Chaka la simba halilali nguruwe

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Kuna hofu kubwa imetanda juu ya mwelekeo wa uongozi wa Mama Samia kulingana na matukio mengi yanayojitokeza kila siku iwe ya Ukiukaji wa maadili, uvunjaji sheria, haki na Usalama wa Wananchi upo mashakani.

Kuna hofu kubwa imetanda mioyoni mwa watu kama ugonjwa ya Uviko maana hawajui hata manufaa na usalama wa kinga zake.

Haipiti siku bila kuona ama kusoma habari za udhalilisha, Ujambazi, Uvunjaji wa sheria, Ufisadi ulokiuka na hata mauaji mengine ya kustaajabisha kabisa pale mzazi anapomuua mwanae ama mkewe kwa sababu ya Chakula!

Mauaji ni mengi, Uasherati umekuwa sifa! Uchawa ni kipimo cha utendaji! Umaskini umekithiri majumbani hakuna wa kuwasemea.

Kumeibuka hata Wachungaji wa ajabu, Masheikh wa ajabu, dini imekuwa simulizi za mapenzi na udhuru wa hadaa zinazokiuka maadili ya UTU wetu.

Maswala mazito ya Kijamii hupewa majibu mepesi sana ama hata wakati mwingi huwa hayajibiwi isipokuwa pale vipande vya video vinaposambazwa.

Haitoshi hatuoni hatua zikichukuliwa na kesho yake vitendo hivyo hujirudia tena na tena. Imefikia wakati Wananchi wageuka Chungu, kula ganda la muwa la jana.

Yawezekana Mama Samia amekuwa mpole sana ama yawezekana katika Mapungufu ya Mama ni huruma ya Mwanamke kwa wanawe jambo ambalo halitakiwi kabisa kwa kiongozi wa familia ama nchi.

Ukweli lazima tuseme maana hizi teuzi zimekuwa kama kugawa peremende.

Haiwezekani kabisa Chaka la Simba (lion den) tunawaona hata nguruwe wakilala, hapo pana tatizo la msingi kabisa.

Namshukuru sana ndugu yangu Charles Kitwanga kwa nasaha zake aliposema kuna Genge la watu (mtandao) ndani ya Serikali na nje linalomshauri vibaya Mama Samia.

Mimi labda niongezee kauli yangu kusema kwamba yawezekana Mama Samia hakuwa tayari kuliongoza Taifa hili ila alilazimika tu kwa mujibu wa Katiba. Haiwezekani maamuzi mengi ya Mama Samia anategemea sana kuona watu Wamebadilika tabia zao - haiwezekani.

Mazingira ndio hujenga tabia ya mtu na sii vinginevyo. Kila mara yeye husisitiza twende tukarekebishe! Kina nani? Matokeo bado mambo ni yale yale..

Nakumbuka siku akiapishwa hata yeye mwenyewe alikiri na kubaini kuwa hakuwa tayari.kuongoza nchi na akaambiwa (sijui na kina nani) kwamba watamsaidia asiwe na shaka! Kazi hiyo anaiweza.

Na wengi wetu tuliweka tumaini kubwa kwake kwa sababu anarithi Uongozi wa Hayati Magufuli na anajua Vema mazuri na mabaya ya kiongozi mtangulizi wake.

Waswahili wanasema "Usitupe Jongoo na mti wake" na kule Colombia nao husema "Ukila ndizi usitupe ganda lake" hizi zote ni methali zenye nasaha kubwa ndani yake na kama muumini naamini ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu ni wajibu wangu kutoa nasihi pale napoona maadili yetu yanapotoshwa makusudi - Tuendako siko hata kidogo.

Usemi usemao "Ukila ndizi usitupe ganda lake" unamhusu sana Mama Samia maana pamoja na faida nyingi za ulaji wa ndizi mbichi au mbivu, pengine Mama hakufahamu kuna lishe bora pia ndani ya ganda la ndizi ambalo hurutubisha kinga ya mwili na maradhi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Saratani.

Ganda la ndizi pia ni dawa ya ngozi huondoa madoa na mistari za uzee usoni. Katika hekma za Mwenyezi Mungu amelifanya Ganda la ndizi kuwa kinga ya tunda la ndizi lisiingiwe na wadudu hivyo, Maradhi ya Mgomba hayaathiri tunda lake.

Kwa hiyo, yawezekana kabisa Mama Samia alitofautiana sana na mtangulizi wake kiimani lakini haibadilishi malengo ya awamu, kwani mimi naamini Rais ni kiongozi msimamizi wa utekelezaji wa sera na ilani ya Chama kama zilivyo nadiwa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Sitaki kuamini kwamba hayati Magufuli hakuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura, pia sitaki kuamini kwamba Sera na Ilani za Chama cha Mapinduzi hazikuwa za Chama bali matakwa ya hayati na kundi lake wakiitwa 'Sukuma Gang'.

