CHADEMA yataka Tanganyika irudishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yataka Tanganyika irudishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Dec 11, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na Edward Kinabo


  [​IMG]
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka serikali kuitikia wito wa kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala, ikiwa ni pamoja na kuufanyia marekebisho muundo wa sasa wa muungano ili kuirudisha nchi ya Tanganyika iliyopata uhuru wake mwaka 1961.
  Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kinondoni, John Mnyika, wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana wa chama hicho, lililoandaliwa mahususi kutathmini miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika.
  “Nashangaa tunaposherehekea uhuru wa nchi ambayo haipo. Kimsingi uhuru tunaousherehekea wa miaka 48 ni uhuru wa nchi iitwayo Tanganyika, kwani ndiyo iliyopata uhuru mwaka 1961.
  “Lakini Tanganyika kikatiba haipo, nchi zilizopo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Zanzibar ipo lakini Tanganyika iliyoungana nayo haipo, tunasisitiza tena wito wetu wa kuitaka serikali kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala, ikiwa ni pamoja na kuufanyia marekebisho muundo wa muungano utakaoirejesha Tanganyika.” alisema Mnyika.
  Alisema wakati Tanganyika ikiadhimisha miaka 48 ya uhuru wake, bado haijafanikiwa kupambana na maadui wanne; ambao ni ujinga, umaskini, maradhi na rushwa.
  “Ujinga bado upo, serikali inajenga sekondari za kata zisizokuwa na walimu wala vifaa vya kutosha kuondoa ujinga. “Maradhi yapo, leo hapa Wilaya ya Kinondoni tu tunakabiliwa na kipindupindu na mama wajawazito wanaendelea kupoteza maisha yao pale Hospitali ya Mwananyamala.
  “Umaskini upo, kwa mfano wakati wa Mwalimu, pato la Mtanzania lilikuwa dola mbili kwa siku (takriban sh 2,000 kwa siku), leo pato la Mtanzania ni chini ya dola moja kwa siku (chini ya sh 1,000 kwa siku). Rushwa ya kawaida iliyokuwapo wakati wa Mwalimu, sasa imeota mizizi na kuwa ufisadi unaotamalaki ndani ya mfumo mzima wa uongozi,” alisema Mnyika.
  Alisema wakati Tanganyika ikiadhimisha miaka 48 ya uhuru wake, hali halisi inaonyesha kuwa taifa hilo ambalo halipo kikatiba, linakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tishio la kuvunjika kwa amani na umoja uliojengwa na waasisi wake.
  “Waasisi walijenga amani na umoja. Leo mijadala ya kidini imekithiri na inazidi kufufua hisia za ubaguzi wa kidini kati ya waumini wa dini moja na nyingine. Leo pengo la kiuchumi kati ya matajiri na maskini linazidi. Migogoro ya kirasilimali nayo inazidi.
  “Tumeshuhudia mapigano kati ya wakulima na wafugaji kugombania rasilimali ya ardhi. Tumeshuhudia Watanzania wakiondolewa bila taratibu katika ardhi yao kupisha wawekezaji, mfano kule Loliondo na kwenye maeneo yenye madini. Chaguzi zetu pia zimekuwa za hatari, tumeona ya Zanzibar na tumesikia na kushuhudia umwagaji damu katika chaguzi ndogo za ubunge kwenye majimbo ya Tarime, Kiteto, Busanda na Biharamulo. Haya yote ni tishio kwa amani na umoja wa taifa letu,” alisema Mnyika. Alitoa wito kwa Rais Kikwete kukubali kufanya maamuzi magumu ya kulinusuru taifa kama ilivyopendekezwa katika maazimio ya kongamano la Mwalimu Nyerere na yale yaliyotolewa katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichomalizika hivi karibuni. Katika kongamano hilo, Mnyika alizindua tuzo kwa vijana ya uhuru wa kweli ya Freeman Mbowe ‘Freeman Mbowe Youth Real Freedom Award’, itakayokuwa inatolewa kila ifikapo Desemba 9 ya kila mwaka, kwa vijana wa umri wa miaka 18 hadi 35, watakaokuwa wanashinda mashindano ya uandishi wa hotuba kuhusu uhuru wa Tanganyika, yatakayokuwa yanaandaliwa na uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni.
   
 2. O

  Omega.Omega Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa tu.
  Hakuna la maana hata tanganyika ikirudishwa.
  Ufisadi ni ule ule.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mwisho wataomba na mangi wao arudishwe... wamefulia hao na kugombana kama wake wenza!!!
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hii ni sera ya CUF kuwepo kwa serikali tatu tangu mwanzo..kama chadema wanafikiri the same...then hakuna sababu ya kutoungana
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,790
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  ..idea ya kurudisha serikali ya Tanganyika bila kuuvunja muungano sikubaliano nayo.

  ..ningependelea CUF na CHADEMA waende hatua moja mbele kwa kupendekeza MUUNGANO UVUNJWE.
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Swali. Je swala la Tanganyika kurudishwa lipo kwenye sera rasmi za Chadema?
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Muungano uvunjwe? mzima kweli wewe?

