Chama cha Mapinduzi: Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chama cha Mapinduzi: Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ha ha ha ha hebu leteni tena yale matokeo ya NECTA ya Nnape... Singapole ndio nchi gani?
 
mmetoa tuhuma leo na leoleo mnakanusha,kwani ccm mmejipangaje?ndooorooooobo.acheni kumbwela
 
Tatizo chama kinaendeshwa kama kampuni ya wakandarasi wa Kibongo...wengi tutaamini hata kama ni Uvumi!!
 
Hilo sawa, vipi kuhusu suala la Mhe.Ndugai kumpiga mtu mpaka kuzimia kama atakuwa hajafa mpaka sasa? Mhe.Wassira nae kamtwanga mtu juzi juzi tu hapo.Vipi kamati ya maadili haitawajadili?
 
Lini CCM ikaripoti mambo ya Serikali eti Uchunguzi unaendelea?

Rudi Nsumba Sec ukareseat paper lako la Form 4
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Siku za hivi karibuni kumeibuka baadhi ya watu ambao wamekuwa kwa makusudi na kwa malengo maalum wakitunga na kujiandikia taarifa, za uongo, kujenga hofu na au kupotosha na kisha kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa malengo mahsusi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi.

Watu hao katika nyakati tofauti wamekuwa wakitengeneza uzushi na uongo huo na kuusambaza kwenye mitandao pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kwa lengo lisilo wazi.

Baadhi ya uzushi na uongo uliotungwa na kusambazwa na watu au kikundi hicho ni pamoja na hii ya leo inayoeleza mambo mbalimbali juu ya Ndugu Edward Lowasa na ambayo watunzi wake wameandika kuwa imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.

Ifahamike kuwa uzushi huo na mwingine uliofanywa na watu au kikundi hicho umekusudia kujenga msukumo ambao haupo ili kuujengea umma hofu ya huruma dhidi yao ili kusukuma na kushinikiza agenda zao.

Jambo hilo ni uzushi mtupu kwa sababu kwanza Ndugu Nape na wajumbe wote wa Sekretarieti hawapo jijini Dar es Salaam badala yake wapo mikoani kushiriki katika zoezi la kura ya maoni kwa ajili ya uteuzi wa wagombea Udiwani na Ubunge zoezi ambalo litakamilika Agosti Mosi, 2015.

CCM inasisitiza kuwa habari hizo si za kweli, zimeandikwa na watu kwa malengo binafsi ya kugombanisha, kujenga chuki na uhasama baina ya Ndugu Nape, Chama, Wajumbe wa Sekretarieti na wananchi kwa ujumla bila sababu.

Viongozi, wana-CCM na wananchi kwa ujumla hawana budi kupuuza uzushi wowote ule unaotolewa na kusambazwa na watu au vikundi vya hovyo vinavyotumiwa na watu kwa maslahi binafsi, badala yake CCM itakuwa inatoa taarifa sahihi kwa wakati ili kutoruhusu uwepo au kuibuka kwa ombwe la mawasiliano baina ya umma na Chama.

Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano na Umma
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM
Lumumba, Dar es Salaam.
29/07/2015


Kwamba taarifa ile nyingine Nape hayupo na hivyo haiwezekani kuwa aliyeitoa ni Nape,lakini hii ya sasa ni kuwa Nape hayupo na bado wameweza kuitoa,DUH!
 
Ww Informer issue ya Job Ndugai , Naibu Speaker wa Bunge mbona kimya au sio taarifa ya mhimu?
 
Last edited by a moderator:
CCM wanapingana wao kwa wao...yaani ni hatari... hadi washaanza kutoana ngeu na mangumi wao kwa wao...

Kwani Nape akiwa mikoani hawezi andika kwa smartphone yake na kurusha mtandaoni...?? Kwani Nape kuandika huo ujumbe ni lazima uwe Dar...? Hizi akili za kizee na very primitive mind...!!! Hajajibu kitu hapo...!!!
 
Back
Top Bottom