@rizt, kwa maana hiyo nyie mko karibu na Labour party au? Kama jibu ndiyo basi tambua kuwa Labour party ndio waliokuwa madarakani wakati sheria inayoruhusu ndio za watu wa jinsia moja kupitishwa. Vyama vyote vikuu Uiengereza vinaunga mkono ushoga!
Demokrasia tunayoifikira tunaifuata hapa bado sana, ushabiki wetu wa siasa tunaufananisha kama ushabki wa Simba na Yanga, msimamo uliosemwa na Membe (pamoja na ukigeugeu wake mf. 'nchi haiwezi kuongozwa na DJ akimzungumzia Rajoelina, na waendesha pick ups NTC halafu kesho tunamuona JK akishikana mikono na NTC) ndio msimamo wa nchi, Tanzania ni zaidi ya vyama vya ccm, cuf na cdm, matamko ya vyama hivi kwa namna yoyote ile yanakuwa yanawahusu wananchama wao na si tanzania.
Unapotaka cdm watoe msimamo wao kwa kuwa tu conservative ni washirika wa cdm kwa jambo linalohusu nchi ni HOJA dhaifu sana na isiyo na mashiko yoyote kwa TAIFA Tanzania, nchi yetu ina itikadi zake na moja tu ni kuheshimu UTU wa mtu, watu wote ni sawa, sasa kama utaniambia itikadi na misingi ya Taifa hili inaweza kubomolewa kwa misaada au mapenzi ya vyama, nitakuelewa vinginevyo KIOJA chako kiko sawa sema kimekuja sehemu isyo sahihi.
PM wa UK alikuwa akizilenga NCHI na si vyama, kifupi ilikuwa ni kama anatuambia WATANZANIA wote kuwa kama hatutafanya wanayoona ni sahihi basi MISAADA yao wataipunguza.
Labda cha kujiuliza hapa, kama NCHI Tz, misaaada yao tunastahili kuipokea na je tunaihitaji kweli na kama tunaihitaji kweli ni isaada ya aina gani, je endapo tukiuvunja uhusiano nao kuna kitu gani tutafaidika na wao watapoteza nini.
Imani yangu ni kwa Tanzania nje ya vyama tunavyovishabikia ambavyo bila kujali ni kipi itikadi kwao na menejiment ni tatizo na kwa kuongozwa na watu wa aina hii tuliyonayo (madarakani na wanaosubiri kuingia madarakani) wanaofikiria matumbo na viuno basi si ajabu tukaendelea 'kufanywa' ombaomba na tunaowaamini kutuongoza.
Vyama tulivyonavyo bila kujali urafiki vinavyounda na vyama vya nje hatutakubali kuharibu TANZANIA yetu
Ritz, umewashika magwanda pabaya.
Wakitoa tamko la kupinga alichosema mfadhili wao si watakosa fadhila?
Mkuu, fuatilia siasa za Uingereza ndio useme, sera za kukubali mashoga ni sera za Conservative..
Chama cha Labour kinapingana na sera za mashoga..
Hakuna sehemu yoyote kwenye katiba ya Uingereza mashoga wanaruhusiwa
Wanabodi.
Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kinatakiwa kiweke wazi msamamo kwa watanzania mahusiano yao na chama cha Conservative cha Uingereza..
Conservative ni wadhili wakubwa wa Chadema wanawapa misaada mingi sana Chadema.
Tunakumbuka 2005 na 2010 Chadema walipokea misaada mingi kutoka Conservative, Pikipiki, Magari, Baiskeli, pamoja na pesa..
Waziri mkuu wa Uingereza Davidi Cameron, kutoka chama cha Conservative, alitoa kauli kwenye mkutano wa nchi wanachama wa Jumuia ya Madola (CHOGM) uliofanyika Perth, Australia..
Nchi zinazoomba misaada kwao zitambue haki za mashoga kama moja ya masharti ya kupewa misaada hiyo..
Tunaomba viongozi wa Chadema walitolee maelezo jambo hili sababu kati ya wanaopokea misaada Chadema nao inapokea
Mkuu, fuatilia siasa za Uingereza ndio useme, sera za kukubali mashoga ni sera za Conservative..
