Kishimbe wa Kishimbe
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 6,121
- 6,062
Jamani 'ACHENI MASKHARA' basi, yaani mnamaanisha huyo askari anayeruka, kushoto, ndiye CHAGONJA?
mangatara
Ninyi muishi tu kwa assumpitions hizohizo badala ya kustuka na kutoa ushirikiano kwa serikali,kalieni hayohayo kwamba ni mbinu zaCCM.
Tuombe uzima. Mtakiri tu kwamba ushabiki kama huo mnaoufanya hauna mantiki hata kidogo.
Take my words with a special regards. Nakuhakikishia jambo hilo.
Yaani factors zote zinazoifanya Boko haram iwepo hakuna hata moja TZ, halafu hivi kama hata hao alshabab wameshindwa kukaa kwenye ardhi ya Kenya zaidi ya kuvizia na kukimbia, wanalikimbia Jeshi disorganised kama Kenya halafu kikundi cha wahuni ambao hawajui hata dunia inaendaje kilisimamishe JWTZ kwa masaa 48? Kisha unasema hii issue ni serious, kwani serious kuliko bomu lililorushwa kwenye mkutano wa chadema halafu polisi wakawa wanamlinda mrushaji?Mh! kwamba Tz ndo mwamba kuliko Nigeria ktk Africa au Kenya kias yakwamba hakuna Kikundi chochote cha kigaidi kinaweza kufanya vurumai?
Huo ni mtazamo wako tu mkuu. Amini issue hii iko serious.
Unajivamia,unajiteka,unajitorosha,unajisaka na hatimaye unatangaza kujitafuta kwa udi na uvumba.Matukio yote haya haya hayana majina ya waathirika.
Kweli siasa zimefikia mahala pake!Tutashuhudia mengi 2015.
Yetu macho...
Eti magaidi... inakuwaje watu waingize silaha nzito nzito za kivita mpaka waweke kambi!! Mapango ya mamwe nisehemu ambayo watu kila kukicha wanashinda huko kuvuma amwe ya kuuza...ati leeo ni pango la magaidi...
Wazee wa kushika hatamu wamefilisika, wananjuua hakuna wimbo watakaoleta tuwasikilize, wamegundua vitisho.
Najiuliza, kwani kikiingia magogoni chama chochote si watambapana tu na magaidi au lazima wawe wao... waiti a minute, wakishinda..."magaidi" watapotea...
Tuntemeke kwa jinsi unavyojitahidi kupambana kulazimishia kwamba hili movie ni la kweli nahisi wewe ni mmoja wa watu waliotunga hili movie. Hivi nyinyi viongozi wetu mmelala kwenye kitanda cha aina gani? Toka ile michango ya jana huku ya wananchi kuonyesha wameshtukia hili movie si mngepotezea tu nani angewauliza? Zamani mlikuwa mnatunga movie za aina hii watu wanazikubali maana walikuwa bado wamelala, kumbuku majambia ya CUF, matokea yake wale waliokuwa wamelala wameamka nyinyi ndio mmeingia usingizini. Kama kazi ya ulinzi wa nchi imewashinda si muende mkacheze tu movie za kivita? Au wewe ndio ulikuwa unazunguka zamani na zile sinema za vita za Rwanda kuwaaminisha watu kwamba wakichagua upinzani kutatokea vita?
Huko kwenye jeshi la polisi kuna polisi vijana na wana elimu nzuri tu, si bora muwaachie kuliko kuendelea kuwamezesha mbinu za kizamani wakati dunia imebadilika. Maana ninachokiona baada ya kuona movie linabuma ikabidi muongeze magari kwenda huko ili mlazimishe kile watu wanachopinga, toka lini polisi wakazuia waandishi wa habari kupiga picha? Picha zinapigwa hata kwenye vita sembuse watu mnaodanganya wamejificha kwenye mapango. Halafu kwa usanii wa namna hii ndio tutegemee siku tukivamiwa kukamata adui achilia mbali kumshinda? Acheni kuchezea kodi za wananchi kwa propaganda za kizee wengine tunategemea utalii bana.
