"CHADEMA yasubiriwa kwa hamu visiwani Pemba"

Maishamapya

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,279
375
Niko mjini Wete kwa shughuli za kikazi kwa siku tatu sasa. Nimepata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti kuzungumzia upepo wa kisiasa. Wakiwemo vijana, wazee, na wafanyabiashara. Suala la kuzama kwa meli linaonekana kugusa hisia zao kisiasa.

Wapemba wengi wanausikitikia mwafaka na wanasema umewamaliza kwa vile sasa hakuna upinzani. Mfano wanaoutolea ni suala la kuzama kwa meli ya spice. Wanasema, suala kama hilo ambalo limeondosha watu takribani 4000 katika kisiwa cha watu takribani 400,000 ni sawa na 1% ya wakazi lilipaswa kuwa moto sana lakini sasa sawa na kama waliokufa ni sisimizi tu. Wengi wamesema - "Tunasubiri chama mbadala".

Nilipomhoji aliyekuwa mmojawapo wa wagombea ubunge wa CUF aliyebwagwa kimizengwe kwenye kura za maoni, alisema yeye yuko tayari kuingia chama chochote mbadala. "Niko tayari kwenda chama chochote mbadala. Napima upepo tu". Nilipomhoji juu ya mtazamo wake kuhusu CHADEMA kama chama mbadala, alisema: "Tumekuwa tukilijadili hilo na wenzangu hata wengine waliokuwa wakigombea uwakilishi na tunatambua uimara wa CHADEMA hasa katika kusimamia mambo ya kitaifa. Kina viongozi madhubuti na wenye upeo mkubwa kama Dr. Slaa na wengine. Kama kitakuja kujitambulisha vema huku, tutatafakari mwelekeo wakati huko. Sisi hatukuzaliwa na CUF".

PENDEKEZO: Naomba viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wapange namna gani ya kutumia vaccum hii iliyotengenezwa na CUF, ili kuwa chama mbadala katika visiwa hivi viwili.
 
Natumaini wakuu wa CHADEMA wameipata hiyo na bila shaka wataifanyia kazi ipasavyo, mkuu.
 
Hivi kweli mpemba anaweza kukubali kuingia Kanisani?
 
Nashukuru sana kwa upeo wako wa hali ya juu!
Naamini uongozi wa chama chetu umeliona hili.
 
Chadema waende kufanya nini huko nchi za nje! Kama ni hivyo basi waende pia na Kenya.

Kwa sasa Tanzania ni moja. CHADEMA katika sera yao juu ya muungano wanazungumzia serikali tatu katika Taifa moja. Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano (TANZANIA). Wapemba wanachosema, CHADEMA imeonyesha kufanya kazi njema katika kutetea maslahi ya kitaifa. Visiwa vya Pemba na Unguja (Zanzibar) ni sehemu ya Taifa la Tanzania ambalo linaihusisha Tanganyika pia.
 
Chadema waende kufanya nini huko nchi za nje! Kama ni hivyo basi waende pia na Kenya.

yap! Sikujua kumbe kuna Watu wanaelewa. Zanzibar ni nje ya nchi, vyama walivyonavyo haviwatoshi?? Eti meli, sasa ikizama ndo iweje? Ndio maana sie tuliendelea na mashindano ya u miss kama kawa, kwani kuna mamiss wanatoka zanzibar katika miss Tanzania?
 
CDM ni chama cha siasa. Hakina udini. Tatizo lako wewe udini wa magamba unakusumbua. Na siku magamba wakianguka hakuna wa kukupokea wewe. Kwa sababu sumu unayotaka kuipandikiza kwa watu ni mbaya kuliko unavyodhani. Fikiri kabla ya kupost.

Mkuu nzitunga, huyo jamaa sijui anafaidika na nini kuongelea udini dini kila siku! Jamaa anafanya vitu ambavyo mtu wa kawaida ni vigumu sana, lazima atakuwa ana sense of humanity and he must be feeling so sad for every post. Katika dunia ya leo, udini hautufikishi sehemu yeyote zaidi ya kuigawa jamii kwa manufaa ya wachache.
 
Niko mjini Wete kwa shughuli za kikazi kwa siku tatu sasa. Nimepata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti kuzungumzia upepo wa kisiasa. Wakiwemo vijana, wazee, na wafanyabiashara. Suala la kuzama kwa meli linaonekana kugusa hisia zao kisiasa.

Wapemba wengi wanausikitikia mwafaka na wanasema umewamaliza kwa vile sasa hakuna upinzani. Mfano wanaoutolea ni suala la kuzama kwa meli ya spice. Wanasema, suala kama hilo ambalo limeondosha watu takribani 4000 katika kisiwa cha watu takribani 400,000 ni sawa na 1% ya wakazi lilipaswa kuwa moto sana lakini sasa sawa na kama waliokufa ni sisimizi tu. Wengi wamesema - "Tunasubiri chama mbadala".

Nilipomhoji aliyekuwa mmojawapo wa wagombea ubunge wa CUF aliyebwagwa kimizengwe kwenye kura za maoni, alisema yeye yuko tayari kuingia chama chochote mbadala. "Niko tayari kwenda chama chochote mbadala. Napima upepo tu". Nilipomhoji juu ya mtazamo wake kuhusu CHADEMA kama chama mbadala, alisema: "Tumekuwa tukilijadili hilo na wenzangu hata wengine waliokuwa wakigombea uwakilishi na tunatambua uimara wa CHADEMA hasa katika kusimamia mambo ya kitaifa. Kina viongozi madhubuti na wenye upeo mkubwa kama Dr. Slaa na wengine. Kama kitakuja kujitambulisha vema huku, tutatafakari mwelekeo wakati huko. Sisi hatukuzaliwa na CUF".

PENDEKEZO: Naomba viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wapange namna gani ya kutumia vaccum hii iliyotengenezwa na CUF, ili kuwa chama mbadala katika visiwa hivi viwili.
Hayo ni ya kweli chama mbadala cha kisiasa kinachowafaa Wazanzibari ni CHADEMA, CUF ni CCM B. Wakuu wa CDM changamkieni hiyo deal!!!!!!!
 
Back
Top Bottom