Chama cha Labour kinapingana na sera za mashoga..
Hakuna sehemu yoyote kwenye katiba ya Uingereza mashoga wanaruhusiwa
Hapa hujanena kitu...okay...chukulia mfano. Una mwanao mpendwa wa kiume, first born. Mara ghafla anaanza mambo ya kishoga, na anakwambia ana mume wake na anataka kuolewa, Kweli kuna dhambi kama hiyo? Ndugu yangu ushoga usikie kwa jirani tu! Ni aibu kubwa sana!ubatili mtupu, kwani ni kwa nini jamii yetu inachukia ushoga?-hata mmi nachukia sana tena sana na nikiona shoga au hata nikisikia uwepo wao napata kichefuchefu.
Lakini huwa najiuliza na naomba wan jf tujiulize, hivi ni nini hasa msingi wa sisi kuuchukia ushoga?
Ni mafundisho ya dini zetu? Ni maagizo ya vitabu vyetu vitakatifu?
Kwamba tunaogopa dhambi?
Tunaogopa kumkosea mungu wetu mkuu?
Na ufisadi je?
Uzinzi je?
Uwongo je?
Wizi je?
Udikteta?
Ubinafsi je?
U sisi tu je?
Yeye aliye msafi na awe wa kwanza kurusha jiwe.
Ushoga si haramu zaidi kuliko hayo mengine,
ccm na serikali yake haina haki ya kupinga ushoga kwa nguvu zake zote.
Ukichukia dhambi moja na ukakumbatia zingine inakuwaje?
Nadhani hizo nchi za magharibi zilijiuliza sana maswali haya kabla ya kutoa huo uhuru wa mashoga.
Naomba nieleweke kwamba mimi siungi mkono na wala sitaunga mkono ushoga.
Hivi kwa mfano shoga akikuuliza swali hili, ipi ni haramu zaidi kwa jamii ushoga na uzinzi utajibu vipi?
Ufisadi na ushoga?
Mbona mafisadi na wazinzi serikali zetu zinawapenda?
Jamii zinawafanyia sherehe mafisadi na akina membe hawasemi?
Serikali na wananchi wengi wayatendayo kila siku hayana tofauti na ushoga.
Kwanini mashoga wanyimwe haki wakati mafisadi wananyenyekew na kuheshimiwa?
Ni ubatili mtupu.
Kaka umeshajibiwa vizuri sana lakini inaonekana una asili ya ubishi usio na msingi hata kwa mambo yaliyo wazi. Hapo kwenye red; hivi Cameroon alikuwa anaongea kama kiongozi wa chama chake ama kama Mkuu wa Serikali ya Uingereza? Hivi alikuwa anaongelea sera za chama au sheria za nchi kutambua haki za mashoga? Hebu tumia akili bro.
Well, hebu tuliangalie suala hilo kwa mtazamo tofauti: ANC cha Afrika ya Kusini ni chama rafiki (wa damu, kufa na kuzikana) wa CCM na vyote ni vyama tawala na tena vikiwa na udhibiti wa mabunge ya nchi zao. Miaka michache iliyopita, Afrika Kusini ilitambua na kuingiza katika sheria zao "Haki za Mashoga" likiwa taifa la kwanza na pekee Afrika kufanya hivyo! Mbona hatujasikia CCM ikitangaza kuvunja "urafiki" na ANC? Tafadhali, hebu tumia akili kidogo.
Mimi naamini kabisa, kwa mtiririko wa mambo unavyoenda, CCM (CCM kama taasisi) ndicho chama kitakachoingiza nchi hii katika ushoga na si vinginevyo.
Kwa ufahamu mdogo nilionao, vyama vikiwa marafiki kabla ya kuingia madaraka, uhusiano unakoma chama kimoja kinapoingia madarakani, kwani vinginevyo mahusiano ya kibalozi lazima yatakuwa na matatizo, sasa hapa chadema wato tamko la nini wakati wao hawapo serikari?