Mkuu lakini hii hali ya kutoaminika kwa baadhi ya mambo yakiwemo haya ya ugaidi ni CCM wenyewe ndio wamesababisha kwa ujinga wao.Mara ooh CHADEMA magaidi wakiulizwa wamefanya ugaidi gani? utawasikia wanaume wazima wanakwambia wamemwagia mtu tindikali,mara ooh Lwakatare anataka kumteka Msaky,mara ooh CHADEMA wamemteka Ulimboka huku Raisi wa nchi anacheka bila kuona athari ya ujinga huu wa akina Mwigulu.Mara ooh Chadema Wamejilipua Arusha.Wakiambiwa unda tume hawataki,mara ooh kitu chenye ncha kali kutoka wafuasi wa Chadema kilimpiga marehemu Ali Zona,mara kitu kilirushwa kutaka walipo wafuasi wa Chadema kikamlipua Mwangosi.Sasa upuuzi wote huu unawafanya raia wanaidharau serikali kwa matukio kama haya (Ugaidi) Polisi,Mwigulu,Nape na yule mkubwa wao ujinga ujinga ujinga.
Naam, You may have point. Lakini yote hii ni ishara kwamba kila kukicha ufa ndani ya Tanzania unazidi kupanuka na ghadhabu miongoni mwa baadhi ya wananchi inaongezeka. Mimi na wewe, pamoja na watawala wetu, tunadhani hao ni wachache; hawatufanyi kitu! Lakini hawa ni wa-tz, swali ufa huu na ghadhabu hizi zimetoka wapi? mbona miaka michache hazikuwepo? Hivi, zimeanza lini hasa? Kila mmoja wetu ana jibu lake. Lakini Mwalimu alituonya katika uhai wake kuwa ni ujinga kudhani kuwa Tanzania ni tofauti na Somalia; kwa maana kwamba ipo "stable'. Alionya kuwa nchi za Kiafrika zote ni dhaifu sana kiasi kwamba kitu kidogo kinaweza kuwagawa wananchi na nchi ikasambaratika. Kwetu sisi hapa, hicho kitu kidogo kinachotugawa sasa ni ubinafsi wa wanasiasa wetu. Tufanye tafakuri ya kina; vinginevyo tutaumia sote kama jamii moja.
Mh! mimi si kiongozi. Ni raia tu kama wewe mkuu. Najaribu kutumia haki yangu ya msingi kueleza kile ninachokiamini juu ya jambo hili na mengneyo.
Ni bahati mbaya sana kila mtu ana uhuru wa kusema yanayomsibu na anayoona ni sahihi. Na ni katika uhuru huu ndipo watu hupindisha kwa maslah binafsi(tena bila hata sababu maalum).
Shime Watanzania. Nchi hii inahitaji mitazamo zaid ya ushabiki huu tunaojiingiza kwao.
Thnx!
Unajivamia, unajiteka, unajitorosha, unajisaka na hatimaye unatangaza kujitafuta kwa udi na uvumba. Matukio yote haya haya hayana majina ya waathirika.
Kweli siasa zimefikia mahala pake! Tutashuhudia mengi 2015.
Umesahau mapanga ya IGP Mahita na hayo makontena? Kumbe mapanga hayo yalichorowa rangi na bendera ya CUF pale polisi Kilwa Road. Uchaguzi unakuja, elimu bure, matokeo ya kidato cha nne WOTE wamefaulu, MUNGU wangu nchi hii.........
Wakumbuke "to every action there is an equal and opposite reaction" wanatengeneza magaidi wa kufeki ipo siku watakuja kuwadhulu wao wenyewe.
Hii sio serikali ya kuipa ushirikiano hata kidogo jinsi walivvogeuza taifa kuwa lakizushi ni kuwakatalia kabisa Polisi kuendelea na sinema za kichinamangatara
Ninyi muishi tu kwa assumpitions hizohizo badala ya kustuka na kutoa ushirikiano kwa serikali,kalieni hayohayo kwamba ni mbinu zaCCM.