Sitaki pia kuamini maamuzi mengi aloyafanya hayati hayakutokana na vikao vya chama ama baraza la mawaziri bali yake mwenyewe. Kwa sababu tunayoshuhudia leo ni uwepo wa Genge la Wahuni hatari zaidi, genge ambao walifaidika sana na mikataba mibovu na misaada ya nje leo wao ndio wapokezana vijiti. Sitaki pia kuamini haya pia ni maamuzi ya Mama Samia pekee.

Nachelea kusema kwamba kama kuna wakati ambao Upinzani wana nafasi kubwa ya kushinda Uchaguzi Mkuu basi hakuna kama 2025 na wakifanya makosa basi nafasi hiyo haitarudi tena. Iwe kwamba Mama Samia atagombea, au hatagombea tunapigwa changa la macho wao wanajua vema hatagombea, basi nasema CCM hii imekalia kuti kavu. Wananchi wana hasira kuliko mwaka 2010.

Wakati huu imeanza Mikutano ya hadhara na inatumiwa kama Kampeni za Uchaguzi tayari badala ya Vyama hivyo kujiimarisha wao wakitafuta Wanachama. Kama sheria ya vyama kujitangaza ni moja ya kampeni za Uchaguzi Mkuu ujuo, bila shaka Upinzani wamewasha cheche za mageuzi!

Na kama itatokea kweli Machawa wa Mama Samia au wa vyama hivi kutokubaliana na hiki kinacho endelea, ipo hatari kubwa sana ya vurugu hatarishi kwa Usalama wa Wananchi maana Siasa sio Unazi wa Simba na Yanga. Siasa ni Maisha ya Wananchi, Siasa ni Chaka la Simba, likiingiwa Nguruwe hakuna atakaye kuwa salama..

Maasalaam.
 
Nchi ya Tanzania imechakaa mapema mno. Taifa lina miaka 62 tu, lakini tumepoteza mwelekeo na kuchoka kiakili utadhani tumepata uhuru miaka 200 nyuma.

Kikawaida ilitakiwa saa hizi ndiyo maendeleo ya kiuchumi na kisiasa yawe yamepamba moto kwasababu tabaka kubwa la nchi limejengwa na vijana wa miaka 15-35.
 
Dah!
Ni ndefu, kwa hiyo sijamaliza kuisoma yote.

Hii ni mada toka kwa "Great Thinkers Original" wenyewe, kwa hiyo siyo mada ya kubezwa hata kidogo.

Lakini imenibidi nicheke tu mwenyewe nikisoma baadhi ya hayo mambo yaliyoorodheshwa kuwa hayafai kwa jamii.

Mbona itakuwa kazi ngumu sana kuijenga nchi yenye maadili yasiyokuwa na mengi ya mambo hayo.
Hii dunia ya leo, itatoka wapi serikali yenye uwezo wa kuzima hizi takataka nyingi zisiingie kwenye jamii?

Ngoja nirudi kwenye mada, nikamalize kuisoma yote.
 
Unakumbuka zamani tukisema Waafrika wavivu wa kusoma? Basi tafadhali chukua muda wako isichoke tunakumbushana tu. Kisha Crimes hatuwezi zimaliza lkn basi japo zipungue kuwe na nidhamu na maadili yapande. Nimesoma pahala huko Mbeya Ujambazi na Kulawiti ndio jinai kubwa! Sikuyasikia haya enzi zile tukijadili Siasa na sii madudu haya.
 
Naungana nawe mtoa mada huyu kiongozi wetu hakua amejiandaa ama kuandaliwa kushika majukumu aliyopewa

Kwa hivyo yafaa mfumo uandae mtu makini na anaeweza kuongoza nchi panapo 2025 apewe upanga na nyundo atunyooshe
 
Kuna hofu kubwa imetanda juu ya mwelekeo wa uongozi wa Mama Samia kulingana na matukio mengi yanayojitokeza kila siku iwe ya Ukiukaji wa maadili, uvunjaji sheria, haki na Usalama wa Wananchi upo mashakani.

Kuna hofu kubwa imetanda mioyoni mwa watu kama ugonjwa ya Uviko maana hawajui hata manufaa na usalama wa kinga zake.

Haipiti siku bila kuona ama kusoma habari za udhalilisha, Ujambazi, Uvunjaji wa sheria, Ufisadi ulokiuka na hata mauaji mengine ya kustaajabisha kabisa pale mzazi anapomuua mwanae ama mkewe kwa sababu ya Chakula!