..........Ndugu yangu umenena uwezo wa wananchi kuelewa ukochini sana tizama sisi tunaodhani twaelewa hatujui tofauti ya chama na serekali MEMBE BENARD hajatoa msimamo wa CCM ametoa msimamo wa serekali DAVID CAMERON ametoa msimamomo UK. haya ya chama ni USHAMBA wetu.Cameroun ni PM alitoa kauli ya serikali na siyo chama. Kama sheria hiyo ipo katika katiba yao hata angekuwa wa chama kingine angesema hivyo kukidhi matakwa ya nchi yao.
Hapa hujanena kitu...okay...chukulia mfano. Una mwanao mpendwa wa kiume, first born. Mara ghafla anaanza mambo ya kishoga, na anakwambia ana mume wake na anataka kuolewa, Kweli kuna dhambi kama hiyo? Ndugu yangu ushoga usikie kwa jirani tu! Ni aibu kubwa sana!
Kaka hakuna ubishi tunawekana sawa tu, labda na mimi nikuulize swali langu..
Hivi hii mikataba serikali inayongia kama mikataba ya madini kule Geita, Kahama, Nyamongo, Nyarugusu, pamoja na kuuza mali za umma. Ubinafsishaji wa makampuni, CCM hawamo wamo?
Nijibu mkuu wangu
..........Ndugu yangu umenena uwezo wa wananchi kuelewa ukochini sana tizama sisi tunaodhani twaelewa hatujui tofauti ya chama na serekali MEMBE BENARD hajatoa msimamo wa CCM ametoa msimamo wa serekali DAVID CAMERON ametoa msimamomo UK. haya ya chama ni USHAMBA wetu.
Hivi wewe juha unajua unachosema, I guess hujawahi kutoka nje ya Tanzania. Unajua maana ya
conservative? Vyama ambavyo viko pro-homesexual Ulaya na Marekani ni liberal parties hata republican
ya USA, members wake wengi including W Bush ni ma-conservative na wanapinga ushoga.
Cameroon kwenye commonwealth alikuwa anawakilisha Uingereza as head of States na sio chama cha
Conservatives, no wonder alisema NCHI read again NCHI zote ambazo hazitatambua haki ya mashoga
... na sio VYAMA read again vyama.
Eti Katiba ya Uingereza haitambui mashoga, you real look like a laughing stock, mambo ya ushoga sio
Uingerza tu bali Ulaya yote yanatambuliwa na yako kwenye katiba ya nchi hizo. Acha kuonesha upumbavu
wako hapo. Kabebe mabengi ya Nape wakati anapokwenda Ulaya ili ufunguke akili na macho unasumbuliwa
na UPORINI.
Cameroun ni PM alitoa kauli ya serikali na siyo chama. Kama sheria hiyo ipo katika katiba yao hata angekuwa wa chama kingine angesema hivyo kukidhi matakwa ya nchi yao.
Hapo kwenye red ..Acha kunidanganya ww, biblia inaniambia mfira.ji na mfirwa.ji hawatauona ufalme wa mbingu!..Hapo kwenye red; tunapotea kwa kukosa maarifa. Ukishatamka neno dhambi maana yake unazungumzia masuala ya rohoni na kiroho dhambi zote ni sawa mbele za Mungu. Usitake kupoza UFISADI kwa kutisha watu na USHOGA; tena jana nilionya kwenye thread nyingine kwamba makuwadi wa kisiasa hapa nchini wamepata hoja ya kudandia ili kuwasahaulisha wananchi taabu walizo nazo likiwepo suala la UFISADI, KUTOWAJIBIKA, UPENDELEO serikalini, na mengineyo chungu nzima kwa kushadidia hoja mpya ya ushoga.
Kijamii UFISADI ni mbaya kuliko USHOGA ila kimaadili USHOGA ni mbaya kuliko UFISADI. Kiroho (yaani kidini) UFISADI ni sawa na USHOGA. Natumaini umepata mwanga. Sasa pima mwenyewe unatazama suala lipi kwa "angle" ipi!
Hapo kwenye red ..Acha kunidanganya ww, biblia inaniambia mfira.ji na mfirwa.ji hawatauona ufalme wa mbingu!..
Ww unapata wapi ujasiri wa kuona ufisadi na ushoga ni sawa?