Chafya

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,077
Habari zenu wanajamvi,nilikuwa naomba ufahamisho,hivi ni kwann binadamu tunapga chafya?na je? wanyama nao wanapga chafya.
 
Kupiga chafya (sternutation) ni kitendo cha utowaji wa hewa kwa nguvu bila ya kutarajia (burst of air), kutoka kwenye mapafu kwa kupitia njia ya pua na mdomo. Kwa kawaida chafya inasababishwa na chembechembe ndogo sana ambazo uleta aina ya muwasho kwenye pua.

Wakati mwingine chafya inaweza kusababishwa na mwanga mkali wa taa, ukikupiga usoni, au aina fulani ya virusi (mafua), chafya pia upelekea kusambaa kwa aina ya maradhi, ndio maana huwa tunashauriwa tunapotaka kupiga chafya tuzuie kwa kuweka kitambaa karibu na mdomo au kuzuiya kwa kiganja cha mkono.

Upigaji wa chafya ujumuisha misuri mbali mbali ya kwenye mwili wa binadamu, ikiwemo misuri ya tumbo, misuri ya kifua, dayaflam (diaphragm), vile vile misuri ya koo bila kusahau misuri ya kwenye macho. Ndio maana upigaji wa chafya uendana na ufungaji wa macho.

Kwa hayo machache ni matumaini kuwa utakuwa umeelewa japo kidogo, sababu za upigaji chafya.
 
NB:
Wanyama pia upiga chafya.

Last edited by a moderator:
Mkuu X-PASTER, siku hizi ili kupunguza uwezekano wa kuambukiza wanashauri kama huna kitambaa basi ukunje mkono wako wowote ule ili kukinga pua na mdomo wako ili kupunguza uwezekano wa chembechembe zinazoruka wakati wa kupiga chafya kuwafikia watu wengine na pia kama itatokea kusalimiana na mtu kwa kupeana mikono basi pia uwezekano wa kumuambukiza utakuwa ni mdogo.
 
Kupiga chafya (sternutation) ni kitendo cha utowaji wa hewa kwa nguvu bila ya kutarajia (burst of air), kutoka kwenye mapafu kwa kupitia njia ya pua na mdomo. Kwa kawaida chafya inasababishwa na chembechembe ndogo sana ambazo uleta aina ya muwasho kwenye pua.

Wakati mwingine chafya inaweza kusababishwa na mwanga mkali wa taa, ukikupiga usoni, au aina fulani ya virusi (mafua), chafya pia upelekea kusambaa kwa aina ya maradhi, ndio maana huwa tunashauriwa tunapotaka kupiga chafya tuzuie kwa kuweka kitambaa karibu na mdomo au kuzuiya kwa kiganja cha mkono.

Upigaji wa chafya ujumuisha misuri mbali mbali ya kwenye mwili wa binadamu, ikiwemo misuri ya tumbo, misuri ya kifua, dayaflam (diaphragm), vile vile misuri ya koo bila kusahau misuri ya kwenye macho. Ndio maana upigaji wa chafya uendana na ufungaji wa macho.

Kwa hayo machache ni matumaini kuwa utakuwa umeelewa japo kidogo, sababu za upigaji chafya.
asante kwa majibu yaliokwenda shule,ila kuna uvumi kwamba mgonjwa mahututi akipiga chafya basi atapona je?kuna ukweli wowote kuhusu hilo.
 
Kupiga chafya (sternutation)

Upigaji wa chafya ujumuisha misuri mbali mbali ya kwenye mwili wa binadamu, ikiwemo misuri ya tumbo, misuri ya kifua, dayaflam (diaphragm), vile vile misuri ya koo bila kusahau misuri ya kwenye macho. Ndio maana upigaji wa chafya uendana na ufungaji wa macho.

Zoezi zuri kwa misuri
 
Back
Top Bottom