Mauaji ni mengi, Uasherati umekuwa sifa! Uchawa ni kipimo cha utendaji! Umaskini umekithiri majumbani hakuna wa kuwasemea.

Kumeibuka hata Wachungaji wa ajabu, Masheikh wa ajabu, dini imekuwa simulizi za mapenzi na udhuru wa hadaa zinazokiuka maadili ya UTU wetu.

Maswala mazito ya Kijamii hupewa majibu mepesi sana ama hata wakati mwingi huwa hayajibiwi isipokuwa pale vipande vya video vinaposambazwa.

Haitoshi hatuoni hatua zikichukuliwa na kesho yake vitendo hivyo hujirudia tena na tena. Imefikia wakati Wananchi wageuka Chungu, kula ganda la muwa la jana.

Yawezekana Mama Samia amekuwa mpole sana ama yawezekana katika Mapungufu ya Mama ni huruma ya Mwanamke kwa wanawe jambo ambalo halitakiwi kabisa kwa kiongozi wa familia ama nchi.

Ukweli lazima tuseme maana hizi teuzi zimekuwa kama kugawa peremende.

Haiwezekani kabisa Chaka la Simba (lion den) tunawaona hata nguruwe wakilala, hapo pana tatizo la msingi kabisa.

Namshukuru sana ndugu yangu Charles Kitwanga kwa nasaha zake aliposema kuna Genge la watu (mtandao) ndani ya Serikali na nje linalomshauri vibaya Mama Samia.

Mimi labda niongezee kauli yangu kusema kwamba yawezekana Mama Samia hakuwa tayari kuliongoza Taifa hili ila alilazimika tu kwa mujibu wa Katiba. Haiwezekani maamuzi mengi ya Mama Samia anategemea sana kuona watu Wamebadilika tabia zao - haiwezekani.

Mazingira ndio hujenga tabia ya mtu na sii vinginevyo. Kila mara yeye husisitiza twende tukarekebishe! Kina nani? Matokeo bado mambo ni yale yale..

Nakumbuka siku akiapishwa hata yeye mwenyewe alikiri na kubaini kuwa hakuwa tayari.kuongoza nchi na akaambiwa (sijui na kina nani) kwamba watamsaidia asiwe na shaka! Kazi hiyo anaiweza.

Na wengi wetu tuliweka tumaini kubwa kwake kwa sababu anarithi Uongozi wa Hayati Magufuli na anajua Vema mazuri na mabaya ya kiongozi mtangulizi wake.

Waswahili wanasema "Usitupe Jongoo na mti wake" na kule Colombia nao husema "Ukila ndizi usitupe ganda lake" hizi zote ni methali zenye nasaha kubwa ndani yake na kama muumini naamini ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu ni wajibu wangu kutoa nasihi pale napoona maadili yetu yanapotoshwa makusudi - Tuendako siko hata kidogo.

Usemi usemao "Ukila ndizi usitupe ganda lake" unamhusu sana Mama Samia maana pamoja na faida nyingi za ulaji wa ndizi mbichi au mbivu, pengine Mama hakufahamu kuna lishe bora pia ndani ya ganda la ndizi ambalo hurutubisha kinga ya mwili na maradhi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Saratani.

Ganda la ndizi pia ni dawa ya ngozi huondoa madoa na mistari za uzee usoni. Katika hekma za Mwenyezi Mungu amelifanya Ganda la ndizi kuwa kinga ya tunda la ndizi lisiingiwe na wadudu hivyo, Maradhi ya Mgomba hayaathiri tunda lake.

Kwa hiyo, yawezekana kabisa Mama Samia alitofautiana sana na mtangulizi wake kiimani lakini haibadilishi malengo ya awamu, kwani mimi naamini Rais ni kiongozi msimamizi wa utekelezaji wa sera na ilani ya Chama kama zilivyo nadiwa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Sitaki kuamini kwamba hayati Magufuli hakuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura, pia sitaki kuamini kwamba Sera na Ilani za Chama cha Mapinduzi hazikuwa za Chama bali matakwa ya hayati na kundi lake wakiitwa 'Sukuma Gang'.

Sitaki pia kuamini maamuzi mengi aloyafanya hayati hayakutokana na vikao vya chama ama baraza la mawaziri bali yake mwenyewe. Kwa sababu tunayoshuhudia leo ni uwepo wa Genge la Wahuni hatari zaidi, genge ambao walifaidika sana na mikataba mibovu na misaada ya nje leo wao ndio wapokezana vijiti. Sitaki pia kuamini haya pia ni maamuzi ya Mama Samia pekee.

