"CHADEMA yasubiriwa kwa hamu visiwani Pemba"

Akili za memberz wengi humu ni kama maisha ya funza. Fupi mno kujiita great thinkers. Hivi, mna log in kujibishana na ritz? Au nanyi mnataka umaarufu humu? Mnaboa kupitiliza.
Back to topic, huu ni wakati wa cdm kujiimarisha visiwani ili kupata mwonekano wa kitaifa zaidi. Ni wakati wa kuwa CHAMA HALISI kikuu cha upinzani nchini, kwa sura ya utaifa.
Ni kweli sana kuwa kwa sasa wazanzibari ndio wako kwenye uhitaji mkubwa kuliko wakati mwingine wowote, wa kuwa na chama cha upinzani cha kweli kitakacho simama upande wao siku zote.
 
Nashukuru Mungu huko visiwani wameelewa ndoa hii ya ccm na cuf kwamba haina manufaa wala tija kwao.
 
Toa ujinga wako hapa..NATO ni majeshi ya Wakristo wakishirikiana na wanafiki period
Mimi na wewe nani mjinga? NTC ndo wamemuua Gadafi, hao jamaa wanaswali swala tano na mtutu wa Bunduki mkononi kisa wamtoe Gadafi madarakani,NATO wako pale kulinda raia.
 
Toa ujinga wako hapa..NATO ni majeshi ya Wakristo wakishirikiana na wanafiki period
Acha kutokuwa na kumbukumbu kama umesahau uliza, kabla hata NATO hawajatia miguu wale walibya waliokuwa wanaandamana kudai reforms hukuwaona/kuwasikia? Gaddafi alipokuwa anawaua wewe ulifurahia?
Tujadili kwa kujenga sio kuwabiased hatutafika kwa mtindo huo!!!!
 
Hahhahahahahahahah, tunawasubiri CHADEMA pemba. Wapemba ni ndondondo, hahhahahahahahahahah. Mukija muje na mipesa maana sisi tunashida ya mipesa vinginevo hapa hamuna chenu. Mipesa baba ndio tunayotaka. siasa tunazijua zamani.
 
Inapendeza na itajenga wigo mpana kwa Chadema na itakuwa safi sana na kheri kwa wapemba na wa unguja, sera ya Chadema sio kuitenga Zanzibar ila ni kuifanya Zanzibar iweze kujiendesha ki uchumi kama jimbo na sio Zanzibar tu! kutakuwa na majimbo makubwa matano ya kiuchumi Tanzania bara, mfano watu wa kanda ya ziwa wanatakiwa wajue na wanufaike na kila natural resource inayopatikana pale ( Ziwa Victoria, Dhahabu, Almas utalii nk,)

vivyo hivyo kwa kanda zingine na hii itasaidia uwajibikaji wa moja kwa moja na kila sehemu watu watakuwa bize nchi itashamiri na uchumi utakuwa tofauti na sasa serikali inategemea sana kodi ya PAYE kwa waajiri, Sigara na Pombe ili kujiendesha huku migodi ikiwa haina tija kwa eneo husika na kwa Taifa, lazima tuamke Chadema twendeni Zanzibar ila tukafanye siasa za kistaarab, tushike hatamu salama,. Uwezo tunao, Utajiri tunao tuamke watanzania tuweke umoja tusiwatenge Wazanzibar labda watake wao kujitenga ila tuwape nafasi waijenge nchi watoe mchango katika Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
Hivi kweli mpemba anaweza kukubali kuingia Kanisani?
Chagua jibu sahihi katika swali lifuatalo (20 marks)

Wewe (ritz) ni ..........................
A . Mdini kwa asili
B . Mbaguzi wa kikanda kwa asili
C. Huwezi kuishi na jamii nyingine tofauti na yako [ ]
D. Mkabila kwa asili
E. Yote hapo juu
 
