Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,555
- 113,738
Wanabodi,
Iwapo itathibitika pasipo shaka, (proven beyond reasonable doubt), kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi toka ndani ya daftari la vyama vya siasa, (scraped from the book of political parties), mara moja na bila huruma yoyote!.
Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifyonyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.
Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia mara kwa mara, ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.
Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.
Katika maongezi yetu kuhusu hali ya siasa hali ya siasa nchini, niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana " proved beyond reasonable doubt!" by "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA walihusika kwa kujua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili wa vyama nchini, Jaji John Tendwa, atakuwa hana option nyingine, bali kukifuta rasmi Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini, yaani CHADEMA, toka ndani ya daftari la vyama vilivyosajiliwa, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo sheria ya vyama vya siasa inavyoelekeza kwa mujibu wa katiba ya nchi hii! ambayo yeye ameapa kuilinda.
Kwa kifupi amemaanisha iwapo chama cha siasa kitathibitika kufanya ugaidi, kitafutwa!.
Hata hivyo nikadadisi zaidi, iwapo tuhuma za ugaidi zatathibitika kufanywa na chama tawala CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Baada ya swali hilo, kwanza Msajili alisita kidogo na baadae kusema kuwa kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa ya ugaidi, hatakifuta right away eti kwa sababu ni chama tawala!, kukifuta chama tawala ni kuvunja serikali iliyopo madarakani!, CCM kikifanya ugaidi, hata kivunja, bali atakipeleka mahakamani ili mahakama ndio itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!.
Hii inamaanisha as of now, Tanzania bado hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali iliyopo madarakani nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni serikali dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata chama hicho kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.
My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio ya double standards za mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kustahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake kwa kuvifuta, watu wakaishia kupiga kelele na kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki, waki vyama vingine, vikifanya makosa yale yale, vikiachwa eti kwa sababu ni chama tawala!.
Pia nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na baadhi ya wachangiaji ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa serikali na viongozi wa taifa hili!. Nilimwambia hiyo ndio maana halisi ya social forums, watu kujiachia watakavyo!.
Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha kwa watu wote wakiwemo viongozi wa kitaifa!.
Najua kuna wenzetu humu, kwao JF ni just their favorite past time na huja humu wakati hawana shughuli au kitu kingine chochote cha kufanya!, nawaomba mtuhurumie sisi ambao kwetu JF ni zaidi ya nyumbani kwetu, jf ni sebuleni kwetu, jf ni chumbani kwetu, jf ni kitandani kwetu, tunashinda JF, tunakula jf, tunalala JF, tunaamka JF, in short kwa sisi wengine wetu, jf ndio kila kitu kwetu, tunaiishi JF, yaani kwetu JF is our life that we are living for!.
Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.