KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
Kuna msemo wa kiswahili unasema baniani mbaya kiatu chake ni dawa,binafsi si mtaalam sana wa kiswahili lakini msemo huu naona unatusaidia kuyatazama mahusiano na sintofahamu za mara kwa mara baina ya katibu mkuu mdogo wa chadema bwana zitto kabwe na chama chake kinachojipambanua(kwa jina tu)kama ni chama cha DEMOKRASIA pamoja na maendeleo kiujumla.
ZITTO KABWE kabwe ni kama vile amekua akitumiwa na watu wa chadema kama condom,kwa maana hutupwa baada ya matumizi yake kuisha.Nasema hivyo kufuatia mtitiriko wa matukio mbali mbali ambayo amekua akikumbana nayo mwanasiasa huyo kijana na machachari.ZITTO mara kwa mara amekua akiibua hoja nzito zinazoihenyesha serikali toka alipoingia bungeni for the first time kiasi cha kujipatia umaarufu mwingi hasa kwa wapiga kura vijana yeye binafsi zitto kama zitto na pia chama chake mfano katika bunge lililopita zitto hapa kwa kuepuka fitna nimtaje pia bwana slaa,kwa pamoja walifanya kazi nzuri sana bungeni kila mtu anafahamu,na hivi karibuni zitto tena aliiingisha serikali ya ccm mpaka kukaribia kuiangusha kwa kutishia kumng'oa waziri mkuu madarakani,japo lengo halikutimia lakini serikali ilitikisika na kuifanya chadema izidi kupata umaarufu kupitia mgongo wa huyu huyu zitto.
Lakini tatizo linakuja pale tu zitto kama mwanasiasa ambae kazi yake inaonekana kwa alama mbalimbali na sote tunaikubali hata kimoyo moyo tu anapotaka kujaribu kuomba ridhaa ya chama chake kugombea nafasi iliyo wazi ya kukiwakilisha chama chake kwenye nafasi ya mgombea urais au kujaribu kuomba nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama kilichomkuza,kuna watu hawapendi tena sio hawapendi awe mgombea urais basi,wao hawapendi hata afikirifikirie kuomba kupewa nafasi hiyo,wanajaribu kumziba mdomo kwa kila mbinu chafu na safi,wanamuonyesha kama mwanasiasa tamaa asieambilika wala kusikia la mkuu,hali hii inakera watu wengi waumini wa demokrasia ya kweli.kwanini zitto anakua mzuri tu wakati anapofanya kazi yake ya upinzani sawasawa kwa kuihenyesha serikali lakini anapotaka kutumia haki yake tena kwa njia halali kabisa kuna watu hawapendi?kwanini chadema imekua na inataka kuendelea kumtumia zitto kujipatia umaarufu wa kisiasa lakini haitaki zitto aombe nafasi ya kushika hatamu za uongozi au kuomba kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye urais?je kinahisi hana uwezo wa kushawishi?lakini mbona wengi wamejiunga na chadema kutokana na kazi nzuri ya zitto na bwana slaa pia huko nyuma?TAFAKARI,MWISHO WA SIKU UTAGUNDUA ZITTO BANIANI MBAYA NDANI YA CDM LAKINI KIATU CHAKE DAWA!