CHADEMA yatangaza kumtambua Meya Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yatangaza kumtambua Meya Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by nngu007, Jun 21, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Monday, 20 June 2011 19:22 newsroom


  NA SHAABAN MDOE, ARUSHA
  SAKATA la Meya wa Jiji la Arusha, limefikia tamati baada ya CHADEMA kutangaza kumtambua rasmi Meya wa Jiji hilo, Gaudance Lyimo (CCM). Awali, CHADEMA wakiongozwa na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), waligoma kumtambua Lyimo licha ya kuchaguliwa na kikao halali. Katika kuhalalisha kutomtambua huko, CHADEMA walifanya maandamano makubwa kinyume cha sheria, ambayo yalisababisha mauaji ya watu kadhaa na wengine kujeruhiwa. Akizungumza mara baada ya kikao cha Baraza Maalumu lililofanyika jana kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji, Mwenyekiti wa kikao, Michael Kivuyo, alisema mwafaka juu ya suala hilo umepatikana. Kivuyo, ambaye ni Diwani wa Kata ya Sokoni One (TLP), imeridhiwa Lyimo kuwa Meya wa Jiji kwa kipindi cha miaka mitano, huku nafasi ya Naibu Meya ikishikwa na CHADEMA kwa miaka mitatu na mwaka mmoja utakuwa chini ya TLP.
  Alisema kuwa katika kikao hicho, ilikubaliwa kufanyika kwa uchaguzi wa Naibu Meya, ambapo Diwani wa Kimandolu Estomii Mallah (CHADEMA), alichaguliwa kwa kura 21 kati ya 25, huku tatu zikiharibika na moja kumkataa.
  Katika makubaliano, Mallah ataanza kushika madaraka hayo kwa miaka mitatu na baadaye Kivuyo atahitimisha kwa kumalizia muda uliobaki. Kivuyo ndiye diwani pekee wa TLP.
  “Unajua hali ilikuwa mbaya na wananchi walikuwa wakitushangaa, huku wakihoji walituchagua kuwa madiwani si meya, sasa tumeelewana ili kuweka mambo sawa,” alisema.
  Alisema hatua inayofuata sasa ni kwa madiwani na watendaji wote kufanya kazi, kwani ndani ya halmashauri hiyo kuna ubadhirifu mkubwa unaofanywa na watendaji wasio waaminifu.
  Pia, alisema madiwani walifanya uchaguzi wa nafasi za kamati tatu zikiwemo za Elimu, Afya na Uchumi, ambayo itaongozwa na Diwani wa Kata ya Elerai John Bayo (CHADEMA).
  Kamati ya Mipango Miji ya Ujenzi na Mazingira, itaongozwa na Diwani wa Olasiti, Ismail Katamboi (CCM).
  Nyingine ni Fedha ambayo inakuwa chini ya Meya wa Jiji, Lyimo na Katibu wake anakuwa Naibu Meya, Mallah, huku wajumbe wake wakiwa ni Bayo, Katamboi, Alphonce Mawazo, Mary Kisaka, Reuben Ngowi na Michael Kivuyo.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,983
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  POLITICS IS THE GAME OF DIRTY PEOPLE....! People died bse of this....the same to ZANZIBAR....!
  Wakishapata madaraka kimyaaaaaaaaaaaaaaaa........PIPOOOOOOOOZZZZZZZZZZZZZZZ
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,184
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kama kweli "imetangaza" basi weka tangazo tulione.
   
 4. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu habari hiyo ni ya ukweli sana tu sio uongo wamekubali kwa misingi ambaya bado hata mimi sijawaelewa
  nadhani ni funika kombe hii
  lakini bora kuna wawakilishi wapambanaji kwenye hiyo kitu hakuna madhambi kufanyika kijinga
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Magamba wameengeza mke wa tatu?
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tee hee hee navunja mbavu kwa kauli za Magwada eti hakuna Dhambi kufanyika kijinga. Sasa ni nani mjinga kati yao, Magamba au magwanda? Nyie ni watani wa jadi tusonge mbele!
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,128
  Likes Received: 21,933
  Trophy Points: 280
  Kikowapi?

