Nakupongeza kwani umejibu kwa busara, lakini busara yako haitalisaidia taifa letu kwani wewe ni mmoja wapo ya watu ambao hata mambo yakiharibika huwa mnasema usibishane na serekali. Inakuwa kama serekali ni sehemu ambayo hata ikifanya kosa basi hupaswi kuionya. Na huwa najisikia vibaya sana ninapokutana na mtu anayekwepa wajibu wake kwa serekali tena kwa kutumia majibu ya busara kama yako. Watu kama nyinyi ndi mmechangia nchi yetu kuendeshwa kitapeli na kiujanjaujanja eti kisa ni serekali imeamua. Jitambue ndugu serekali ni wewe na unao wajibu mkubwa kuliko kuweka busara mahali unaona kodi zetu zinapotea bure. Hivi kama kweli sio unayechangia serekali kufanya ipendavyo, imegundulika walioko kule sio magaidi bali ni vibaka tu kama vibaka wengine kwanini itumike nguvu kubwa vile wakati zingeweza kwenda gari zisizozidi 3, yale mavx siku hizi yamekuwa magari yakivita? Unakwenda kupambana na gaidi ukiwa kwenye kiyoyozi!! Ndugu yangu jisikie aibu kutetea mambo yasiyo na tija. Ni kweli wewe umejaribu kuchomoka kwenye tundu la kusema ni ushabiki nakubaliana na wewe kabisa. Hivi si umesikia kuna hela zilichukuliwa kule stanbic kinyume na utaratibu? Ni madifender na mavx mangapi yamekwenda kujua hayo majina achia mbali hata kurudisha hizo hela. Unapoamua kuonyesha unatumia busara huoni kama umekuja kupotosha zaidi. Naomba dhamira yako ikusute kama wewe ni mkweli. Samahani kwa kukukwaza ndugu yangu. Ila tafakari na simamia ukweli.
maneno hayo aliyasema baada tuu yakukabidhiwa sanduku lekundu lilojaa mafwedha, na wewe ukawa ndio msabazaji wa taarifa ulipotea kidogo baada ya kutoka kwenye pay roll ya Lumumba karibu
Hakuna anayengoja majibu labda wewe na co Lumumba product wote tunajua mchezo wa CCM umefika kikomo manake kila mtu anawajua uchaguzi ukikaribia wanakuja na mbinu za kuwatisha wananchi history lives kwa sasa wawadanganye wake zao, waume zao na wana wao sio watanzania kuchele kumekucha hakuna mamburulazi
Teh! mara ooh CHACHA WANGWE aliuawa na CDM?(naona hili ulilisahau Mkuu).
Lakini naamini hata kama si ktk matukio yote hayo, lakini kuna baadhi kabisa CDM imejihusisha nayo. Be it directly or indirectly.
Habari ya CDM kumuua Wangwe imekuja kutanabaishwa na Z.KABWE.
"Mlimuua Chacha Wangwe, mimi hamtaniweza"-Z.KABWE akiwaeleza CDM. Sasa sijui huyo naye ni CHAGONJA au aje!
Ndiko wanakoelekea mkuu!CHAGONJWA muvi imeshitukiwa,aibu yenu aibu yao waliowaingiza mkenge(ccm).....bora ufilisike mali sio akili,mnakoelekea mtakuja mumteke tezi dume mseme magaidi
Ondoa upuuzi,usalama wanchi haulindwi kwa mbwembe na vitisho vyakipumbavu.Huko uliko unaishi dunia ya miaka ipi?Embu acha siasa kwenye maswala serious kama usalama Wa nchi..
Kama ki2 hukijui no bora unyamaze
Unajivamia, unajiteka, unajitorosha, unajisaka na hatimaye unatangaza kujitafuta kwa udi na uvumba. Matukio yote haya haya hayana majina ya waathirika.
Kweli siasa zimefikia mahala pake! Tutashuhudia mengi 2015.
Madhara kama hayo ya watu kukataa kutoa ushirikiano kwa polisi, mie na wewe tunakubaliana kuwa ni jambo la hatari lakini tunatofautiana ktk suala la nani anawajibika kwa hilo na jinsi ya kulitatua. Mie naamini anayetakiwa kubeba lawama ni ccm kwasababu wao ndio wamekuwa wanavunja katiba kwa kulitumia vibaya polisi na wameparalyse system kiasi kwamba wao wanaweza kufanya lolote na system isiwadhibiti, hii tabia wameifanya muda mrefu mpaka imeanza kutupeleka sehemu mbaya. Na kwasasa anayeweza kututoa hapa tulipo ni ccm wenyewe wakubali sheria zifuatwe na kila mtu awajibike inavyotakiwa bila kujali kama ni mwanaccm au la. Na polisi waoneshe utendaji wa haki na usawa, kinyume cha hapo nchi itafikia mahali ambapo hata Congo kuna afadhali. Kwa upande wako wewe unataka tusympathise na vyombo vya ulinzi na tufanye kazi ya kulaani tu bila kuaddress mzizi wa tatizo ambao ni ccm, Hapo ndipo sasa hatuwezi kukubaliana hata kama amani inaanza kulegalega. Dawa ni kumtwisha lawama na ikiwezekana kumuwajibisha anayehusika na sio kupiga chenga na kufumbia macho uozo kama enzi za zidumu fikra za mwenyekiti. Nashindwa kuelewa kwanini huoni uwezekano wa baadhi ya watu kuweza kuwatoa kafara hata polisi na wanajeshi wakati ni hao hao walioweza hata kutengeneza visu na kuipakazia CUF huku wakijua athari zake zinaweza kujenga ufa utakaokuja kuua mamilioni ya watz, Kama wanaweza kuigawa jamii kwa misingi ya wakristu na chama chao na waislam na chama chao, wanashindwaje kuwatoa kafara polisi na wanajeshi wawili watatu ili mradi wabaki madarakani?Si kweli mkuu.
