Chakula hufungua moyo

Chakula hufungua moyo

Bujibuji biblia imeandikwa zawadi hufungua moyo.

Hii inamaana kuwa ukikunjua mikono yako kwa namna yyte ile lazima itapokea baraka tuu. Ukimlisha mhitaj ujue na wewe utapokea na uzuri utapokea zaidi ya kile ulichokuwa unahitaj ama.kile kile.

Kwa kulijua hilo na huu msimu wa siku kuu hebu Fanya maarifa ya kapu la sikukuu kwangu. Japo tunanasi na tuembe. Tumchele kidogo na tunyama. Uone jinsi milango ya baraka itakavyo funguka kwako
looh! ndugu we utakuwa mwinjilist au paroko kabisa. sio kwa hitimisho hilo.

mmh sijawahi kujutia kusoma nyuzi za jf
 
Kweli ase.. Tatizo lipo kwa sisi binadamu wa zama za leo, tukishiba. Hatuwezi kuwakumbuka wala kuwafahamu wenye njaa.. Kutoa ni kheri.
 
Kweli kabisa mkuu, ila kwa mademu wa leo anaweza akufirisi, unakuta demu anakata tonge kama kazaliwa mashine, na akipata ofa kali yupo ladh kuhifadh chakula hata kwenye tumbo la uzazi, yan unageuzwa kua Min Hotel bila kujijua.
Hahahahaha
 
Siku ya kwanza kukutana na shemeji yenu, nilimnunulia sprite na ndizi nyama pale HAPPY cafeteria UDOM.. Nilimkuta km hana raha hivi, sikumuuliza why Yuki vile, nilimuambia karibu tule lunch akasema asante akijua natania, nilikuwa ba 5000, nikachukua tiket mbili nikapewa msosi nikaenda kwenye soda nikanunua sprite mbili, bdy alishukuru kwani hakua na kitu zaidi ya 500 ya soda tu aende kulala, sasa siku moja aliniambia mama love pamoja na mambo mengine ila nikikumbuka ile siku uliyoninunulia msosi nazidi kukupenda maana sikuwa na namna ya kuishi, Jana Yake nilikuwa numelalia chapati 2 tuu.. I niajisemea kweli ukarimu umenipa mume anipendae.
 
Mkuu Bujibuji, ndiyo maana sisi tuliopitia unyagoni tunafahamu kuwa tumbo ka mwanaume lihudumiwe kwanza kabla ya yote.

Wafaransa walilitambua hili na ndiyo walioanzisha utaratibu wa chakula na maongezi ya usuluhishi au deal za serikali. Baada ya chakula na mvinyo makubaliano hufikiwa.
 
Na njaa huuza Utu wetu.
Esau aliuza haki yake ya uzaliwa wa Kwanza alipokuwa na njaa. Njaa ni mbaya sana, yaweza kukupeleka utumwani kama ilivyowapeleka wa Israel utumwani Misri kwa miaka 400
njaa kitu kingine waweaza kufanya jambo la aibu la fedheha ili utulize njaa baadae hujikuta uko hewani mweeeee njaaaa kiboko
 
Back
Top Bottom