uso wa nyoka;
ngoja tu niweze ku declare my interests;
Mimi simo kwenye system, ila naona kuwa weye umo kwenye system. Yaani waweza sema kitu kikaeleweka huko kwenye hii serekali.
Uso wa nyoka
Mkuu Mimi ni raia wa kawaida mwenye mapenzi mema na nchi yangu, na pia natambua thamani ya amani katika nchi.
Mangatara
Elewa hivi, nataka nikufahamishe kuwa sijakosea niliposema; Aliyeibuni propaganda hii asilipwe mshahara au posho yake. Hakujua tyming.
Uso wa nyoka
Sawa inawezekana ni propaganda ndio, lakini je hutambui kuwa kuna watu wenye nia za kufanya uhalifu kama huo hapa nchini? Tukio la amboni ni mfano mzuri na ushahidi kuwa tunao katikati yetu, sasa je ushahidi kuwa hizo ni propaganda au matukio ya kutengenezwa ni upi hadi tuconclude hivyo? Nasema hivyo kwa sababu swala la chokochoko kama hizi tukilichukulia kwa mzaha, litatugharimu sana kwa kuwa tunachukulia na kujiaminisha kuwa hivi vitu havipo na kuendelea kuwalea wanaofanya hayo au walio na nia hiyo ambao tunaishi nao miongoni mwetu kwa kuamini kuwa serikali ndio culprit.
Mangatara
mara nyingi, hao wadau wa serekali huwa aidha nusu siku nyuma ya kila propaganda yao. Unaposema mfano wa maaskari waliokufa huko na huko kuwa je ni wote tulioneshwa, nasema sio wote ila usilinganishe 50 wakaoneshwa 5 tu ili kukidhi mioyo/ kuisuuza mioyo ya watz waliofiwa kuwa huenda yule wa kwangu ataoneshwa siku moja. Nadhani umenielewa halafu ulinganishe na askari mmoja tu aliyeuawa na magaidi akiwa kazini yaani kwenye field ya vita. Huyu usipo mwonyesha alivyo fanyiwa heshima, nasema penda usipende, huku ni kuua ari ya jeshi letu.
Uso wa nyoka
Siku zote askari anaeenda kwenye mapambano kwa ajili ya taifa lake huwa ni mtu mwenye kujitolea kufa kwa ajili ya nchi yake kwani hiyo ni sehemu ya matokeo ya kazi aliyojitolea kuifanya. Sifa na heshima iliyo katika mtazamo wetu ni sehemu ndogo sana ya mambo muhimu anayozingatia askari na endapo wangetaka hayo, nchi ingekuwa ya ovyo iliyo na askari wasio na discipline kwani askari wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu sana kwa ajili ya kuilinda nchi. Pamoja na kulipwa mshahara, marupurupu n.k ile sacrifice ya maisha yao ni jambo linaloonyesha jinsi ambavyo kulitumikia taifa wamekuweka mbele zaidi ya vitu vingine. Sasa unaposema heshima ya kuzikwa kwenye TV, sidhani kama hilo lidipofanyika basi kuna askari watakosa ari kwa sababu labda nikwambie tu kuwa kifo sio sherehe na askari yoyote analijua hilo. Na hata kama unaona kulikuwa na ulazima wa hilo swala kutangazwa kwenye luninga na haikuwa hivyo, mamlaka za jeshi zinafahamu sababu za kufanya hivyo ambazo si lazima wazieleze na kwa hili zipo nyingi tu na hata walio katika vitengo husika wanajua hilo.
Mangatara
Huwezi onesha vifaru na mizinga uache kuonesha mmoja wa hao vinara alipoanguka na kuzikwa. Amini utakavyo ila that is not good