Tuombe uzima. Mtakiri tu kwamba ushabiki kama huo mnaoufanya hauna mantiki hata kidogo.
Take my words with a special regards. Nakuhakikishia jambo hilo.
exactly![]()
Jamani 'ACHENI MASKHARA' basi, yaani mnamaanisha huyo askari anayeruka, kushoto, ndiye CHAGONJA?
TUNTEMEKESang
Mheshimiwa usiitetee CCM, unless kama unajua unachokitetea. Toka mwaka 1995 CCM imekuwa ikitumia mbinu chafu kuwavuruga watz ili kibaki madarakani. Mwaka 1995 walivitumia vyombo vya habari kurusha picha za mauaji ya Rwanda na kuelezea kuwa Vyama vya upinzani vikichaguliwa vitaleta mauaji. Mwaka 2000 CCM walisimama kidete kupublish kuwa CUF ni chama cha kiislam huku wakijua kabisa kuwa hakuna chama cha kidini kinaweza kupata usajili nchini, walilitumia Polisi pia kuonesha kuwa CUF walikuwa na mpango wa kuleta vurugu.
Mwaka 2005 walitumia sana habari ya ukabila, wakiichafua chadema na mbowe kwa kusema chama ni cha wachagga na kwamba chadema ikishinda itakuwa balaa. Mwaka 2010 hilo kila mtu aliona jinsi ccm walivyoimarisha nguvu kubrand chadema kama chama cha kikristu na kuwa Slaa ni padre ambaye akishinda atasimamia ajenda za RC na propaganda hizi ziliambatana na matukio ya kuhatarisha usalama ili kuwakumbusha watu umuhimu wa kutowachagua wapinzani.
Ndio maana nasema Polisi kwasasa hawawezi kushawishi watu kwa sasa mpaka baada ya uchaguzi ndio sasa tunaweza kuongea lugha moja. Lakini vinginevyo hii itabaki ni mpango wa ccm na chagonja, maana naona movie inaelekea kuonesha kuwa kikundi hicho ndio kimekuwa kikiiba silaha za polisi kwaajili ya shughuli zao.
maneno hayo aliyasema baada tuu yakukabidhiwa sanduku lekundu lilojaa mafwedha, na wewe ukawa ndio msabazaji wa taarifa ulipotea kidogo baada ya kutoka kwenye pay roll ya Lumumba karibuTeh! mara ooh CHACHA WANGWE aliuawa na CDM?(naona hili ulilisahau Mkuu).
Lakini naamini hata kama si ktk matukio yote hayo, lakini kuna baadhi kabisa CDM imejihusisha nayo. Be it directly or indirectly.
Habari ya CDM kumuua Wangwe imekuja kutanabaishwa na Z.KABWE.
"Mlimuua Chacha Wangwe, mimi hamtaniweza"-Z.KABWE akiwaeleza CDM. Sasa sijui huyo naye ni CHAGONJA au aje!
Hakuna anayengoja majibu labda wewe na co Lumumba product wote tunajua mchezo wa CCM umefika kikomo manake kila mtu anawajua uchaguzi ukikaribia wanakuja na mbinu za kuwatisha wananchi history lives kwa sasa wawadanganye wake zao, waume zao na wana wao sio watanzania kuchele kumekucha hakuna mamburulaziSi kweli mkuu.
Kwamba kikundi kiundwe na Serikali kwa dhumuni la kuzuru na kuuwa Polisi & Wanajeshi?
Tuache "poor assumptions" jamani. Mwisho wa siku ni mimi na wewe ndio tutakaoteteleka in case tukibeza na kuchangia kuliangusha jeshi lisifanye kazi yake.
Nina ushahidi wa mahala fulani huku kwetu. Watu wamewanyima ushirikiano Polisi kuchunguza mauaji fulani kisa tu eti ni PoliCCM.
Let's go. Itafahamika tu.