  Siku nyingine msidanganywe kwenda kufa bure.
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,983
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  wakati CUF wanaandamana ili kupata public support watu walitiwa vilema na wengine kupoteza maisha hadithi ikafika mwisho wake......WALIOPATA VILEMA BADO NI VILEMA...WALIOFIWA NA NDUGU ZAO MAPENGO BADO HAYAJAZIBIKA.........zamu yao ikapita....... wengine wakafuata na hadithi bado ni ile ile!
  MWEREVU HUJIFUNZA KWA MAKOSA YA WENGINE
   
 9. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hawa wanyarwanda nao kazi tunayo ndio tatizo la nchi yenye wakimbizi
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,983
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  NILIMWONA REV. MASA HAPA.....VIPI KAPITA KIMYAKIMYA?.....! credibilty ya vyama vya misimu utaijua tu
   
 11. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nafikiri Wanyarwanda ni nyie mnaotangaza umwagaji wa damu kila siku, au labda mnawaonea kijicho ndugu zenu kwani damu haisemi uongo.
  Kuwa na aibu kidogo mtu akivuliwa nguo huchuchama. Kwani nani anaekuamulieni misimamo halafu mnakuja kuibadilisha na nkikumbushwa nongwa.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,164
  Likes Received: 782
  Trophy Points: 280
  Rekebisha statement yako iwe hivi: "Siku nyingine msikubali kutupinga, tutawaua tena mpaka mkubaliane nasi"
   
 13. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,184
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  It seems to me that a mistake has been made. CDM should have continued to insist on a mayoral re-election. A principle is a principle.

  What happens to the stands taken by Archbishop Lebulu and the KKKT Bishop of Arusha? Recall that they too refused to recognize the Mayor on the grounds that he was not democratically elected.

  By compromising on a matter of principle, CDM may have let down a lot of people. It is not a good day for CDM.

   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 145
  if this is true, then your point is very valid

  CHADEMA WAMECHEMKA KWENYE HILI
   
 15. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Habari yenyewe imejichanganya kama walishakubaliana kupeana madaraka kwa awamu ya nini kumchagua naibu meya kwa kura.ilikuwa ni kiasi cha kumteua mtu na meya amepata kura ngapi tafadhali.
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,184
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kama CDM ingekuwa imekubaliana na CCM wakapiga kura mpya ya Meya na Gaudence Lymo akashinda, basi hakungekuweko na tatizo la kimsingi. Maana kuna swala la msimamo hapa. Msimamo wa CDM ambao uliungwa mkono na wengi, ikiwa ni pamoja na Maaskofu wa Arusha, ulikuwa ni kwamba uchaguzi wa Meya urudiwe.

  Dr. Slaa alishirikishwa kweli kwenye kitu hiki? Yeye ni makini mno kuweza kukosea kiasi hiki.
   
 17. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CDM inazidi kuonekana kuwa hawana principle wanayoshikilia bali ni bla bla bla tu za vijiweni!
  Jana wametangaza kutaka kuungana na wenzao wa upinzani........kitu ambacho walikipinga kwa kejeli nyingi!
  Leo mayor wa Arusha wame-concede............kwa nini mmepoteza muda na maisha ya watu?
  Pia kuna kesi juu yenu juu ya hili................

  Hii ni first class comedy!
   
 18. n

  nyantella JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kwani nani zaidi kati ya Mbowe na Slaa? kama Mbowe kakubali basi lazima kuna sababu!! sometimes you have loose in order to gain!
   
 19. mwakichi

  mwakichi JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: May 14, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  hongere CDM kwa maamuz magum lkn yenye manufaa kwa wakaz wa arusha..!!!
   
Loading...