Nachelea kusema kwamba kama kuna wakati ambao Upinzani wana nafasi kubwa ya kushinda Uchaguzi Mkuu basi hakuna kama 2025 na wakifanya makosa basi nafasi hiyo haitarudi tena. Iwe kwamba Mama Samia atagombea, au hatagombea tunapigwa changa la macho wao wanajua vema hatagombea, basi nasema CCM hii imekalia kuti kavu. Wananchi wana hasira kuliko mwaka 2010.

Wakati huu imeanza Mikutano ya hadhara na inatumiwa kama Kampeni za Uchaguzi tayari badala ya Vyama hivyo kujiimarisha wao wakitafuta Wanachama. Kama sheria ya vyama kujitangaza ni moja ya kampeni za Uchaguzi Mkuu ujuo, bila shaka Upinzani wamewasha cheche za mageuzi!

Na kama itatokea kweli Machawa wa Mama Samia au wa vyama hivi kutokubaliana na hiki kinacho endelea, ipo hatari kubwa sana ya vurugu hatarishi kwa Usalama wa Wananchi maana Siasa sio Unazi wa Simba na Yanga. Siasa ni Maisha ya Wananchi, Siasa ni Chaka la Simba, likiingiwa Nguruwe hakuna atakaye kuwa salama..

Maasalaam.
Wewe ndiye yule prof mwenyekiti wa kikosi kazi?
 
Mbona umerundika maandishi tu na kugusa gusa maneno bila kuonesha unataka kusema nini?

MATATIZO mengi ya kimfumo nchi hii hasa yanayowasumbua wananchi wa chini, yanatengenezwa kwa makusudi.

Tanzania Kuna vi-system vidogo vidogo viiiiingi na kwenye kila kisystem kuna TABAKA la ulaji ambalo linafanya hivyo ili kulinda TABAKA la juu.

MIFANO.

- Kikokotoo Cha MAFAO ya wastaafu wa chini hakiathiri TABAKA la kisiasa, kinaumiza wananchi wa chini pekee. Kwa lugha rahisi, BUNGE lilipewa muswada wa Kikokotoo lipitishe Kama Rushwa kwakuwa WAO HAKIWAHUSU.

- Mwananchi wa kawaida anavyotaabika na FOLENI, wao genge la kisiasa wanapita na Ving'ora hivyo foleni kwao siyo TATIZO.

- Tunaishi ndani ya nchi MOJA lakini katika MIFUMO TOFAUTI kabisa ndio maana MATATIZO YA NCHI HII HAYATAKUJA KUISHA.

Na sababu kubwa ni kuwa HAKUNA TEUZI zinazofanyika ili kuweka PROBLEM SOLVERS na THINKERS kwenye maeneo ya Utawala.

Sote tunajua, January Makamba Ridhiwani Kikwete Mchengerwa, Pinda Jr, Zahra MICHUZI, Nnape Nnauye etc sababu ya kwanza ya kwanini wapo kwenye nafasi walizonazo ni FADHILA kutokana BABA ZAO. Suala la Wana uwezo au hawana linakuwa namba 2, maana hata wasipofanya chochote hakuna kitu watafanywa.
 
Unakumbuka zamani tukisema Waafrika wavivu wa kusoma? Basi tafadhali chukua muda wako isichoke tunakumbushana tu. Kisha Crimes hatuwezi zimaliza lkn basi japo zipungue kuwe na nidhamu na maadili yapande. Nimesoma pahala huko Mbeya Ujambazi na Kulawiti ndio jinai kubwa! Sikuyasikia haya enzi zile tukijadili Siasa na sii madudu haya.
Tatizo siyo uvivu wa kusoma bali ni kuelewa mada wanazosoma. Ukiandika mambo ya kidaku udaku hata ukaweka page mbili watasoma zote! Kuna mwandishi mmoja huwa anaweka page hadi kumi ndefu sana za kiudaku hapa na huwa zinasomwa zote!
 
Nilidhani wewe Mkandara na Kichuguu mlipitiwa na Covid 19, hongereni sana na Asante kwa Muweza kuwapa pumzi ya uhai make sikuwasoma muda mrefu sana kwenye jukwaa la Great thinkers.

karibuni sana, au mlitishwa mkatishika kwelikweli.
 
Mkandara,
Umezungumzia kwanini Mama Samia anatupa Ganda la Ndizi...ukimaanisha anawaondoa wasaidizi wa walioteuliwa na awamu iliyopita.
Swali ni je, Ganda la ndizi likiwa na makovu, uchafu pamoja na wadudu bado linakuwa na maana ya kutibu afya?
 
Back
Top Bottom