CHADEMA yatikisa Manyoni na kuvuna wanachama

CDM msipuuze amri halali ya dola, serikali kwa kutumia wataalamu wake wameona ardhi haifai kwa mahindi, nyie mnatumia siasa pahala pasipostahili

Kwani walianza kulima hayo mahindi baada ya kuja huyo mkuu wa mkoa au ni desturi yao kulima mahindi kwa miaka mingi? Hao wataalamu hawakuwepo huko nyuma mahindi yakilimwa? Wenyeji ndio wanajua wanachokitaka, mkuu wa mkoa ni nani hadi si-impose matakwa yake ya kilevi kwao?
 
CDM msipuuze amri halali ya dola, serikali kwa kutumia wataalamu wake wameona ardhi haifai kwa mahindi, nyie mnatumia siasa pahala pasipostahili

Wataalam wepi hao unaowazungumzia?hebu tanabaisha basi hao wataaam unaowaamini.
 
Nadhani imefika wakati wakuu wa mikoa watoke kwenye mikoa yao (walipo zaliwa) ili wazijue asili ya mazao yalimwayo,icje kuwa yeye kwao wanalima Ndizi/Mhogo akaona Mahindi c dili... BIG UP CDM ....Sana tu..
 
Kama wananchi walikuwa wanalima mahindi toka zamani sioni haja ya mtu mmoja kutumia mgongo wa serikali kuwakataza watu kufanaya shughuli halali za kujiletea chakula na maendeleo,kuna watu wanadhani serikali ni kama kikundi fulani bila kujua kuwa serikali ni wananchi wenyewe ambao wana uwezo wa kuamua lolote,mifano tunayo na wenye serikali huwa wakiamua jambo hakuna wa kujifanya ana amri ya serikali kuwazuia.
Tuamke na tuache tabia ya kukumbatia mambo ambayo si ya msingi kwa maendeleo ya taifa letu.
 
nyie wanyampaa mnawapotosha wananchi kwa kung'ang'ania kulima mahindi af baada ya muda mnalia njaa,shauri yenu hamtapata msaada kama hamjafa wote.huyo isango muongo tu hana lolote na wala manyoni hakuna mtu atakayedanganyika aende upinzani.
 
lengo la mkuu wa mkoa ni kuwasaidia nyie na wananchi wengine wa singida mlime mazao yanayostahimili ukame,sasa kwa ubishi wenu wa kutaka sifa mnawadanganya,hamna kazi za kufanya?mwahari waa
 
Kinachonifurahisha sio kuenea kwa CDM bali ni elimu kwa watu ambao hawajawahi kuipata tangu uhuru. Ujinga wa Wadanganyika umekuwa mtaji wa Magamba tangu uhuru. Tunahitaji elimu ili watu wajitambue na kudai haki zao kutoka kwa WATAWALA.

Na hapa ninaposema WATAWALA sina maana ya Magamba peke yao, na wote watakaofuatia baada ya iwe CUF, NCCR or CDM, tunahitaji uwajibikaji kwa wananchi.
 
Nadhani imefika wakati wakuu wa mikoa watoke kwenye mikoa yao (walipo zaliwa) ili wazijue asili ya mazao yalimwayo,icje kuwa yeye kwao wanalima Ndizi/Mhogo akaona Mahindi c dili... BIG UP CDM ....Sana tu..

katiba mpya ni either hawa jamaa wasiwepo au watoke sehemu husika. Kuna mkuu wa wilaya makete nimesikia analazimisha kila familia iwe na ekari mbili za pareto. Mi najiuliza,hii nchi kuna wilaya nyingi zina njaa aafu wewe unasisitiza watu walime zao lisilo na soko,una akili kweli?
 
Safi sana makamanda tupo pamoja katika mapambano ya kumng'oa mkoloni mweusi madarakani CCM
 
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, jana kimevuna wanachama wengi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Mjini Itigi, JImbo la Manyoni Magharibi. Leo Chama hicho kinatarajia kufanya mkutano mkubwa Manyoni mjini.

Mikutano hiyo inahutubiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijan a wa Mkoa huo Ndugu Josephat Isango, huku akiwaasa wananchi wa Mkoa huo kumpuuza Mkuu wa Mkoa huo kwa agizo lake alilosema wananchi wa mkoa huo wasilime mahindi.

"Limeni Mahindi wananchi, ninyi mnajua hali ya hewa ya mkoa wenu tangu zamani, mnajua udogo unavyostawisha mahindi, kauli ya mkuu wa mkoa haina tija katika maisha yetu ipuuzeni...amekuwa akiwaasa wananchi hivyo. Hata hivyo kinachoonekana kama mashindano, Mikutano ya Mkuu wa Mkoa huyo haipati watu isipokuwa watoto, ila kamanda anafunika ile mbaya.. viva CHADEMA!

Hii taarifa ni ya kisiasa na si ya kitendaji, wanachama wengi waliovunwa ni wangapi? tusiige utoaji taarifa wa kimagambagamba hautasaidia kuijenga CDM
 
Huyo mkuu wa mkoa naona kama hanazo. Anapingana na kiongozi wa CDM? Anapigana na nguvu ya umma?

Huyo Mkuu wa mkoa Si Ndo alipewa onyo na 'mtoto wa mkulima' ili awaombe msamaha wanasingida juzi juzi tu ?
 
Kilio changu ni kuwaona hawa makamanda wakija Mtwara na Lindi. Njooni tunawahitaji kwa nguvu sana. CCM imechemka huku kwanza kuna ugomvi wa korosho Za wananchi hazinunuliwi na wahindi.
 
Teh!Hadi Chikuyu,Chibumagwa,Kintinku na Maweni kwa Chiligati!

Naamini tafsiri ya nchi kutotawalika imeanza kusomeka, kiongozi anatoa agizo ambalo halitekelezeki, anapanda jukwaani mwenyenchi na kuwaambia wenyenchi wenzake kinachopaswa kufanywa, na wanakubaliana, kwa staili hii hapo kuna kutawala tena!!!! msisahau kufika saranda, ilalo, hika, msemembo, londoni, majirii, rungwa, mkwese, mitoo, agondi, sukamahela, sasajila ...........!!!!
 
Back
Top Bottom