Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 57,199
- 46,628
- Thread starter
- #41
Inaonekana kuna mijitu humu ndani hata haijui maana ya NGUVU YA UMMA,the PEOPLES' POWER.
- Nguvu ya Umma ni Wananchi kwa ujumla wao KUKATAA kutawaliwa kimabavu na SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI kwa kipindi hicho. Kama ilivyo sasa kwa CCM hapa Tanzania.
- Nguvu ya Umma lazima iwe na uongozi au chanzo utakaochochea hiyo nguvu, haijalishi ni mtu mmoja,kikundi fulani au Chama cha Siasa ambacho haikubaliani na Serikali iliyoko Madarakani.
Tukumbushane vuguvugu lililoanzia Ulimwengu wa Kiarabu. ALGERIA ndiyo iliyowasha moto wa mageuzi ya Nguvu ya Umma. Kijana tu muuza mboga za majani alianzisha huo moto na ukaenea nchi zote za Kiarabu. Just a single man,was able to turn around the mind set of the people. Nguvu ya Umma ilianzia hapo.
Kule kwa marehemu Ghadaffi ilikuwa ni Baraza Taifa la Mpito, The National Transition Council-NTC, hiki kilikuwa ni kikundi cha watu waliokuwa wakipinga sera za Ghadaffi. Kule Misri ni watu walikusanyika Tahrir Square na wakalianzisha. Tunapozungumza watawala wote hao katika nchi hizo leo ni historia.
Hapa kwetu Tanzania kwa sasa CHADEMA ndiyo chenye mawazo ya kuleta mabadiliko au mageuzi kwa Taifa letu baada ya miaka 50 isiyo na tija. CCM wameng'ang'ania Ikulu ilhali nchi inazidi kudorora KISIASA na KIUCHUMI. Mifano michache tu ni maandamano ya baada ya Uchaguzi Mkuu 2010 katika miji ya Arusha,Mwanza,Mara na Mbeya kwa uchache. Hizo zote ni ishara za Nguvu ya Umma inayofukuta chini kwa chini hapa Tanzania. Na kama hali za Watanzania zitaendelea kuwa mbaya na Serikali kuendelea kuwapuuza Watanzania basi believe me THE PEOPLES POWER MUST TAKE ITS COURSE VERY SOON!!!
Makoye,
Umeandika maneno mengi lakini hakuna cha maana ulichoandika zaidi ya kujichanganya mwenyewe nakujibu machache tu.
Kwanza hizo nchi ulizozitaja zilifanya nguvu ya umma waliofanya ni wananchi sio chama cha siasa, hakuna chama hata kimoja duniani kimeongoza kufanya mapinduzi kupitia nguvu ya umma..
Chadema hawawezi kuwa na nguvu ya umma, bali wana nguvu ya kikundi kinachojaribu kutikisa nguvu ya umma iliyopo..
Chadema wangekuwa na nguvu ya umma wasingepata wabunge 23 Tanzania nzima..
Chadema ni kikundi cha watu kama NGO tu, hawawezi kuwaunganisha watanzania wote