  Kuna matatizo kwenye muungano lakini kama vile nimeshazoea kuishi Tanzania

  Nafikiri wanatakiwa waende mbele zaidi kuwe na serikali moja yenye nguvu na heshima..vunja mabunge mengi yasiyo na maana na kufaidi synergies mbalimbali za ku-merge
   
 8. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Haya ni mawazo ya Mnyika au msimamo wa Chadema?.
   
 9. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kwa nini Zanzibar bado ipo hata baada ya muungano na Tanganyika haipo, Je kungekuwa na serikali tatu(serikali ya Tanganyika, Serikari ya Zanzibar na Serikali ya Muungano) toka enzi ya muungano ingekuwaje, Julius angechagua kuwa rais wa Tanganyika au rais wa Muungano, kuna mchezo mkali sana hapa..sugueni vichwa mtanielewa tuu.
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tumain,
  Kwa muungano tupo pamoja kabisa.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,790
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  Tumain,

  ..I am serious kwamba Muungano uvunjwe.

  ..Wazanzibari hawataki kuacha utaifa wao na kujiunga na wenzao wa Tanganyika kuunda nchi moja, yenye serikali moja, Tanzania.

  ..bado kutakuwa na uwezekano kwa Watanganyika na Wazanzibari kushirikiana kwa namna mbalimbali kama majirani. kwa msingi huo you wont miss that much "Utanzania" wako.
   
 12. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Sometimes you speak points
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Mwungano uvunjwe ili iweje? Una hakika gani kuwa ukivunjwa Tumain hatamiss Utanzania wake? Kwanza mkiuvunja kutakuwepo uhasama na sidhani utakubali kumwona Tumain akiwa na Utanzania. Mtawaambia rudini kwenu Zanzibar na hamtaishia hapo. Mtawafukuza Wapemba na dhambi hiyo ikianza kuwatafuna hamtaishia hapo. Baadaye mtaanza kujiangalia ni nani Mtanganyika halisi na sisi ambao tunaunga mwungano mtatujengea zengwe.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,790
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..Wazanzibari hawautaki huu Muungano. they simply do not want to be identified as Tanzanians. sasa ya nini kuwalazimisha?

  ..Watanganyika kule vijijini hawana habari nao kabisaaa.

  ..vurugu zitatokea kama tutaendelea kungangania huu Muungano mpaka Wazenj watakapoamua kufanya vurugu na maasi. sasa kabla hawajafika huko bora tuwarudishie mamlaka kamili ya nchi yao.

  ..kuna taratibu zinazopaswa kufanyika ktk kuvunja muungano huu. tunaweza kutafuta msaada na ushauri on how to proceed.

  ..tunapaswa kuzingatia hayo hapo juu ili kuondoa uwezekano wa kutoa vurugu na uhasama unaouzungumzia.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu. Inategemea itakavyofanyika. Tuige kutoka kwa former Czechoslovakia na si Yugoslavia! Mimi naamini kuna haja ya kufanya referendum ya kweli na wazi kuhusu huu Muungano na kama wengi katika kila upande wakitaka uendelee, uendelee. Moja ya upande ukikataa uendelee, basi tupeana talaka na kila mmoja achukue zake hamsini. Tunahitaji legitimacy ili hao ambao kila siku wanawabeza watanganyika kuwa wanalazimisha muungano wasiwe na la kufanya. Hatuwezi kuendelea hivi tulivyo.

  BTW, mimi nilidhani mambo yatakuwa vice versa? Wazanzibari hawafichi kuwa hawataki watanganyika nchini kwao wakati sijasikia mtanganyika akisema kuwa wafunge virago. nadhani kitakachotokea ni wale wenye asili ya bara walio Zanzibar watafukuzwa na wale wazanzibari walio bara watapewa chaguo la uraia. Wakitaka utanganyika watakubalika na wasipotaka basi aidha wabaki kwa residency permit au waondoke waende kwengine wanakotaka ( si lazima Zanzibar)!

  Amandla.........
   
 16. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  chadema QWAKO DISORGANISED, KILA MTU ANASMEA LAKE. KESHO UTAMSIKIA DR SLAA NAE ANAKUJA NA LAKE.
   
 17. C

  Chuma JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Huku ni kumfukua Mwalim Nyerere...!!!

  Chadema nafikiri huu mtizamo wenu juu ya Muungano usiwe wa kificho uwe wa Wazi. Isije akatokea Kiongozi Mwingine akasema ule ulikuwa msimamo wa Mnyika na si Chadema.

  Wakati Wenzetu wa Europe wanafikiria kuungana ili kuwa na Power kama US, sisi twafikiria tofauti. Sie tumeungana lkn bado twafikiria Kunyonyana.
   
 18. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  CHADEMA oyee....mie kama mzenji sitaki muungano kabisa, kama kulazimishwa basi ziwe hizo tatu...but I prefer the first one!!!

  Sitaki mapaspoti ya kijani kibichi!!!:rolleyes:
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wengi bado wanahitaji Muungano... tena kwa nia ya kuwa na muungano bora zaidi kuliko huu!
   
 20. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #20
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Katika kusugua vichwa, haya ni miongoni mwa maswali ya kujiuliza;
  Serikali ni nini?
  Tanganyika ni nini?
   
Loading...