Makamanda kiualisia sasa ni muda muafaka kwa cdm kujitambulisga vema zenji na kuizzika cuf kabisa maana tumebaki na kazi mbili tu zenji na vijijini baada ya hapo mhe slaa tutajusindikiza pale magogoni.ukifika futa vumbi yote katika vioo inayosababisha viongozi wa ccm husiwaone wana nchi wake kila la khe;i cdm mnapo weka mikakati ya kuvuka maji
 
WanaJF,
Nimerudi bongo. Ukweli nimefurahia kukutana na wapemba wale na kujadili nao kwa uwazi sana siasa za taifa letu. Nilijitahidi nisiegemee kwenye chama chochote ili niweze kupata mtazamo wao. Kwa kifupi kama nilivyoeleza mwanzo; wanatamani chama kitakachotetea maslahi ya wanyonge. Nautakia uongozi wa CHADEMA maamuzi mema
 
cuf ndanii ya ndoa na bwana wao,wanasikia mapenzi yamenoga wapemba na waunguja munmeunmiammhamna jipya zaidi kudhoofisha democrasia huhko bara,hamieni cdm,,limbwwata la ccmm dhidi ya caf limenoga mmmsitegemee jipya kkutoka kwa hao magamba
 
hii si inbox ya chadema!! Peleka ushauri wako ofisini kwao au kwenye facebook yao!!!

niko mjini wete kwa shughuli za kikazi kwa siku tatu sasa. Nimepata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti kuzungumzia upepo wa kisiasa. Wakiwemo vijana, wazee, na wafanyabiashara. Suala la kuzama kwa meli linaonekana kugusa hisia zao kisiasa.

Wapemba wengi wanausikitikia mwafaka na wanasema umewamaliza kwa vile sasa hakuna upinzani. Mfano wanaoutolea ni suala la kuzama kwa meli ya spice. Wanasema, suala kama hilo ambalo limeondosha watu takribani 4000 katika kisiwa cha watu takribani 400,000 ni sawa na 1% ya wakazi lilipaswa kuwa moto sana lakini sasa sawa na kama waliokufa ni sisimizi tu. Wengi wamesema - "tunasubiri chama mbadala".

nilipomhoji aliyekuwa mmojawapo wa wagombea ubunge wa cuf aliyebwagwa kimizengwe kwenye kura za maoni, alisema yeye yuko tayari kuingia chama chochote mbadala. "niko tayari kwenda chama chochote mbadala. Napima upepo tu". Nilipomhoji juu ya mtazamo wake kuhusu chadema kama chama mbadala, alisema: "tumekuwa tukilijadili hilo na wenzangu hata wengine waliokuwa wakigombea uwakilishi na tunatambua uimara wa chadema hasa katika kusimamia mambo ya kitaifa. Kina viongozi madhubuti na wenye upeo mkubwa kama dr. Slaa na wengine. Kama kitakuja kujitambulisha vema huku, tutatafakari mwelekeo wakati huko. Sisi hatukuzaliwa na cuf".

pendekezo: naomba viongozi wa kitaifa wa chadema wapange namna gani ya kutumia vaccum hii iliyotengenezwa na cuf, ili kuwa chama mbadala katika visiwa hivi viwili.
 
Great thinkers wa humu JF siwawezi utadhani wanapitia kozi ya matusi kabla ya kuwa member,taratibu jamani busara na hekima mbele
 
Kwani wapemba wana tabia gani?(Ritz),mimi nimekaa pemba tena Wete sasa ni mwaka 3,kama ni kanisani tunaenda kama kawaida kwani makanisa yapoa na yana wahumini.
Wapemba ni wagumu ktk dini ila ni wpesi kuchange ktk siasa.its true kwamba yale waliyoyatarajia kwa Seif hawajayaona apart from kupanda kwa bei ya karafuu,ila maisha yao yamekuwa magumu zaidi.kama cdm itaingia Pemba muda huu ni rahisi sana kuwachange from cuf to cdm.
Msiponde wapemba kwa maneno ya mitaani njoo uhakikishe nini kipo pemba.
 
Back
Top Bottom