Kwamba kikundi kiundwe na Serikali kwa dhumuni la kuzuru na kuuwa Polisi & Wanajeshi?
Tuache "poor assumptions" jamani. Mwisho wa siku ni mimi na wewe ndio tutakaoteteleka in case tukibeza na kuchangia kuliangusha jeshi lisifanye kazi yake.
Nina ushahidi wa mahala fulani huku kwetu. Watu wamewanyima ushirikiano Polisi kuchunguza mauaji fulani kisa tu eti ni PoliCCM.
Let's go. Itafahamika tu.
Duh, kuna mtu humu anajiita TuntemekeSanga! Kwa kweli haifanyii haki hilo jina...Tumeshuhudia serikali za mataifa dunia nzima zikipambana na ugaidi na hata jana tu Sweden nchi ambayo miaka yote ilikuwa shwari magaidi wamejitokeza. Ni wajibu wa serikali kuwafahamisha wananchi wake kila hatua wanayochukua katika mapambano dhidi ya magaidi ili kurudisha imani kwamba vyombo vya usalama na ulinzi viko imara na vinafanya kweli.
Akiuawa hata gaidi moja ni jambo kubwa la kupongezwa...ni breaking news na picha yake inaoneshwa. Akiuawa mwana usalama moja ni jambo kubwa la kusikitisha na katika vyombo vyote vya habari ni breaking news kwenye redio na runinga na front page kwenye magazeti. Waandishi wa habari wana jukumu la kufuatilia na kuripoti hatua zote zinazochukuliwa na serikali kuyakabili hao magaidi...wananchi wana haki ya kupata habari kuhusu kinachoendelea.
Hii ya Tanzania haijawahi kutokea popote pale labda nchi ya kusadikika. Hata kwa majirani zetu Kenya, dunia ilijua kinachoendelea serikali ilipokuwa ikipambana na magaidi. Hii ya Tanzania ni usanii wa kipumbavu na wa kitoto na mtu yeyote mwenye akili timamu anayeunga mkono kauli ya serikali kwa huu ujinga unaotendeka ameshupaa. Namkumbuka msemaji wa Polisi, Advera Senso na tamko lake kuhusu kulipuliwa kwa mwandishi wa habari Mwangosi.
Tuliambiwa kuwa kuna bomu lililotupwa kwa mkono kutoka kwa wafuasi wa Chadema na kuwa waliohusika wamekamatwa wakiwa njiani kuelekea Mbeya. Kama si ushahidi wa picha hadi leo kuna viongozi wa Chadema bado wangekuwa wanaozea selo. Hii serikali kweli kwa sasa imezidi uhuni. Sitamsahau mnadhimu wa JWTZ, Abdulrahman Shimbo huku akizungukwa na maafisa wa juu wa Polisi na TISS akitoa kauli ya vitisho kwa wananchi mwaka 2010...
....kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!
TuntemekeSanga, je umeiona hii picha? Hii picha kwa sasa ndio inatumika kuonesha mapambano ya Amboni dhidi ya magaidi wa kuchonga. Hebu soma maelezo yaliyoambatana na hiyo picha halafu uangalie ni lini hii picha ilipigwa."Tanzania ni zaid ya tuijuavyo"...Kwamba sasa tusiseme lolote au?
By the way,nimekusoma vizur tu. Shida kubwa ni kwa nini picha za polisi walojeruhiwa na JW alouawa hazijawekwa bayana. Naku aliana na wewe kuwa hii si nzuri na inaweza ikazalisha hari ya sintofahamu ktk zama hizi za TEKNOHAMA. Ila, tumeelekezwa hadi kijiji alichoenda kuzikwa Shujaa huyo. Sidhani sasa kama itakuwa ni usanij tena maana wanakijiji wapo na wanaweza toa ushahidi(tofauti na kaburi la Balali)
Lakini,jambo kubwa na lakuhimizana hapa nikutofanya masihara na kubeza habari hizi ambazo ni hatari of course. Kwangu mimi ni sawa na kupuuza habari ya Mungu na Mbingu halafu unfortunately ukaenda kukumbana navyo huko.
Tuache siasa badala yake tujikite ktk kutafuta ukweli na kuchukua tahadhari stahiki juu ya jambo hili. Sio kuingiza uCCM na uCHADEMA.
"Tanzania ni zaid ya tuijuavyo"...Kwamba sasa tusiseme lolote au?
By the way,nimekusoma vizur tu. Shida kubwa ni kwa nini picha za polisi walojeruhiwa na JW alouawa hazijawekwa bayana. Naku aliana na wewe kuwa hii si nzuri na inaweza ikazalisha hari ya sintofahamu ktk zama hizi za TEKNOHAMA. Ila, tumeelekezwa hadi kijiji alichoenda kuzikwa Shujaa huyo. Sidhani sasa kama itakuwa ni usanij tena maana wanakijiji wapo na wanaweza toa ushahidi(tofauti na kaburi la Balali)
Lakini,jambo kubwa na lakuhimizana hapa nikutofanya masihara na kubeza habari hizi ambazo ni hatari of course. Kwangu mimi ni sawa na kupuuza habari ya Mungu na Mbingu halafu unfortunately ukaenda kukumbana navyo huko.
Tuache siasa badala yake tujikite ktk kutafuta ukweli na kuchukua tahadhari stahiki juu ya jambo hili. Sio kuingiza uCCM na uCHADEMA.
Panya road,uvamizi wa vituo vya police,kikombe cha babu loliondo,homa ya dengue, hizi filamu zote zime hit kwa muda mfupi sana kupotea sokoni