CHADEMA yatikisa Manyoni na kuvuna wanachama

CHADEMA yatikisa Manyoni na kuvuna wanachama

MADORO

Senior Member
Joined
Nov 12, 2011
Posts
198
Reaction score
117
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, jana kimevuna wanachama wengi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Mjini Itigi, JImbo la Manyoni Magharibi. Leo Chama hicho kinatarajia kufanya mkutano mkubwa Manyoni mjini.

Mikutano hiyo inahutubiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijan a wa Mkoa huo Ndugu Josephat Isango, huku akiwaasa wananchi wa Mkoa huo kumpuuza Mkuu wa Mkoa huo kwa agizo lake alilosema wananchi wa mkoa huo wasilime mahindi.

"Limeni Mahindi wananchi, ninyi mnajua hali ya hewa ya mkoa wenu tangu zamani, mnajua udogo unavyostawisha mahindi, kauli ya mkuu wa mkoa haina tija katika maisha yetu ipuuzeni...amekuwa akiwaasa wananchi hivyo. Hata hivyo kinachoonekana kama mashindano, Mikutano ya Mkuu wa Mkoa huyo haipati watu isipokuwa watoto, ila kamanda anafunika ile mbaya.. viva CHADEMA!
 
Ahsante kwa taarifa mkuu, ukiweza pata picha, ambatanisha kwa ajili ya kumbu kumbu zetu!!
 
Isango kweli unajitahidi kutujengea heshima wana Singida, Mungu akubariki, uendelee kuwa mfuatiliaji wa Maendeleo ya Singida. Vipi Sakata la Mtoto wa Mkuu wa Mkoa kuwamwagia wananchi sumu, amehojiwa? Polisi wa Singida nao inaelekea wanamlinda mkuu huyu. Peopleeees! Safi sana kamanda. Mtujulishe na mengine yatakayojiri leo.
 
Haya sasa mapambano ya hewani atakayepata shida mwisho wa siku ni mwananchi
 
Huyo kiongozi wa CDM naona kama hanazo. Anapingana na serikali? Anapigana na rais wa mkoa?
 
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, jana kimevuna wanachama wengi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Mjini Itigi, JImbo la Manyoni Magharibi. Leo Chama hicho kinatarajia kufanya mkutano mkubwa Manyoni mjini.

Mikutano hiyo inahutubiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijan a wa Mkoa huo Ndugu Josephat Isango, huku akiwaasa wananchi wa Mkoa huo kumpuuza Mkuu wa Mkoa huo kwa agizo lake alilosema wananchi wa mkoa huo wasilime mahindi.

"Limeni Mahindi wananchi, ninyi mnajua hali ya hewa ya mkoa wenu tangu zamani, mnajua udogo unavyostawisha mahindi, kauli ya mkuu wa mkoa haina tija katika maisha yetu ipuuzeni...amekuwa akiwaasa wananchi hivyo. Hata hivyo kinachoonekana kama mashindano, Mikutano ya Mkuu wa Mkoa huyo haipati watu isipokuwa watoto, ila kamanda anafunika ile mbaya.. viva CHADEMA!

CDM msipuuze amri halali ya dola, serikali kwa kutumia wataalamu wake wameona ardhi haifai kwa mahindi, nyie mnatumia siasa pahala pasipostahili
 
Suala la msingi ni kujua kwa nini wananchi wamezuiwa na Mkuu wa mkoa kulima mahindi na baada ya hapo tujue sababu za CDM kuwaambia wananchi waendelee ili tuweze kupima na kuchangia tukiwa tuna uelewa wa nini kinaendelea.... Naomba mtoa maada atusaidie hayo kwanza kabla hatujachangia zaidi...!!
 
Wakati wa mabadiliko ukifika, hata vichanga vinajua kuwa IT IS TIME FOR CHANGE
 
Nguvu ya umma ndio mjipendekeze kwenda kunywa juice Ikulu?

IKulu sio nyumba ya baba yake Kikwete wala ya Babay yako is a Tanzania house No 1 yeyote anayetaka atakwenda ili mradi havunji sheria
 
Huyo kiongozi wa CDM naona kama hanazo. Anapingana na serikali? Anapigana na rais wa mkoa?

Me naona wewe na huyo mkuu wa mkoa ndio hamnazo,atakatazaje watu wasilime mahindi?
 
Back
Top Bottom