Ana ndoto nzuri,
ni lazima tumsapoti,
Anaota mafanikio,
akijua uwezo tunao.
Mafukara wa akili,
huiga wakoloni,
Mkoloni aliiba Tanzania,
na kupeleka ulaya.
vibaraka weusi pia,
Waiibia Tanzania,
wapeleka ulaya bila aibu,
huku wakijiona wajanja,
wangekuwa na akili lau kidogo,
wangeenda kuishi huko.
Chenge na wenzake hufurahi,
akaunti zao zikijaa vijisenti,
ndoto zao ni nyonga na viuno,
akili zao makalio matupu.
Na wale wenye 300 billions Uswis,
Ndoto zao ni Wao na wake zao,
Wameiba wameharibu na kutapanya,
bado watamani hata maziwa ya watoto?