifahamike kuwa uzushi huo na mwingine uliofanywa na watu au kikundi hicho umekusudia kujenga msukumo ambao haupo ili kuujengea umma hofu ya huruma dhidi yao ili kusukuma na kushinikiza agenda zao.

Jambo hilo ni uzushi mtupu kwa sababu kwanza Ndugu Nape na wajumbe wote wa Sekretarieti hawapo jijini Dar es Salaam badala yake wapo mikoani kushiriki katika zoezi la kura ya maoni kwa ajili ya uteuzi wa wagombea Udiwani na Ubunge zoezi ambalo litakamilika Agosti Mosi, 2015.

CCM inasisitiza kuwa habari hizo si za kweli, zimeandikwa na watu kwa malengo binafsi ya kugombanisha, kujenga chuki na uhasama baina ya Ndugu Nape, Chama, Wajumbe wa Sekretarieti na wananchi kwa ujumla bila sababu.

Viongozi, wana-CCM na wananchi kwa ujumla hawana budi kupuuza uzushi wowote ule unaotolewa na kusambazwa na watu au vikundi vya hovyo vinavyotumiwa na watu kwa maslahi binafsi, badala yake CCM itakuwa inatoa taarifa sahihi kwa wakati ili kutoruhusu uwepo au kuibuka kwa ombwe la mawasiliano baina ya umma na Chama.

Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano na Umma
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM
Lumumba, Dar es Salaam.
29/07/2015

 
Kwa ccm hakuna tofauti kati ya uzushi na ukweli!.
 
Ile sheria ya makosa ya mtandao iko wapi? Mbona haifanyi kazi au imewashinda utekelezaji? Mliikimbiza bungeni ikiwa ya moto tena kwa dharura sasa mbona kimya tu. Kama ni uzushi kamata tia ndani. Kuja kulalamika hapa haitasaidia cho chote!
 
Hata Ndugai Kuua ni Uzushi? Nchemba kugawa Rushwa za Escrow kama Njugu ni Uzushi?
 
Mwenye akili na akimbie haraka huko CCM ... Mafuriko yatazoa hadi makalio yao ....
 
kimbunga kimbunga kinafunua nyeti za kuku,Lumumba mapanya buku yanakimbilia porini
 
Kama mpuuzi mmoja aliyesema kuwa CCM yamsajili Messi wa CHADEMA wakati kwa kiwango alichonacho Messi wa CHADEMA,CCM hawana mahali pa kumuweka kwa kuwa CCM ni kama kakichuguu mbele ya Messi wa CHADEMA.
 
Haya mambo ni ya kwenu hukohuko ndani, kama kamati ya maadili ilifanya kinyume, je tutakuaminije wewe?
 
Back
Top Bottom